Bank kupiga mnada nyumba.

misasa

JF-Expert Member
Feb 5, 2014
13,919
9,730
Wanajf kuna jamaa yangu alikopa pesa kwenye bank flani ivi vinafanania kama saccos na alichukua muda wa miaka miwili hadi deni lihishe.

Na mkataba wake ulianza desemba 2015 hadi desemba 2017,kalipa rejesho hadi September mwaka wa jana,sasa kuanzia October alipata tatizo akachelewa kulipa kama miezi mitatu ivi.

Sasa mwaka jana November wakampelekea demand note ya siku sitini(sixty days) ambayo imeishia january mwaka huu,mara ghafla akapata mwezi watatu huu akapata pesa kidogo ya kupunguza deni.Sasa anaingiza pesa bank anapata simu siku iyo iyo kwa kiongozi wa serikali wa mtaa kwamba yupo na madalali kwenye nyumba yake.

Akawaeleza yupo bank yao anapunguza wakakata simu akijua wamemuelewa kumbe wana pandika vipeperushi vya tangazo kwenye nguzo za umeme kwamba kesho yake kutakuwa na mnada saa 5 asubuhi.

Sasa katoka kuweka pesa anarudi ndio anapata taarifa tena kwa kusoma vipeperushi katika nguzo za umeme nyumba yake inapigwa mnada kesho.

Sasa anataka kumpigia simu kiongozi wa mtaa simu yake imezimwa,kwaiyo akalala hadi asubuhi ili akaingize tena pesa nyingine mara ghafla gari ya matangazo na madalali wananidisha.

Wanasheria kisheria limekaaje ili?
 
Kisheria hapo imekula kwako. Maana ulishavutuga mkataba na wao walishakupa demand notice ya siku 60 haukurespond so wanatekeleza kinachofuatia baada ya 60 days. Hapo fanya uwapelekee hela zote madalali.

Tambua hapo ilipofikia benki hawana lolote la kufanya wamekabidhi kwa madaali lila kitu
 
Mkuu hamna tena demand note nyingine ya siku kumi na nne kama ya kukumbusha?
 
Hii kwaakili ya kawaida tu Mwenye nyumba alikosea kwasababu unapopewa demand Notice lazima Ujibu tena kwa maandishi ili kuweka kumbukumbu.

Inawezekana huyu kiongozi wa mtaa hakukusudia kuzima simu kwaajili ya suala hilo kwasababu yeye alifanya kupewa taarifa tu
 
Kweli na brother hakutushirikisha mwanzo mambo yamearibika ndio akafunguka ila hapo hakuna utaratibu wowote wa kulipa kwa instalments?
 
Mkuu hamna tena demand note nyingine ya siku kumi na nne kama ya kukumbusha?
Atakuwa alipewa na Bank. Cha msingi hapo alipofikia ni yeye kukubaliana na madalali alipe deni lote na gharama zao. Hii sio issue ya benk tena
 
Bank hua zinacheza na faida tu..kuna bank zingine ni kama zimekaa ki kukwapua kwapua.ukilega tu kidogo wanapata pesa kwako badala ya wewe kupata pesa kwao
 
Atakuwa alipewa na Bank. Cha msingi hapo alipofikia ni yeye kukubaliana na madalali alipe deni lote na gharama zao. Hii sio issue ya benk tena
Ok sawa na nashukuru kwa ushauri wako.
 
Ila muwe makini, wakati wa kuchukua mkopo na kuweka asset yako bond kuna kitu kinaitwa forced sale. In case utakuwa umebakiza kiasi kidogo, usije ukakubali nyumba iuzwe chini ya hicho kiasi. Kisheria hairuhusiwi. Wengi wanauza kwa kiasi kilichobaki kitu ambacho sicho.
 
Niliangalia valuation report waliyomuandalia nimeona hiki kitu na kingine ni market value imefika nafikiri milioni mia na sabini na hiyo forced sale milioni mia lakini cha kushangaza wameuza milioni hamsini na wakati anadaiwa milioni kumi na moja,iyo imekaaje mkuu anaweza kuokoa mali yake kwa sasa?
 
Mkuu unapata hela yako bila wasiwasi. Na moja ya kitu Lukuvi alikuwa anapiga vita ni hii kitu. Tafuta mwanasheria. Au nenda wizarani kabisa!
 
Back
Top Bottom