Informer
JF-Expert Member
- Jul 29, 2006
- 1,582
- 6,627
Asasi za kiraia zinazotetea Haki za Binadamu zaidi ya 18 toka Tanzania zinashiriki mkutano wa 63 wa Tume ya Haki za Binadamu barani Afrika huko Mjini Banjul kuanzia leo tarehe 22 hadi 30 Oktoba 2018.
Kabla ya kuanza mkutano huu, watetezi jana wameadhimisha siku ya haki za Binadamu Afrika wenye ujumbe wa “Pambana na rushwa kama njia ya kulinda Haki za Binadamu”.
Mada mbalimbali zimejadiliwa leo zikiwemo usalama wa Watetezi wa Haki za Binadamu na waandishi, rushwa, haki za watu wenye ulemavu, haki za wanawake, wazee na makundi maalum.
Suala la rushwa limeelezwa kuwa ni adui mkubwa wa haki za binadamu na kikwazo kwa watetezi wa haki za binadamu.
Pamoja na changamoto nyingi za haki za binadamu, watetezi kutoka Tanzania wameeleza kutambua jitihada anazonyesha Rais Magufuli katika kupambana na rushwa. Watetezi hao wameueleza mkutano huo kuwa katika eneo rushwa, Rais Magufuli amejaribu sana kulifanyia kazi na mambo mengi ambayo wamekuwa wakiyalalamikia na kuwashauri marais wengine barani Afrika waige mfano huo.
Changamoto kubwa kwa sasa Tanzania imebainishwa kuwa ni ukiukwaji wa uhuru wa habari, kujieleza na uhuru wa kujumuika.
Aidha, imeelezwa kuwa Demokrasia imeshuka sana nchini huku hali ya watetezi ikizidi kuwa mbaya na ya kuogofya.