Bango la "Mwizi Mkenya!" Mlimani City ni Ubaguzi!, Udhalilishaji!, na Very Undiplomatic Gesture!.

Kutoa taarifa kamili za Muhalifu inasaidia kuweka takwimu za kiusalama na taarifa muhimu za matukio. Kwa hiyo binafsi sijaona kosa hapo. Kuna watanzania wanakamatwa na dawa za kulevya au Uhalifu nchi za watu na hutajwa Utaifa wao. Mara kadhaa kuna majambazi yanakamatwa au kuuwawa na vyombo vyetu vya Usalama huwa yanatambuliwa na kutangazwa kama yametokea Kenya au Burundi......its called standard procedure.

There is NO such thing as a "Diplomatic Gesture" kwenye masuala ya UHALIFU.
 
au mimi ndio sielewi
kwani kaiba au hajaiba?je katoka kenya au hajatoka kenya?
toka lini mwizi akachagua adhabu.
Hivi mnajua uchungu wa kuibiwa kweli? mbona wanaokamatwa njia ya magari ya mwendo kasi na kubebeshwa mabango kama hayo haijalalamikiwa?
 
WE UNASEMA NN ATI? Kwan cha ajabu ni kipi? Huyo si mwizi kweli au kasingiziwa? Au we unatetea wezi?? Na si kweli anatokea Kenya au we ulitaka wezi wote watokee Tandale?
Acha atangazwe ili ajulikane mapema kabla hajaleta madhara zaid ya wizi, Watu wengi tumemjua kupitia hiyo picha, je wasingemtangaza then kesho akakuibia wewe, ungefurahi, au una kahusiano nae hivyo imekugusa??...ngoja na mie niendelee kuituma kwenye magroup ya whatsapp wamjue vizuri ila wawe na tahadhari pindi wamwonapo...huku kwetu wezi wanachomwa moto kabsa..nini kutangazwa bana.. dada unakuwa mwivi kah, SHAME ON HER!!!

word
 
Hapa issue sio huyo mwizi wala utaifa ila mtoa mada ana mengine mbona kachora sana kama mwandishi wa habari...pia nae kamrusha sie tunamuona nae si ataingia katika hii kesi ma vipi?!!
 
Kwako yeye alipokuwa akiiba hadharani, tena katika nchi ambayo siyo take, hakujua kuwa anahatarisha diplomasia baina ya nchi take na waibiwa? He hakujua kuwa anavunja haki za binadam za wenye mali?
 
Maelezo mareeeeefu ati ya kumtetea mwizi, kwa kua ni mwanamke, kwa kua ni mkenya au kwa kua unamjua?

Haki za binaadam my foot, wakati anaiba hakujua kua hatendi haki kwa binaadam wenzie??

Mwizi sio raia wa Tz, kwanini asitajwe utaifa wake??

Amekamatwa papo kwa hapo hlf useme sio mwizi mpk mahakama iseme kwa hiyo alikua anawahifadhia??

Acheni ujinga wenu bhana, msitake kuhalalisha haramu iwe halali, hilo haliwezekani na kamwe halitawezekana.
 
Unafiki ni kitu kibaya sana... Naona watu mnatetea ujinga eti kadharilishwa kwa namna ipi labda?!!.. Mtu kaiba tena mlimani city sehemu ambayo kama umewahi kufika kwa miundombinu ya pale ilivyo mtu huwezi kupakaziwa umeiba... Ukiambiwa umeiba mlimani city wewe ni mwizi kweli huyo sio Wa kwanza madada wengi tu wamekuwa wakikamatwa na wengine hukiri pale pale kuwa waliiba kweli na kutoa mpaka bidhaa hapo hapo.... Acheni kutetea ujinga nendeni duka husika mkachukue video clip ya CCTV camera muone alivyoiba...

Suala lingine kuhusu bango.... Acheni unafiki jamani kwani huyo dada akitolea front page gazetin na kuandikiwa mwizi kutoka Kenya akamatwa m.city kungelikuwa na tofauti ipi na kushikishwa bango....

All in all kiafrika mwizi huna haki mikonon mwa waibiwa.. Huwezi kutuibia halafu utupangie tukufanye nini.

Tena tushukuru hajapgwa fire
 
Nilitaka tu kujua haya:
-Je,sio mwizi?
-Je,sio mkenya?
Kama majibu "SIO" basi wamekosea sana,ila kama ni kinyume chake wako sahihi kabisa.MWIZI ni mwizi tu hata awe m-vietnam.Acheni kutetea wizi kwa kisingizio cha 'Diplomasia',hivi nyie mnajua uchungu wa kuibiwa?

Mwizi hana Diplomasia akija kwako kukuibia acheni ushabiki usio na maana!
 
Huu ni udhalilishaji wa utaifa wake sio kwa wizi wake. Huyu dada katumiwa tu kwa chuki za watu fulani. Inafaa kukemea hii tabia kabla haijafika mbali.
 
Kenyans are "experienced in stealing and perpetuating other crimes", the president has said, during a state visit to Israel.

Uhuru Kenyatta added that Kenya was "20 times more wonderful" than Israel, but "all we ever do is complain".

Kenyans were also abusers, and promoted tribalism, he said, in an address to Kenyans living in Israel.

Mr Kenyatta has been accused of failing to do enough to curb corruption and of stirring up ethnic violence.

His comments were seen as an attempt to encourage Kenyans to develop their country, like Israel, says the BBC's Wanyama Chebusiri in Kenya's capital, Nairobi.
 
Maneno marefu wakati kilichobandikwa ni fact !ni mwizi kweli tena raia wa kenya na hata vyombo vya usalama vita establish hayohayo tena wataenda mbali watamuuliza kabila na imri wake na atokako kenya!Pasco tuache na mwizi wetu na ana bahati ni mkenya tena jike angekuwa mmanzese au mtogole tena me angechezea kibiriti huyo
 
Back
Top Bottom