Bangi yatumika kuendesha ibada Dar,

johnsonmgaya

JF-Expert Member
Oct 16, 2015
2,818
3,725
Wakati serikali ikiimarisha mapambano dhidi ya matumizi na biashara ya dawa za kulevya,
Watu wenye imani za kirastari, ambao hutumia bangi katika ibada zao kama sakramenti, wamesema aina hiyo ya kilevi si mihadarati.

"Bangi ni sakramenti kwa Rastafari, kama diavi katika makanisa ya kikristo.
Inatumika kiroho wakati wa kuomba inatumika kwa kutafakari(meditation) wakati wa ibada" alisema mwenyekiti wa umoja wa marastafari duniani Thau-Thau Haramanuba,
pia Rastafari hutumia bangi kama dawa kwa watoto wanaosumbuliwa na mafua, trachoma na magonjwa mengineyo,

"wakati wa ibada tunatumia bomba maalum linaloshikanishwa na kifuu cha nazi, unaweka mwanzi na hiyo bangi kisha unapitisha kwenye maji, kwahiyo kuna muunganiko wa maji,moto na hewa huu ndio uumbaji wa mungu.
"tunatumia nazi na mwanzi kama sehemu ya udongo,tunatumia moto kuchoma na maji kupoza.Hiyo ni sehemu ya maombi kwenye ibada zetu,unavuta unapitisha kwa mwenzio mnavuta huku mkitafakari.

Akitoa mifano ya watu katika biblia waliokuwa na nywele nyingi(rasta) ni pamoja na yesu kristo, Samson, Ezekiel, yohana, hata mama yake samweli alimwambia mungu kwamba hatanyoa nywele zake mpaka atakapopata mtoto. Pia zaburi 18:8 inaelezea kuhusu kuvuta moto na moshi kwenye pua.

Alisisitiza kuwa mmea wa bangi uliumbwa na mungu na ulikuwepo katika bustani ya eden hivyo haupaswi kubaguliwa.

Alipoulizwa kuhusu sheria zinazoitambua bangi kama dawa ya kulevya , Haramanuba alisema ni kushindwa kuelewa na kwamba tayari nchi kama marekani, jamaica na africa kusini washapitisha na Tanzania inakuja maana imeshaanza kujadiliwa bungeni,

Haramanuba wanaunga mkono serikali kuhusu kupiga vita dawa za kulevya lakini si bangi
"hapana, tutajadiliana na serikali iweje mmea uwe dawa ya kulevya? dawa ya kulevya inatengenezwa maabara, cocaine ni mmea lakini unachakatwa kwenye maabara unaongezewa vitu vingi,
"mtu aliyeathirika na bangi atakuwa amechanganya, vinginevyo haiwezi kukuathiri, mbona watu wanaathirika na pombe na sigara lakini imehalalishwa? Pia kuna panadol na aspirini ni hatari ila tunazipata katika maduka yetu kila siku..

Chanzo: Mwananchi

NB:
hekalu la marasta lipo mto ubungo mkabala na tanesco linaitwa melkizedeck house.
 
[/QUOTE
 
Back
Top Bottom