Wavuta bangi waliokuwa maskani walipokolewa mmoja akatoa ushauri kuwa ukuta ulio mbele yao unawazuia kuwaona manjagu wakija, kwahiyo wausukume wausogeze. Wakavua mashati na flana zao wakawa wanasukuma ukuta, akapita kibaka akaondoka na nguo zile. Mmoja kati ya wavuta bangi kuangalia haoni mashati, akawaambia wenzake: "Washkaji eeeh inatosha tumekwisha ufikisha mbali hamuoni hata nguo zetu hatuzioni? au vipi.