Bandari yetu. Bandari ya salama | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Bandari yetu. Bandari ya salama

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by engmtolera, Jun 20, 2011.

 1. engmtolera

  engmtolera Verified User

  #1
  Jun 20, 2011
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 5,081
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  Ebu fikiria,
  Dar tuna bandari ya asili ( natural harbour) ambayo Mungu hatutozi kodi hata senti moja. Holland inategemea sana Roterdam kama kitega uchumi chake cha maana. ( Roterdam) ni bandari kama ilivyo Dar Es Salaam.

  Wateja tunao wengi sana kuliko hata walivyo nao HOLLAND, wateja hao ambao wanatakiwa wailetee bandari yetu pesa nyingi za kigeni.

  Zipo nchi kama Rwanda, Burundi, Uganda, Congo, na Zambia ambazo hazina bahari hivyo kutegemea sana bandari ya Salama kama geti la kuchukua na kupeleka mizigo yao nje ya nchi. Lakini cha ajabu Bandari ya salama inaonekana ni ya kuchumia watu matumbo yao na si kwa lengo lililokusudiwa la kukuza uchumi,hatuitumii bandari hii salama kama kitega uchumi kwa Taifa letu ila Bandari hii ya Salama inatumika kujaza vitambi vya watu wachache na kumfanya Raisi kulalamika kuwa KUONGOZA NCHI MASIKINI NI TAABU

  Sisi si masikini jamani,tumekosa mtu wa kusimamia mali asili zetu tulizopewa bure na mungu,Tumekosa mipango iliyo bora na hata kama tunayo mipango hiyo basi tumekosa wasimamizi,walio wengi wameweka ubinafsi mbele

  kwa nini tusiwe na mkakati mbadala kama wenzetu wa HOLLAND na kuifanya Bandari hii kuwa ni kitega uchumi cha Taifa na si kichumia tumbo cha wachache?

  Angalia tumeua hadi chuo cha Bandari DSM Kilichopo pale Temeke

  hivi tupewe nini wazungu weusi?


  [​IMG]
   
 2. Sizinga

  Sizinga JF-Expert Member

  #2
  Jun 20, 2011
  Joined: Oct 30, 2007
  Messages: 7,924
  Likes Received: 455
  Trophy Points: 180
  kazi ni kubwa sana iliyo mbele yetu...mi inanisikisha sana jinsi bandari ya Mtwara ilivyosahaulika...ile nduyo bandari yenye Clif nzuri (na ndiyo yenye kina cha asili, hakijachimbwa na mtu yeyote) ukanda wote wa afrika mashariki, lakini nothing comes from it!!
   
 3. Utingo

  Utingo JF-Expert Member

  #3
  Jun 20, 2011
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 7,121
  Likes Received: 185
  Trophy Points: 160
  hiyo picha kama masalia baada ya tsunami ya japani
   
 4. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #4
  Jun 20, 2011
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,767
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  kuu hapo umeongelea kakipande kamoja tuu ka bandali kuna
  1 Gesi asilia
  2 maziwa, mito, na bahari kwa ajili ya uvuvi
  3 Makaa ya mawe Kiwila
  4 Ardhi yenye Rutuba sana
  5 misitu asilia na wanyama weengi
  yaani mkuu hivi vitu vyoote badala ya kuwa ni BARAKA vimegeuka kuwa Ni laana, tunabaki kulialia tuu!
  MUNGU atupe nini jamani hata kama tukiambiwa leo tukaishi dubai tutaichafua tuu jangwa lile!
  MUNGU ATUONGOZE!

  [h=6][/h]
   
 5. engmtolera

  engmtolera Verified User

  #5
  Jun 20, 2011
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 5,081
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  Tena mkuu ebu angalia China kwa sasa wanavyo pambana na Vietnum,Philipines na ambao wanamshilikisha USA ktk mgogoro wa white sea,kila mtu analilia apate angalau kanafasi ka kuweka bandari

  lakini sisi tumeweka siasa mbele na hakuna uwajibikaji,tumefumbwa macho na akili hatuoni hata oportunity iliyoo mbele yetu hususani ktk maswala ya Bandari,kila kitu kwetu ni sawa.

  Tuamke jamani,tumechoka kuwa na viongozi wasiofikilia wala kuona mbali
   
 6. engmtolera

  engmtolera Verified User

  #6
  Jun 20, 2011
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 5,081
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145

  Nina jamaa zangu ni makaburu,jana walikuwa wananieleza kuwa

  wako tayari watanzania wote tuende South Africa na wa kule south Africa waje Tanzania,wakasema tupeni miaka 8 tutakuwa zaidi ya South Africa,

  nikawauliza nyie makaburu kwanini mwa tutusi namna hiyo? wakasema hapana hatuwatusi ila madini tuliyonayo hapa Tanzania yanatisha,wanasema kuna kamkondo wamekagunduwa kapo tz ka madini hakaishi leo wala kesho na wapo mbioni kuja kuwarubuni viongozi wetu na kuingia mkataba wa kuchimba madini hayo

  kweli shamba la bibi
   
 7. Sizinga

  Sizinga JF-Expert Member

  #7
  Jun 20, 2011
  Joined: Oct 30, 2007
  Messages: 7,924
  Likes Received: 455
  Trophy Points: 180
  Dah kama hii ni habari ya kweli basi Mungu atuepushe nayo!!
   
 8. Shark

  Shark JF-Expert Member

  #8
  Jun 20, 2011
  Joined: Jan 25, 2010
  Messages: 20,140
  Likes Received: 7,394
  Trophy Points: 280
  Mbona mnaota mchana kweupe namna hiyo, tuna maliasili nyingi sana kuzidi hata hizo mlizotaja lakin ni kweli hatujui nini tatizo?mbona tunataka kufika peponi lakin hatupendi kufa?inajulikana dhahir tuko hapa kwa ajili ya serikali dhalimu ya CCM, But wangapi wapo tayari kuingia msituni kupambana nayo baada ya kuibiwa kura?Tutaendaje peponi bila kufa kwanza?Hizi ni ndoto hakika!!
   
 9. engmtolera

  engmtolera Verified User

  #9
  Jun 20, 2011
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 5,081
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  MMMMMMMMMH, hilo nalo neno mkuu,kwenda peponi bila kufa? hapana lazima nife kwanza
   
 10. lukindo

  lukindo JF-Expert Member

  #10
  Jun 20, 2011
  Joined: Mar 20, 2010
  Messages: 7,892
  Likes Received: 6,086
  Trophy Points: 280
  [FONT=&amp]nimesoma hii hbari hapa chini pia, ninachojiuliza hizo Trilioni 13 za budget yetu ni hela ndogo!??
  Sasa unatega 50% ya budget yako kwa mambo yasiyo na tija halafu unasema hatuna hela! Tatizo tunashindwa (watawala sio mimi) kujua vipaumbele vyetu na matokeo yake sio ajabu mali zinaozea shambani kwa kukosa wavunaji kama bandari yetu. Ukisema vitu vinaoza (kama Arusha/Tarime/Babati) unapigwa risasi na vijana wa Mwema!


  JK: Ukosefu wa fedha unakwamisha maendeleo Mwandishi Wetu
  Source: Mwananchi.co.tz
  RAIS Jakaya Kikwete amesema ukuaji wa kasi wa uchumi na maendeleo katika Bara la Afrika unakwamishwa na ukosefu wa fedha za kutosha za kugharimia miradi ya maendeleo.
  Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais Ikulu jana, Rais Kikwete alikuwa akizungumza kwenye siku ya kwanza ya mkutano wa Kimataifa wa mwaka huu wa Taasisi ya Smart Partnership Dialogue ambao pia unajulikana Langkawi International Dialogue 2011, ulioanzishwa rasmi mwaka 1995.
  Rais Kikwete alisema kwamba njia za jadi za kupata fedha za kutosha ili kuharakisha ukuaji kasi wa uchumi, hazina uwezo wa kutoa fedha za kutosha kwa ajili ya maendeleo.
  Rais Kikwete alisema kutokana hali hiyo ni lazima nchi za Afrika zitafute namna nyingine mpya ya kugharimia maendeleo ya bara hilo na watu wake.
  "Tatizo ni ukosefu wa fedha za kutosha kugharimia miradi inaweza kuzitoa nchi za Afrika na watu wake katika umasikini kwa haraka zaidi," Rais Kikwete, mjini Kuala Lumpur, Malaysia.[/FONT] ......
   
 11. Ndibalema

  Ndibalema JF-Expert Member

  #11
  Jun 20, 2011
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 10,916
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Kwanini Tanzania bado ni masikini?
  "..SIJUI.."
   
 12. engmtolera

  engmtolera Verified User

  #12
  Jun 20, 2011
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 5,081
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  Lakini kwa Tanzania sisi hatuitaji hiyo misaada,sisi hatuhitaji hizo pesa zitolewe na watu kutoka nje,tuna uwezo wa kukusanya mapato na tukawa na pesa za kutosha kabisa,,Tutambue kuwa Tanzania ni nchi ya 3 Africa kwa kuzalisha ALMASI,yaani ya kwanza ni kwa madiba na wa pili ni ghana na sisi ni wa tatu,je tumefaidika na hilo,je tumeweka mkazo wa kweli ktk kuwabada wawekezaji wa migodi ya madini ili walipe kama wanavyolipa botswana?

  sasa kama hatufuati misingi tuliyojiwekea tutakuwa tukilalama kila siku kuwa miradi haina pesa,huku wao wakiiba almasi yetu na kuendeleza nchi zao
   
 13. Tanganyika1

  Tanganyika1 JF-Expert Member

  #13
  Jun 20, 2011
  Joined: May 10, 2011
  Messages: 396
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 45
  tanzania sio maskini, ila watanzania ndo maskin...jiulize wewe na vijana wenzako, baba yako mnasoma mkiwa mnalenga kuajiriwa, miaka inapita hujapata ajira bado una ngangania kuomba kazi. Huo ndo umasikini.....maana kuna tofauti ndogo sana kati ya MTUMISHI NA MTUMWA....Inuka kijana, tafuta idea, join forces, and come up with somethng new. Familia yako/zenu zitakua kiuchumi, then jamii yenu na mwisho taifa.....tusibaki kulalamika tu.
   
 14. engmtolera

  engmtolera Verified User

  #14
  Jun 20, 2011
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 5,081
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  hehehehehehehehehe
  Familia zetu zitainukaje nasi hatujawezeshwa? vikwazo vingi walaji wengi ni vipi si tutasonga? hebu jaribu kufuatilia kwa undani juu ya zile pesa za Raisi kikwete je waliofaidika nazo ni kweli wanastahili ama walistaili kupata hizo pesa?


  Kazi kubwa tunazofanya lakini PESA kidogo,kama KULIMA watu wanalima lakini soko bado halikidhi mahitaji,

  sasa nani wakulaumiwa hapo? unataka tujitoe roho?
   
 15. Shark

  Shark JF-Expert Member

  #15
  Jun 20, 2011
  Joined: Jan 25, 2010
  Messages: 20,140
  Likes Received: 7,394
  Trophy Points: 280
  Na nchi ya kwanza na pekee inayozalisha Tanzanite Duniani,
  Misitu ipo kibao tu kama pande, kazimzumbwi n.k, tukiamua kuingia msituni hatutakosa misitu ya kujificha kupanga ukombozi wetu, ni sisi tu kukubali kufa ili tuingie huko peponi
   
Loading...