Bandari yasaka meli 65 zilizotoweka

Bandari yasaka meli 65 zilizotoweka

Shehe...mwezi uliopita nilimjuzeni kwamba bado dili zapigwa kimyakimya tena night....ikaonekana ni BHANG ingawa nalivuta.
Jombaa bhangi hata mimi nalipuliza..ule mmea ukiutumia vizuri ni chemchem ya hekima na utulivu wa akili
 
Iyo atakuwa kaitoa kwa CAG report sidhani kama ni tukio la ivi karibuni meli 65 sio kazi ndogo kupakua.
Wakwepa kodi apo wanahaha hasa wale ambao meli zinawahusu.
Bandari yetu ilikuwa busy kumbe meli zingine ni za wapigaji.
 
Iyo atakuwa kaitoa kwa CAG report sidhani kama ni tukio la ivi karibuni meli 65 sio kazi ndogo kupakua.
Wakwepa kodi apo wanahaha hasa wale ambao meli zinawahusu.
Bandari yetu ilikuwa busy kumbe meli zingine ni za wapigaji.

..labda kuna rekodi kwamba meli[65] zimetia nanga.

..lakini hakuna rekodi za kuonyesha kiasi cha kodi kilicholipiwa na meli hizo.

..kwasababu haiingii akilini meli ya kwanza, ya pili,...mpaka meli ya 65 zinapotea na watendaji wapo tu. halafu hata huko " kupotea" kwenyewe hatuelezwi Raisi alimaanisha nini.
 
Duuh kweli nchi hii inaongozwa na
watu 2 tu, wengne wapo km picha
 
Duh meli za PIRATES hizo.
Wahusika au meneja au mkurungenzi alikua wapi?
 
Labda kila meli ilikuwa inashusha balo moja la mitumba na kuondoka, lakini meli 65 zishushe mzigo wa haja ni foleni na msongamano hapo bandarini, au hizo meli zilishusha mizigo kipindi tofauti kipindi cha mzee wa tezi tume
berth 7 =parking za meli 7

berth 7 (meli 7) x siku 8 = meli 56.
simple mathematics.

kitendo cha siku 8. tu meli 56
 
Endelea kushangaa niliposikia twiga amepandishwa ndege kwenda nje ya nchi mlishangaa.Mliposikia makontena zaidi ya 2000 kupotea mkashangaa sasa mnashangaa nini meli 65 kupotea bandarini nenda mkashangae #ferry
 
Kuna ile Rada ilinunuliwa na Mkapa tukaambiwa uwezo wake sijui nini Afrika nzima ,vipi haiwezi kutumika kusaidia hapo bandari ? Au ipo kwenye makumbusho ya Taifa wanaipiga kama gitaa si ina nyuzi nyuzi ile ?
Watu wengne humu wao ni kutoa tu burudani….. Sawa bhana
 
Hizo meli zimekuwa mitumbwi ziingie kwa wingi bila kujulikana.

Magafuli anatakiwa aanze na hiyo aliyotoa hiyo idadi za meli.

Kajuaje kama meli 65 zimeingia kimya kimya.
kashangae #ferry tunaposema CCM ni janga la taifa mtakuwa mmeshaanza kutuelewa
 
Hata hao waliompa Rais taarifa ni majipu. Inawezekanaje washindwe kumpa Rais taarifa wakati ipo meli moja pekeyake mpaka wasubiri 65?.
 
berth 7 =parking za meli 7

berth 7 (meli 7) x siku 8 = meli 56.
simple mathematics.

kitendo cha siku 8. tu meli 56


siku 365 (mwaka 1) x miaka 9 = ????????????????
why not
 
Nchi hii iliharibiwa sana.Kubadilika ghafla ni ngumu ila kwa kuwashikisha adabu wahusika wa namna hii.Nchi hii haikuwa na viongozi hapo nyuma.
 
MAMLAKA ya Bandari Tanzania (TPA) imesema inatafuta taarifa kuweza kubaini meli zaidi ya 65 zilizoingia na kushusha mizigo nchini bila kulipa kodi.
Hiyo ni baada ya Rais Dk. John Magufuli, kueleza madudu aliyoyakuta ndani ya Bandari ikiwamo jinsi meli 65 zilivyoingia na kushusha mizigo bila kulipa ushuru wa Serikali.

Mkurugenzi wa Mipango na Uwekezaji wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), Gladson Urioh, alisema tangu Rais Magufuli alipotoa kauli hiyo hivi karibuni akiwa wilayani Chato, Mamlaka imekuwa ikifuatilia taarifa hizo.

“Hili suala la meli zaidi ya 65 kuingia na kutolipa kodi tunalifuatilia kwa undani sisi TPA pamoja na wadau wote vikiwamo vyombo vya ulinzi.

“Bandari ina wadau wake ambao ni pamoja na vyombo vya ulinzi, Mamlaka ya Usafirishaji wa Majini na Nchi kavu (Sumatra), Shirika la Viwango Tanzania (TBS), Mamlaka ya Dawa na Chakula (TFDA), Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Maji (Ewura), Idara ya Uhamiaji, Idara ya Afya na Mkemia Mkuu wa Serikali na wengine.

“Tunaamini kwa umoja wetu huu tutapata taarifa kwa undani kuhusu suala hili la meli,” alisema Urioh.

Wiki iliyopita akiwa wilayani Chato, Rais Dk. John Magufuli, alifichua zaidi madudu ndani ya Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) akieleza jinsi meli 65 zilivyoingia na kushusha mizigo nchini bila kulipa ushuru wa Serikali.

Alisema meli hizo zilishusha mizigo katika Bandari ya Dar es Salaam na baada ya kupakua mizigo hiyo ziliondoka bila kujulikana zimekwenda wapi.

“Ndugu zangu tusipochukua hatua nchi itatushinda leo (juzi) pale bandari zimeingia zaidi ya meli 65 zimeshusha mizigo na hazikuonekana, hivi inawezekana vipi meli ishushe mizigo na kutokomea bila kulipa mapato ya Serikali?

“Meli zilileta mizigo zikashusha na zikapotea hivyo hivyo na Serikali ikakosa hela. Jamani ndani ya Serikali kuna madudu ya kila aina hivyo ninawaomba mniombee, nimejitoa sadaka kwa ajili ya Watanzania,” alisema Rais Magufuli huku akishangiliwa.

Source: Mtanzania
Namuomba Rais Magufuli asiwe na huruma kabisa na hii mijizi iliyojificha katika kimvuli cha ajira.
 
meli hazikulipa au hela iliyolipwa haikuingizwa kwenye kumbukumbu za bandari ?
 
Hizo meli zimekuwa mitumbwi ziingie kwa wingi bila kujulikana.

Magafuli anatakiwa aanze na hiyo aliyotoa hiyo idadi za meli.

Kajuaje kama meli 65 zimeingia kimya kimya.





Kamuulize baba yako mzee wa msoga(vasco da gama) maana zimepotea kipindi chake
 
Hizo meli zimekuwa mitumbwi ziingie kwa wingi bila kujulikana.

Magafuli anatakiwa aanze na hiyo aliyotoa hiyo idadi za meli.

Kajuaje kama meli 65 zimeingia kimya kimya.
Najua nyie ndio majambazi-fisadi ya bandarini. Mlikuwa mmezoea mlegezo wa legelege wa Msoga, mswahili mwenzenu. Onyo: Bandarini sasa kuna mashushu wenye uchungu na hii nchi, wazalendo na wamejaa kila kona. Mtaumia na mtapotea!
 
Back
Top Bottom