Bandari yasaka meli 65 zilizotoweka

Bandari yasaka meli 65 zilizotoweka

pale bandari zimeingia zaidi ya meli 65 zimeshusha mizigo na hazikuonekana
Zimezama au..
hii ni kashfa kubwa mno.hajatutajia mabilioni yalio potea..vipi CRDB wanahusika ?
 
Kuna ile Rada ilinunuliwa na Mkapa tukaambiwa uwezo wake sijui nini Afrika nzima ,vipi haiwezi kutumika kusaidia hapo bandari ? Au ipo kwenye makumbusho ya Taifa wanaipiga kama gitaa si ina nyuzi nyuzi ile ?
 
Labda kila meli ilikuwa inashusha balo moja la mitumba na kuondoka, lakini meli 65 zishushe mzigo wa haja ni foleni na msongamano hapo bandarini, au hizo meli zilishusha mizigo kipindi tofauti kipindi cha mzee wa tezi tume
 
Tushukuru Mungu, maana upinzani pia usingeweza hata nusu ya haya. Hii kuwa anawaambia watu ni staili nzuri sana. Maana wananchi wanapokuwa na mwamko na kujua kinachoendelea, ndipo tu atakapofanikiwa kupambana na mafisadi waliokubuhu. Sidhani kama kuna ufisadi kuzidi huu, labda Nigeria!
 
Hapo aliyempa magufuli taarifa inafaa atumbuliwe..iweje ampe taarifa meli zikishaondoka.
 
Miafrika hatuwezi kuendelea mpaka Yesu atakapo rudi, kuna watu wana degree za kuiba makontena pale bandarini na wameajiriwa kwa ajili hiyo!!!
 
Bado najiamini kutoukubali utendaji wa mh.jpm na sasa napata picha na maana ya neno hapa kazi tu inamaana kazi kuchukua na kuendelea kula msisha jpm vinyago kachonga mwenyewe lakini vinamtisha balaa
 
Labda kila meli ilikuwa inashusha balo moja la mitumba na kuondoka, lakini meli 65 zishushe mzigo wa haja ni foleni na msongamano hapo bandarini, au hizo meli zilishusha mizigo kipindi tofauti kipindi cha mzee wa tezi tume
Rais kasema leo yaani juzi akiwa rubondo na odinga. Hata hivyo ni kama miujiza hivi make anadai ilishushwa ndani ya Masaa machahe.
 
Dah binadam bana licha ya kutumbua jipu na takukuru kupewa makucha yani mibongo bado tu haijali inazid kupiga dili. Swali langu ni hili kama hizo meli zimefanya hivyo wakati huu wa Magu je wakati wa dhaifu ilikuwaje?? Tumpeni rais sapoti jaman na kila mara awe anchek BP asifanye maamuz ya ghafla ya wadau kulishwa

RAIS KAMA ANATAKA SAPOTI BASI.NI KATIBA MPYA YA WANAINCHI ILIOANDALIWA NA JAJI WARIOBA
 
Watanzania sasa ngoja tuwasaluti tu maana hamna jinsi!
Pale TPA hatakiwi abaki mtu wa zamani, mfumo ni mkubwa sana! Ukibadilisha watatu ukaacha wengine ni zero work.
 
Rais kasema leo yaani juzi akiwa rubondo na odinga. Hata hivyo ni kama miujiza hivi make anadai ilishushwa ndani ya Masaa machahe.
Ebu naomba rais wangu awe anatulia kidogo na kusubiri taarifa za kina, yaani meli zimepotea vooooooooom baada ya kushusha mzigo??
Naona Majaliwa kaamua achune sasa.
 
Magufuli anapaswa kujiuzulu haiwezekani meli 65 zishushe mizigo ziyeyuke halafu aombe wananchi tumuombee wakati ameshindwa kazi

SIO MELI ZA SASA HIVI ILA NI KABLA YA HAPO.TUMIENI UBONGO KUELEWA
 
Mshauri wa rais ni mtu mwenye akili nyingi sana kuliko rais mwenyewe na ni mtu ambaye hamtakii mema rais.

Ukisoma majibu ya mamlaka ya bandari kwa undani ni kwamba mamlaka inambishia rais kwamba hakukuwa na kitu kama hicho na kwamba ulinzi uliopo na taratibu zilizopo kamwe meli 65 zisingeshusha mzigo na kutoweka.

Mimi naamini anayempa rais habari hana nia njema naye na kwa ajabu rais hafanyi verification za habari anazopata. Tumeona sehemu nyingi akidanganywa hadi kufanya maamuzi ambayo baade anayabadiri. Mfano, kusitisha ujenzi wa bandarini ya bagamoyo, wafanyakazi hewa BoT, wakurugenzi wanaolipwa 36M, kupiga marufuku uingizaji sukari, nk. Ifike wakati rais awe na uhakika na anachoambiwa na ajiridhishe, raia wa Tz anamshangaa rais anaposema kuna meli 65 zimeshusha bila kulipa kodi kipindi hiki ambacho wakusanya kodi wako macho zaidi. Mwananchi wakawaida anajiuliza kwanini usalama wa taifa unaompa rais taarifa hizo haukuwapo wakati meli zikifunga Nanga? Huyo aliyempa taarifa hizi bado amebaki kazini?
 
Back
Top Bottom