Bandari na kituko cha taifa

Ni bora Kina Bashiru wangepindua meza mwanzoni kabisa haya yasingetokea.

Huyu bibi kashasimika mifumo yake sasa anajifanyia tu anachotaka
Nchi ilitakiwa iwe na uongozi wa mpito baada ya msiba kisha ufanyike uchaguzi mkuu
 
Kwa hili JPM ana kila sababu ya lawama....Alidhani yeye Mungu? Ameondoka sasa na kutuachia madhila haya...Mungu amsamehe lakini amelikosea sana taifa hili kwakufanya vile
 
Ni bora Kina Bashiru wangepindua meza mwanzoni kabisa haya yasingetokea.

Huyu bibi kashasimika mifumo yake sasa anajifanyia tu anachotaka
Kumbaka bado kuna Mungu na atatenda tena kwa moto ulao...Just wait and see how things turn arround!

Hakutakuwa na mvua wala jua ila kwa neno langu...Nimerudi mazima na nguvu ya kuvunja kuharibu na kuteketeza tujenge upya...
 
Kwa hili JPM ana kila sababu ya lawama....Alidhani yeye Mungu? Ameondoka sasa na kutuachia madhila haya...Mungu amsamehe lakini amelikosea sana taifa hili kwakufanya vile
Kwa uwezo wake wa kiutendaji hakuhitaji kabisa kuwa na hofu mpaka kutengeneza bunge la namna hii, kiukweli bunge lililopo ni takataka kabisa
 
Inamaana mapungufu yaliyomo kwenye mkataba wwabunge hawakuyaona au msemo wa tibaijuka bundi kapenya bungeni
 
Nchi ilitakiwa iwe na uongozi wa mpito baada ya msiba kisha ufanyike uchaguzi mkuu
Hili ni kosa la kiufundi kabisa, kiongozi kukaa kwenye nafasi ambayo hakuchaguliwa kwa miaka minne bila kuitisha uchaguzi ni kutowatendea haki wananchi. Ndo maana nchi zilizoendelea kiongozi akionekana kupata upinzani kupitisha sera zake anaitisha uchaguzi wa mapema kutafuta kuungwa mkono. Lakini bongo hata uchaguzi ukifanyika unaishia kunajisiwa na chama twawala kwa hiyo huwezi kupata picha halisi ya kiongozi kukubalika.
 
Mkuu umeongea vizuri sana. Nchi hii imefika hapa kwa sababu ya upuuzi wa CCM na kitendo chake cha kuwafuga mafisadi wanaoisumbua na kuiangamiza nchi kwa maslahi finyu ya kutunisha matumbo yao mapana yasiyoshiba. Kwa hapa tulipofikia hakuna namna nchi inavyoweza kuondoka kwenye mkwamo pasipo wananchi kuchukua maamuzi ya kuwaondoa hawa panya madarakani ifikapo 2025 wasiendelee kuguguna rasilimali za taifa. Tukiendelea kuwachekea sio tu tutavuna mabua bali nasi tutauzwa kwa waarabu na mabeberu.
 
kwa kweli hii ni point kubwa sana, intely yangu imeshaniambia kuhusu hilo
 
Najua Athari ya Mapinduzi ya kijeshi.
#Ila Hii Nchi inahitaji MAPINDUZI TU YA KIJESHI.
No Matter Maumivu gani tutapata ila afadhali waondoke wadhalimu hawa.
 
Najaribu kuuliza? Hivi Tanzania kuna majaji waadilifu wa kulinda rasilimali za Taifa?
Kama hata mahakama ya rufaa ina bariki wakurugenzi makada wa Ccm wasimamie uchaguzi wa vyama vingi najiuliza kuna haki wapi?
Kama wabunge wanao jiita wabunge wanajua walifikaje pale mjengoni wako hapo kwa mchongo wana bariki hujuma za serikali badala ya kuisimamia serikali tutegemee nini?
Badala ya kuchambua vifungu vya mkataba kwa hoja wao wana anzisha kikundi cha sanaa ndani ya bunge kupeleka mipasho kwa umma hii si dharau?? Nchi imeuzwa!!!!
 
Dua la kuku halimpati mwewe.Pigeni kelele weeee!Lakini nchi nilazima iende mbele na ushirikiano wa Tz na Dubai ndiyo umeishapita.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…