Bandari na kituko cha taifa

Bandari na kituko cha taifa

Nimesikiliza Clip ya Waziri Mkuu inayo trend, naye amejikita kutetea Mwekezaji, lakini anasahau Watu wanahoji aina ya Mkataba.
 
  • Thanks
Reactions: Ame
Duh! Mi kila siku nafikiria walivyotuaga kwamba wanaenda kwenye maonyesho ya biashara na walivyorudi hawakutwambia kwamba tayari wameshauza bandari zote.

Mara paaaa.. Nikaona jengo refu Dubai lina picha ya mama nikajua tayari Dubai wameshangilia goli hata kama hatujaona mechi yenyewe.
 
Tabia yao nyingine wanayofanana ni uvivu, hawa wote hawawezi kuhangaisha vichwa vyao, wao kila jambo ni kuwaachia wasaidizi wao, matokeo yake sasa nchi imetolewa sadaka huku tukijiita tuna kiongozi, hapana, mimi nasema nchi kwa sasa haina kiongozi, inajiendea tu, kama ilivyokuwa "auto-pilot" enzi za JK.
UVIVU. Sawa kabisa!
 
Binafsi nataka Rais ajiuzulu au aondolewe kwa kura, hafai

Mi nitawaelewa tu siku mkiunganisha kelele hizi na yale yanayotokea migodini kwa wawekezaji wazungu........wanaenda kutua huko na ndege zao (hatujui katu zinabeba nini zinapokuja ikizingatiwa kuwa wao huko makwao wana makampuni kabisa ya kutengeneza silaha (biashara yenye faida kuliko zote navyosikia)) na ndege zao zinaondokea hukohuko baada ya kubeba mzigo (km ni madini pekee au kuna vingine, ni wao na wapinga mkataba wa bandari kina tibaijuka na Dr slaa ndo wanajua).

Kama hiyo haitoshi, mchanga wenye madini unabebwa na kupelekwa huko kwa wazungu kuchambuliwa kisha ndo wanatuambia kuwa katika mchanga uliojaa katika contena fulani, tumepata grams 2. Najua, taarifa hiyo hupokelewa na maneno, 'Praise the Lord!' na kina Dr slaa na kadinali Pengo huku kina prof Tibaijuka na takataka zingine humu huitikia kwa shangwe, ''Aamin!" na makofi juu.

Kama vp tuanze upya kwa kila kitu, lkn biasness kwa misingi ya kiitikadi tu haki ya nani tutakwama. Yakiisha maandamano yenu ya kupinga uwekezaji wa bandari, yatafuata maandamano mengine ya kupinga mikataba ya hovyo ya madini na gesi.....we subiri tu utaona!
 
Uongozi wa awamu hii na ule wa awamu ya 4 ni mapacha
Nakazia.
Hata staili ya uongozi wa Mama nadhani itakuwa ni ushauri 100% kutoka kwa JK mfano sasa hv kaja na ile ya kuweka pamba masikioni asisikie kelele za wananchi...JK yeye alikuwa anajisemea ni upepo tu utapita!
Serikali imewekwa mfukoni na kikundi cha watu fulani, we umewahi kusikia wapi duniani eti safari ya Rais inafadhiliwa na watu binafsi, rejea Royal Tour kule Marekani...badae akasema eti tutaambiwa majina ya wafadhili wa safari hadi leo anaona aibu kuwataja!.
 
Nilimsikiliza mwanasheria Mama mmoja wa Kenya akidadavua jinsi ambavyo Nchi yetu inaingizwa chaka ktk mkataba huu, lakini nikajisemea moyoni kwamba Kenya wana hofu na mafanikio ya Bandari yetu endapo biashara hii itakuwa postive, kwa maana port ya Mombasa na Lamu ni competitor wetu, japo hakuna aliyewahi kutoboa bila ku take risk lakini naanza kuona umuhimu wa kuwasikiliza wanaNchi kabla ya kulipeleka jambo hili haraka haraka.
jambo hili la bandari na kujengwa kwa bandari ya Bagamoyo ambayo JPM aliikataa ni pacha, na maelezo ya PM siamini kwamba suala la DP world linaanzia kwenye DUBAI TRADE FAIR, Hi inaanzia awamu ya Nne na inawezekana kuna ahadi inayosubiliwa kutimizwa na ninaanza kuona azima ya ulazima wa kubadilisha ikologia ya majabu ya dunia ya wanyama kuishi na wanadamu kwa kusudi linaloonekana jema la kuwahamishia Msomera ili Ngorongoro ibakie huru, tusisahau ile kelele ya awamu ya Nne ya kusafirisha wanyama hai kupelekwa nje. kIla kiongozi ana historia yake, iwe njema au mbaya, vizazi vijavyo vitatoa hukumu.
niseme Mama Samia imalize hiyo ahadi tusije kukaa tunaogopa ogopa kumbe huko mbele kuna mambo mema, kama mabaya itakuwa agenda ya historia yako, vilio vya Watanzania huko mbele yakitokea machafuko machozi yatakuwa yetu wote ikitokea neema itakuwa yetu wote hivyo Samia fuata dhamira ya sauti ya Mungu inayonong'oneza moyo wako. ya kuambiwa weka pembeni yasitengeneze hukumu yako.
 
Kila siku nazidi kuiona connection iliyopo kati ya JK na Samia, kwenye mambo mabaya kabisa yanayoliumiza hili taifa.

Kuanzia kwenye udhaifu uliokuwepo awamu ile ya JK mpaka sasa tunauona udhaifu uliopo awamu hii ya Samia, hawa wote wanafanana kwa namna mbaya kabisa ya kuliangamiza hili taifa.

Hapa ndipo Samia anapokosea na hataki kujirekebisha, kumgeuza JK kuwa ndie "think tank" wake, matokeo yake sasa ameanza kubeba uozo wote uliobaki kichwani mwa JK ambao hakupata muda wa kuutekeleza awamu yake, huyu Samia ndio anautekeleza sasa, na inawezekana kabisa anautekeleza kwa manufaa ya JK pia.

Tabia yao nyingine wanayofanana ni uvivu, hawa wote hawawezi kuhangaisha vichwa vyao, wao kila jambo ni kuwaachia wasaidizi wao, matokeo yake sasa nchi imetolewa sadaka huku tukijiita tuna kiongozi, hapana, mimi nasema nchi kwa sasa haina kiongozi, inajiendea tu, kama ilivyokuwa "auto-pilot" enzi za JK.
Unaijua GDP ya tz kabla na baada ya jk!?..GDP huja tu bila uongozi thabiti!?..au umekula sakrament ukashushia divai,unajamba chuki tu now!?
 
Hivi Tulia spika wa Bunge haoni aibu kwa yanayoendelea? Ilitakiwa pale serikali iagizwe kurekebisha baadhi ya mambo ndipo waendelee kupitisha azimio, pale hata kama sio mwanasheria lakini bado utaona mapungufu ya wazi kabisa yaliopo
Hata mimi najuliza hilo swali
 
Mi nitawaelewa tu siku mkiunganisha kelele hizi na yale yanayotokea migodini kwa wawekezaji wazungu........wanaenda kutua huko na ndege zao (hatujui katu zinabeba nini zinapokuja ikizingatiwa kuwa wao huko makwao wana makampuni kabisa ya kutengeneza silaha (biashara yenye faida kuliko zote navyosikia)) na ndege zao zinaondokea hukohuko baada ya kubeba mzigo (km ni madini pekee au kuna vingine, ni wao na wapinga mkataba wa bandari kina tibaijuka na Dr slaa ndo wanajua).

Kama hiyo haitoshi, mchanga wenye madini unabebwa na kupelekwa huko kwa wazungu kuchambuliwa kisha ndo wanatuambia kuwa katika mchanga uliojaa katika contena fulani, tumepata grams 2. Najua, taarifa hiyo hupokelewa na maneno, 'Praise the Lord!' na kina Dr slaa na kadinali Pengo huku kina prof Tibaijuka na takataka zingine humu huitikia kwa shangwe, ''Aamin!" na makofi juu.

Kama vp tuanze upya kwa kila kitu, lkn biasness kwa misingi ya kiitikadi tu haki ya nani tutakwama. Yakiisha maandamano yenu ya kupinga uwekezaji wa bandari, yatafuata maandamano mengine ya kupinga mikataba ya hovyo ya madini na gesi.....we subiri tu utaona!
Nakubaliana na wewe...Hata hayo madini yaunganishwe humo humo mikataba yake kuidai iwe reveiwed, tuanze upya...Hapa kama taifa tumekwama, tunahitaji utashi wa dhati kulikwamua taifa bila kujali dini, itikadi ama kabila...At the end we are all Tanzanians
 
Nimesikiliza Clip ya Waziri Mkuu inayo trend, naye amejikita kutetea Mwekezaji, lakini anasahau Watu wanahoji aina ya Mkataba.
Hana la kufanya kwakua huwezi kutetea kitu ambacho ni obviously hakina substance
 
Hapa kwakweli hawa hitoria itawakumbuka kama akina Mangungo...What a shame!
Shida ya wabunge wetu ni kutokutana na wananchi, wao muda wote wako kwenye biashara zao, wakitoka huko hawana jipya, ni wakati sasa bunge lipunguzwe ukubwa wake liwe controlled na wananchi na ikitokea mbunge hana ufanisi basi aondolewe bila kujali kama muda wake umekwisha au la
 
Nimemskiliza Fr. Charles Kitima, nimemsikiliza Dr. Wilbroad Slaa, nimemsikiliza Adv. Boniface Mwambukusi, nimemsikiliza Mange Kimambi, nimemsikiliza Rostam Aziz, nimemsikiliza Tundu Lissu, nimemsikiliza Freeman Mbowe.

Nimelisikiza Bunge, nimemsikiliza RC Albert Chalamila, nimemsikiliza Rais Samia Suluhu Hassan, nimeskiliza Gerson Msigwa Msemaji wa Serikali, na nimemsikiliza Salim Asas; to mention a few.

Baada ya kuwasikiliza, nimetafiti, nimelinganisha, nimetofautisha kauli zao, fikra zao, hoja zao, na matendo yao, nikapata majawabu haya:

1. Mkataba wa Bandari haujitetei wenyewe, ni mkataba wa kifisadi unaohitaji nyongeza ya maneno ili uwe halali na ukubalike kwa Watanzania. Watanzania wameukataa.

2. Nchi kwa sasa haina uongozi madhubuti; nchi inajiongoza yenyewe.

3. Kuna kikundi cha wahuni wachache wanapora rasilimali za nchi na wanaziweka kwenye mikono ya wageni kwa jina la uwekezaji.

4. Katiba ya nchi na sheria za nchi zimeanajisika. Utawala bora na utawala wa sheria umetoweshwa kwa ulafi wa maslahi ya watu binafsi.

5. Taifa linahitaji hatua za haraka na dharura kuikwamua nchi na machafuko yanayoweza kutokea muda wowote kuanzia sasa. Umaskini umekithiri, achilia mbali pengo kubwa la walionacho na wasio nacho linavyoongezeka kwa kasi.

6. Wakati umefika raia wote wa Tanzania kuamka kudai haki ya nchi yao. Kurejesha mamlaka, madaraka, na nguvu mkononi mwao kutoka kwa viongozi walioko madarakani.

7. Naunga Mkono Mawakili wazalendo Adv. Emmanuel Chengula, Adv. Boniface Mwambukusi, Adv. Livino Ngalimtumba, na Adv. Alfonce Lusako wanaokusudia kufungua kesi Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam "Under Extreme Certificate of Urgency" ili Mahakama ikatupe tafsiri ya huu mkataba unaweka rehani usalama wa nchi. Bunge la JMT limewasaliti wananchi badala ya kuisimamia serikali. Iingie mikataba mizuri, Bunge limegeuka kuwa "Genge la serikali" la kupingana na wananchi.
 
Attachments

  • 6FAA82CE-F3F5-49E4-92EF-D6657E342487.jpeg
    6FAA82CE-F3F5-49E4-92EF-D6657E342487.jpeg
    26.4 KB · Views: 2
  • 2C37D26F-428D-4F25-A22B-5A9EE53ABF5B.jpeg
    2C37D26F-428D-4F25-A22B-5A9EE53ABF5B.jpeg
    48.5 KB · Views: 2
Nakubaliana na wewe...Hata hayo madini yaunganishwe humo humo mikataba yake kuidai iwe reveiwed, tuanze upya...Hapa kama taifa tumekwama, tunahitaji utashi wa dhati kulikwamua taifa bila kujali dini, itikadi ama kabila...At the end we are all Tanzanians
Kabisa mkuu
 
Back
Top Bottom