Bana wa REDET aibukia huku tena | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Bana wa REDET aibukia huku tena

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Lunyungu, Dec 19, 2009.

 1. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #1
  Dec 19, 2009
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Date::12/19/2009Ahadi za urais 2005 zamtesa Kikwete uchaguzi wa mwakani[​IMG]Na Mwandishi Wetu

  MIEZI michache ikiwa imebaki kabla ya kuanza kwenda kwa wananchi kuomba ridhaa ya kuongoza nchi kwa kipindi kingine cha miaka mitano, Rais Jakaya Kikwete anaonekana kukabiliwa na mzigo mzito wa kutekeleza ahadi nyingi alizozitoa wakati wa kampeni za mwaka 2005.

  Kikwete alipata ushindi wa kishindo kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka 2005 baada ya kunyakua takriban asilimia 80 ya kura, akiwa pia ameshinda kwa kishindo dhidi ya wapinzani wake kwenye uteuzi wa mgombea wa CCM.

  Lakini kadri muda unavyokwenda ndivyo umaarufu wake unaonekana kupungua huku tafiti mbalimbali zikionyesha kuwa umaarufu aliokuwa nao wakati akiingia madarakani unaendelea kuporomoka, ikiwa ni miezi tisa kabla ya uchaguzi mkuu wa mwakani.

  Wakati akizunguka sehemu mbalimbali nchini kuomba kura za wananchi, Kikwete alikuwa akitoa ahadi kem kem ambazo alizielezea kwa kifupi kwenye kauli mbiu yake ya “Naisha Bora kwa Kila Mtanzania” ambayo mkakati wake wa kuitekeleza ulikuwa ni “ari mpya, nguvu mpya na kasi mpya”.

  Mbali na ahadi ambazo alikuwa akizitoa kwa wananchi kila sehemu alipoelezwa tatizo, ikiwa ni pamoja na matatizo sugu ya maji, miundombinu, huduma za afya na pembejeo, Rais Kikwete pia alitoa ahadi za ujumla kabla na baada ya kushinda uchaguzi kumrithi Benjamin Mkapa.

  Baadhi ya ahadi hizo za Rais Kikwete kabla na baada ya kuingia madarakani ni pamoja na kuweka kipaumbele katika kilimo, akitumia kaulimbiu ya Kilimo Kwanza, kupitia upya mikataba ya madini ili inufaishe nchi na wawekezaji, na kuhakikisha kuwa hakuna mwanafunzi wa elimu ya juu anayekosa masomo kwa kukosa karo.

  Ahadi nyingine ni pamoja na ujenzi wa vyumba vya madarasa katika shule za umma, kuumaliza mgogoro wa Zanzibar, kuimarisha uhusiano wa kimataifa, kukomesha tatizo la ufisadi, kupambana na tatizo la uhalifu, ikiwa ni pamoja na biashara ya dawa za kulevya na ujambazi, kuandaa mdahalo wa kitaifa wa michezo kwa lengo la kuinua michezo na ujenzi wa Chuo Kikuu cha Dodoma.

  Lakini wasomi na wachambuzi wa mambo ya kisiasa wanaona kuwa ahadi nyingi hazitekelezeki na nyingi hazijawekewa mkakati wa kuzitekeleza na hivyo wanaona zitakuwa mzigo kwa mbunge huyo wa zamani wa Chalinze.

  Kwa mujibu wa uchunguzi uliofanywa na Mwananchi Jumapili, tayari ahadi hizo zimeanza kumtesa Rais Kikwete imeaanza kumtesa na kumpotezea umaarufu mbele ya wananchi, huku mjadala juu ya udhaifu wake katika utendaji kazi ukizidi kupamba moto.

  “Ahadi ya maisha bora kwa kila Mtanzania ilikuwa ni ndoto ya kisiasa,” anasema mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dk Benson Bana alitakiwa na Mwananchi Jumapili kutoa maoni yake kuhusu ahadi za Rais Kikwete.

  Dk Bana alisema pamoja na kuwa serikali imejitahidi katika suala la elimu, imekosea katika suala la elimu ya watu wazima kwa kuwa imeachwa na haijapewa kipaumbele.

  “Elimu ya watu wazima ingekuwa imepewa kipaumbele, tusingekuwa tunazungumzia elimu ya kilimo kwanza kwa kuwa wananchi wangekuwa hivi sasa wanafundishana wenyewe.”

  Dk Bana, ambaye pia ni mwenyekiti wa Taasisi ya Utafiti wa Elimu ya Demokarsia ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (Redet), alisema baadhi ya ahadi hizo hazitekelezeki.

  Mbunge wa Moshi Mjini (Chadema), Philemon Ndesamburo alisema kuwa si kwamba Rais Kikwete hajafanya kitu, bali ameshindwa kutekeleza ahadi zake nyingi.

  Alisema suala alilokuwa akilizungumzia la maisha bora kwa kila Mtanzania ndoto na kwamba kauli mbiu ya “ari mpya, nguvu mpya na kasi mpya” ilikuwa ni siasa ambayo itamtesa.

  “Serikali huwa inataka kushinda uchaguzi, ahadi nyingi hazitekelezeki; ameshindwa mengi na amejitahidi machache,” alisema Ndesamburo.

  Naye Dk Azavael Lwaitama wa UDSM alisema suala si la Rais Kikwete bali kujiuliza CCM imefanya nini mpaka sasa kwa kuwa ndicho chama kilicho madarakani.

  “Wananchi wanaishi kwa matumaini kwa sababu kuongeza shule nyingi si maendeleo kwa kuwa wanafunzi wengi wanafeli; kukosekana kwa waalimu ni tatizo,” alisema Dk Lwaitama.

  Alisema kuwa ni kitu cha ajabu kwa katibu mkuu wa CCM, Yusufu Makamba kusema kuwa Kikwete ndiyo anakibeba chama, wakati chama kipo tangu alipokuwepo Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere na amefariki na kukiacha.

  “Inashangaza Makamba kusema Rais Kikwete ndio anakibeba chama wakati Nyerere alikuwepo, amefariki na amekiacha chama, kilichopo ni kuangalia mustakhabali wa chama na si kumsifia mtu,” alisema Dk Lwaitama.

  Wakati wakisema hayo, Makamba alishawahi kukaririwa akisema Rais Kikwete atatimiza ahadi zake alizotoa katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2005, kama atapatiwa muda.

  Hivi karibuni balozi wa Umoja wa Ulaya (EU), Tim Clarke aliambia Mwananchi Jumapili kuwa anashangaa kuona serikali inasema inakwenda kwa mwendo wa kasi, lakini mambo mengi yapo kama yalivyo.

  Clarke alisema wabia wa maendeleo ya Tanzania wamefanya mapitio ya mwaka na hali inaonekana si nzuri kama ilivyotarajiwa kwa kuwa alama za utekelezaji ziko wastani, huku maeneo kama vile mageuzi katika sekta ya umma yakionyesha alama zinazotia wasiwasi wa kutopata mafanikio.

  Alisema kuwa pamoja na kuwa wabia wamekuwa wakitoa misaada kwa Tanzania, baadhi wanafikiria kupunguza ahadi na utoaji wa misaada kwa kuwa hawaoni mpango ulio wazi wa kushughulikia matatizo katika njia inayoeleweka.

  Naye askofu mkuu wa Kanisa Katoliki, Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo alikaririwa wiki hii akisema kuna kila dalili za kukwama kwa mkakati wa kilimo kwanza, kutokana na kushindwa kuelekeza nguvu za kutoa elimu kwa wakulima ili waendeleze sekta hiyo.

  Akionyesha mtazamo huo tofauti, Pengo alisema:"Kaulimbiu inayotumiwa na viongozi wa nchi (Kilimo Kwanza), haiwezi kubadili au kuleta maendeleo katika kilimo. Cha msingi hapa ni kumwezeshe mkulima kwanza ili apate elimu ya kuendeleza kilimo.”
  Kwa mujibu wa Pengo, ni vigumu kufikia azma ya Kilimo Kwanza bila kuwawezesha wakulima kwa kuwa mabadiliko katika nyanja ya kilimo yanapatikana kwa mkulima mwenye elimu.
  Tuma maoni kwa Mhariri
  [​IMG]Facebook Contact Us DISCLAMEREmail:webmaster@mwananchi.co.tz© Mwananchi Communications Ltd 2006- 2009
   
 2. MchunguZI

  MchunguZI JF-Expert Member

  #2
  Dec 19, 2009
  Joined: Jun 14, 2008
  Messages: 3,623
  Likes Received: 590
  Trophy Points: 280
  Haki Elimu walikwisha fanya mapitio ya ahadi za Rais na wanasiasa wote wa ngazi za juu. Aliye na makusanyo ya ahadi hizo ni bora akazirusha hapa.

  Kwa ujumla kwao ni msalaba usiobebeka. Labda zikikumbushwa tena, watafahamu kwamba siasa siyo uongo majukwaani.
   
 3. Geza Ulole

  Geza Ulole JF-Expert Member

  #3
  Dec 19, 2009
  Joined: Oct 31, 2009
  Messages: 11,065
  Likes Received: 3,992
  Trophy Points: 280
  We inafikiri kuchukua rundo la mawaziri wasio na uzoefu wa kazi kungetufikisha wapi (mtu hajaongoza hata kaya ataweza wizara)? Jiulize wakina Aisha Kigoda, Sophia Simba, Mwangunga na Matilda Buriani wanafanya nini? kama kuwakomboa wanawake isiwe kuwap awale wasio na uwezo! wapo wanaoweza hizo kazi! wanawake wengi tu wanaendesha mashirika! hapa walipewa watu madaraka kufuata mtandao hebu angalia Lawrence masha anafanya nini? zaidi ya miaka mitano vitambulisho vimekwama! Na Shukuru Kawambwa, kwanini mradi wa mabasi ya kasi haujaanza hadi leo? na uwanja wa ndege wa Mbeya je? over 10 years i guess! Je na daraja la Kigamboni? Huyo Prof. Maghembe watoto wetu kila siku wanafeli! Migogoro kila kona na hakuna uvumbuzi!
   
 4. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #4
  Dec 19, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,384
  Trophy Points: 280
  Ningependa kusikia watu wa TPN wana majibu gani dhidi ya hoja za Bana..
   
 5. Cynic

  Cynic JF-Expert Member

  #5
  Dec 19, 2009
  Joined: Jan 5, 2009
  Messages: 5,154
  Likes Received: 628
  Trophy Points: 280
  Huyu Bana anaonekana kioja hata kuliko waliomtangulia (Mkandala/Ndumbaro/Kilian). Sioni tofauti kauli zake na za Makamba
   
Loading...