Balozi za nje zafilisi Nchi !

Balozi za nje zafilisi Nchi !

The Fixer

JF-Expert Member
Joined
Mar 3, 2008
Posts
1,365
Reaction score
599
• Italia yaongoza..
•Ujerumani na Japan zafuata kwa kufuja....

Wana JF,

Balozi za Tanzania zilizopo nchi za nje zimekuwa na matumizi makubwa kupita kiwango kiasi cha baadhi yake kusababisha madeni makubwa kwa Taifa.

Balozi hizo zaidi ya 18 zimekuwa zikitumia fedha zaidi ya bajeti yake iliyopangwa katika kujiendesha, ununuzi wa majengo usiokuwa na hati miliki pamoja na kazi nyingine za ndani.

Hayo yameonekana katika ripoti ya mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za Serikali ( CAG ) ya mwaka 2011/ 12 iliyoishia Juni 2012. Ripoti hiyo inaonyesha kwamba matumizi zaidi ya bajeti zinazopangwa kwa ajili ya ofisi za kibalozi za Tanzania yamesababisha malimbikizo mengi ya madeni yanayolazimu kulipwa katika bajeti ya mwaka ujao wa fedha

Balozi zinazoongoza kwa utaratibu huo mbaya kimatumizi, Ripoti inabainisha ni pamoja na Ubalozi wa Italia ( Bil 5) , Ujerumani ( Bil 2 ), Japan ( Mil 950), Sweden ( Mil 910 ) , Ubelgiji ( Mil 681) na China ( Mil 587 )

Ripoti hiyo inaeleza kwamba baadhi ya balozi hizo zimekuwa zikitumia fedha kutoka kwenye miradi ya balozi hizo , zikiwemo fedha zinazotokana na makusanyo ya ada za Viza. Uamuzi wa kutumia kwa namna hiyo unafanywa bila ya kuwa umeidhinishwa na Serikali



Source: Fahamu

The Fixer,

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Back
Top Bottom