MALCOM LUMUMBA
JF-Expert Member
- Jul 26, 2012
- 21,035
- 64,851
Wasalaam,
Kuna huyu mzee anaitwa Vitaly Churkin kama mtu anapenda kufuatilia sana UNSC (United Nations Security Council) Sessions unaweza kuwa unamfahamu vizuri.
Amefariki leo dunia ambapo alianguka ghafla kwenye ofisi yake ya Umoja wa Mataifa iliyoko Marekani na kupelekwa hospitali lakini chanzo cha kifo chake bado hakijafahamika.
Amefanya kazi kubwa sana na yenye weredi hasahasa pale ambapo alisaidia kuzuia nchi ya Syria isivamiwe kijeshi kwa kutumia kura ya VETO. Alishawahi kusema kwamba siku dunia ikitoa Kura ya VETO basi Umoja wa Mataifa utageuzwa kuwa Uwanja wa Fisi kwa Marekani. Pia mwaka juzi alipinga maoni yaliyotaka mataifa kama Ujerumani na Brazil kupewa kura ya VETO. Mara nyingi kutokana na hoja zake alijikuta kwenye mtanganange mzito na Balozi wa Marekani Umoja wa Mataifa, mama Samantha Smith.
Kinachonishangaza kuhusu bwana Vitaly Churkin ni kimoja tu.
1)Amezaliwa Tarehe 21 February 1952.
2)Amekufa Tarehe 20 February 2017.
Hivyo kesho ndiyo ilikuwa anasheherekea siku yake ya kuzaliwa.
Juzi tu hapa alikuwa anaongea vizuri kweli na nilikuwa natamani kuona atafanya nini na Balozi mpya wa Trump.
Apumzike kwa Amani aisee.
Chanzo: www.rt.com/news/377988-russian-ambassador-churkin-un-dies/
CC: Richard , mngony , Dotworld , Apollo , Bukyanagandi , maalimu shewedy , MSEZA MKULU , herikipaji ,