Balozi wa Marekani na Uingereza mmetukosea sana Watanzania

Frey Cosseny

JF-Expert Member
Feb 4, 2015
1,984
1,405
Nimeona Tangazo la Balozi la America na Balozi la Uingereza, kwanza nimeshamgazwa na matamko yao wakiongelea haki za Raia.

Hivi Waingereza na Wamerikani ni watu wa kutufundisha sisi Watanzania kuhusu haki ya Raia?

Wamerikani hawa kwa kushirikiana na Waingereza ambao walisomba watu kutoka Mataifa mbalimbali na kwenda kuwafunga kwenye gereza la Guantanamo Bay bila hata kuwapeleka mahakamani tena raia wa Nchi za kigeni.

Hawa Wamerikani ambao majuzi mhendesha mashtaka mkuu wa mahakama ya kimataifa ya Uhalifu wa Kivita alitaka wachunguzwe kuhusu Uhalifu wa Kivita waliyofanya Taliban na Pakistani na wakaamua kumfungia visa ya kuingia kwao mwendesha mashtaka huyo.

Hawa Wamerikani ambao Rais wao hivi majuzi alitamka maneno ya Kibaguzi mpk ikasababisha mauaji huko nchini kwao Leo Ndiyo wanakuja kutuambia namna ya kufuata sheria dhidi ya raia wetu.

Hawa Wamerikani na Waingereza waliyoshiriki kudhamini vurugu za Mtwara kwa kisingizio cha Gesi magari ya serikali yalichomwa moto Majengo za serikali zilichomwa moto watu kuharibiwa nyumba na Mali zao.

Hawa Wamerikani ambao wamedhamini mauaji ya Kibiti, Mkuranga na Rufiji ambapo watumishi wa Umma na Viongozi wa Chama Cha Mapinduzi waliuliwa.

Hawa Wamerikani ambao hata hawajui kumchagua Rais wao mpk Warusi wawasaidie Leo wanakuja kutuambia kuhusu Demokrasia?

Tunataka kuwajulisha wamerikani na Waingereza na vibaraka wao kuwa kabla hamjatoa ilo tamko tayari tulijua majadiliano yenu pia tulijua kinachoendelea.

Tunajua mbinu zenu za kupitisha silaha kupitia mpaka wa Namanga na silaha zingine kukamatwa Ngorongoro kutaka vyama siasa mnavyoviita vya harakati kujulikana na kudhibitiwa.

Tunajua mbinu zenu la kuibia Rasimali za nchi yetu kudhibitiwa.

Vyama vya Kiraia (NGOs) mlizokuwa mnawatumia kupitisha pesa Haramu kudhibitiwa.

Sasa mnatafuta chokochoko sisi Watanzania tunawaambia hamtaweza chochote.

Hii nchi haijawahi kushindwa vita mahala popote Duniani iwe ya silaha au vita ya kisiasa.

Mfahamu tu kuwa kabla hamjafanya kitu chochote tayari Watanzania tunayo taarifa.

Sisi kama Watanzania Wazalendo tuliyo na uchungu na Taifa letu tuko tayari kwa Mapambano iwe ya kisiasa hata ikibidi ya silaha kumlinda Rais wa JMT na Amir Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na usalama.

Hatutawaogopa kiumbe yeyote awe Bwenyenye Kabaila Mabeberu au mawakala wao wawe na Pua ndefu au Meno yaliyooza tutapambana usiku na mchana kulinda Taifa letu hadi tone la mwisho la damu yetu.

Tanzania ni nchi huru hatubabaishwi na mtu yeyote vijana, Wanawake na Wazee wapo tayari kupigania Taifa hili na kumlinda Rais wetu na kila aina ya hila ya Mabeberu wa Magharibi na mawakala wao.

Tunawataka mabalozi hao kufuta Mara moja tamko lao la sivyo sisi Watanzania tutaelekeza Serikali yetu tukufu kufunga mahusiano ya Kibalozi na nchi ya America na Uingereza na pia kuacha kusimamia maslahi ya wamerikani na Waingereza yaliyoko kwenye Ukanda wetu.

Ni vyema mabalozi wa Nchi hizo mbili kujikita katika kushughulikia masuala ya diplomasia kama ilivyoanishwa katika Mkataba wa Vienna inavyotamka na kuacha kuingilia masuala ya ndani ya Nchi yetu.

Kuhusu suala la Erick Kabendera sitaweza kuongelea kwasababu suala Ilo katika Vyombo vya sheria (Mahakama) na siyo vyema Mataifa ya Kigeni kuingilia uhuru wa mahakama .

Hii ni Mara ya pili mabalozi wa Nchi za Magharibi kuingilia Uhuru wa Mahakama yetu katika kipindi cha mwaka moja.

Ikumbukwe wakati Mwenyekiti wa Chadema Taifa Freeman Mbowe na Mbunge wa Tarime Mjini Esther Matiko wakiwa mahabusu kwa kukiuka masharti ya dhamana nchi hizo zilitaka Waziri wa katiba na sheria aimuru mahakama kuwaachia huru Viongozi kitendo ambacho ni kinyume cha sheria ya nchi yetu.

Tunawaambia Mabeberu wa Magharibi na mawakala wao kuwa tuko imara hatuyumbishwi na takataka yeyote hata aje na Pua ndefu kama mkonga wa tembo tutashughulika nao mpk dakika ya Mwisho.

Ole wenu Watanzania wazandiki mnaotumika na Mabeberu kutaka kuleta chokochoko tutaanza na nyie kama mnaona mmechoka maisha hapa Tanzania bora mtafute nchi yetu nyingine mkaishi kwa taarifa yenu akina Kambona walijaribu walishindwa hizi ni salaam zenu taarifa zenu zote ziko wazi ni suala la muda tu.

Tata Magufuli Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi na Rais wa JMT chapa kazi na kiumbe yeyote atakayeleta pua lake fekelea mbali.
 
Na sisi hatujakatazwa kuwasema wanapokosea.

Ukiambiwa kitu umefanya vibaya, halafu ukaanza kuondoka katika hiyo hoja kwamba umefanya vibaya ama la, ukaenda kwenye hoja nyingine ya kama aliyekusema naye kafanya vibaya, utaonekana kama unakwepa hoja ya kama umefanya vibaya au la.

Kuna wengi tunaisema serikali, si mabalozi hao tu.

Sasa na sisi Watanzania utatuambiaje?

Tuangalie ukweli, hata saa mbovu inaweza kuwa sawa mara mbili kwa siku.

Hata kichaa anaweza kusema maneno yenye hekima.

Usikatae neno kwa sababu kasema kichaa tu.

Lipime, kama unalikataa, likatae kwa mantiki, si kwa sababu limesemwa na fulani.
 
Na sisi hatujakatazwa kuwasema wanapokosea.

Ukiambiwa kitu umefanya vibaya, halafu ukaanza kuondoka katika hiyo hoja kwamba umefanya vibaya ama la, ukaenda kwenye hoja nyingine ya kama aliyekusema naye kafanya vibaya, utaonekana kama unakwepa hoja ya kama umefanya vibaya au la.

Kuna wengi tunaisema serikali, si mabalozi hao tu.

Sasa na sisi Watanzania utatuambiaje?

Tuangalie ukweli, hata saa mbovu inaweza kuwa sawa mara mbili kwa siku.

Hata kichaa anaweza kusema maneno yenye hekima.

Usikatae neno kwa sababu kasema kichaa tu.

Lipime, kama unalikataa, likatae kwa mantiki, si kwa sababu limesemwa na fulani.
Umepoteza muda kumjibu kwa utulivu mtu huyo,ungempuuza tu maana akili yake ishajiset hivyo alivyoandika!
 
Aisee kweli wametukosea sana . sisi tunateka , UA na kubambikia kesi watu wetu wao inawahusu nini. Kwani Azori ni mmarekani au mwingereza mpaka iwaume ? Wasituingilie hata tukichinja mtu hadharani
 
Umepoteza muda kumjibu kwa utulivu mtu huyo,ungempuuza tu maana akili yake ishajiset hivyo alivyoandika!
Kuna wengi sana wanaosoma mtiririko wa majibizano, zaidi yake, ambao wanaweza kufaidika na hoja za kumpinga.

Kwa hivyo, nikimjibu, si kwa sababu ya kujibizana naye tu, bali pia ni kwa faida ya wengine wengi wanaofuatilia mjadala huu.
 
Wanatakiwa kutambua kwamba Tz ni taifa lenye uhuru kamili wa kujiamulia mambo yake tena ukizingatia kwa sasa Tz ni dona kantre.

Ccm oyeeee
 
Marekani kwa sasa kuna baadhi ya maeneo ni kama Somalia, kusikia milio ya risasi ni kama kumsikia kuku akiwika asubuhi.

Hao wakubwa wanayo matatizo yao mengi tu ya kijamii, yanayowaumiza vichwa viongozi wao.

Hiyo taarifa ya ubalozi inaweza ikawa imetoka kwa wanaharakati wa humu humu ndani.

Yule mzee mwenye kuvaa mawani anayekuwa na JPM katika safari zake, kwa sasa yupo kazini haswa, waliozoea kuifitini nchi yetu katika awamu zilizopita, wamedhibitiwa vizuri.
 
Hata kama UK na US wanakiuka haki za binadamu kwenye nchi zao,hakuondoi ukweli wa tamko lao kwamba hapa Bongo,haki za binadamu zinakiukwa.

Tundu lisu,Dr Ulimboka,Ben SAA nane,Azory,Mdude Chadema.

"Mwizi anaweza kutoa taarifa za wizi unaoendelea kufanywa na mwizi mwingine"

Misaada,tunaomba Ulaya,US,sasa hata mkikosolewa mkubali,

Usilinganishe Tanzania,na UK,na US,sisi ni wadogo sana.

Umeishawahi kusikia,UK,US,Newzealand,Austaria,Canada,wanashutumiana kwa kukiuka haki za binadamu?

Watazilaumu nchi kama China,Russia,Ratino America,

Wakati mwingine ukisikia matamko yao,huwa yanaajenda iliyojificha,"deception"wewe unafikiri wanaongelea haki za binadamu,kumbe kuna ishu kubwa,wameilenga.

Tanzania ya Baba wa Taifa,iliweza kuwavimbia Wazungu,hii ya sasa HV haiwezi,inachoweza ni kuwapiga Chadema,kuzuia mikutano,kudukua,na kupoteza watu
 
Hawa wanawashwa na mradi wa umeme mpya, maana ndyo walikua wanapinga sana usifanyike ila Chuma chetu kimesonga mbele so ni kama wanavisa na sie hv
 
Mkuu pamoja na kujitanabaisha kama kinara wa demikrasia duniani, Marekani bado sio mwanachama wa ICC.

Kwanini sio mwanachama wa ICC mpaka sasa??

Demokrasia ni Vazi la kikondoo tu na ndio fimbo yao ya kuwapiga wote wanaokataa matakwa yao.
 
Bado kuna watu wananunua hizi propaganda mfu? Watu wameshamka, acheni kutenda uovu fullstop.
 
Kuna wengi sana wanaosoma mtiririko wa majibizano, zaidi yake, ambao wanaweza kufaidika na hoja za kumpinga.

Kwa hivyo, nikimjibu, si kwa sababu ya kujibizana naye tu, bali pia ni kwa faida ya wengine wengi wanaofuatilia mjadala huu.
Mkuu mimi nimeshitushwa na madai yake mengine ni makubwa na hayana ushahidi hata wa kimazingira.

Mfano vurugu za gesi isitoke Mtwara na mauwaji ya Kibiti anasema yalikuwa yanafadhiliwa na Marekani na Uingereza.

Hii tuhuma kubwa sana. Serikali kwanini haikutoa tamko baraza la usalama la UN au kwenye vyombo vya habari vya kimataifa kulaani jambo hilo?
 
Back
Top Bottom