Balozi wa Italia nchini Congo DRC auawa katika shambulizi

Screenshot_20210223-122437.png

Huyu hapa masikini..
 
Acha na wao wapate machungu ya vita vya Congo.
Wasifuraie kuvuna mali tu.
Akili zetu waafrika ni tabu, kila tatizo linalotukabili tuna kimbilia kumpa lawama mzungu?!!sio kila tatizo letu chanzo ni nje, sisi wenyewe ndio hasa wenye shida!!toka wametuachia uhuru ni zaidi ya miaka 60!!maji safi tu na salama bado ni tabu?afya bado ni tabu, uchaguzi mnafanya mtu anakatalia madarakani, hapo ni mzungu?kila leo katiba zinabadirishwa ili mtu asitoke madarakani , hapo ni mzungu?!!wanaoleta tabu congo ni kagame na mseveni hao ni MABEBERU?umoja wa afrika uko wapi kuwakemea?unafikikiria chanzo cha jk kutofautiana na kagame ilikuwa ni nini?si baada ya jk kupelekea wanajeshi kupambana na M23?!!
 
Itakua ajabu sana sehemu ya nchi ipewe nchi nyingine,itakua ni maajabu ya dunia
Ni kweli mkuu!!umkaribishe mgeni kwako, baada ya muda na yeye anasema ni kwake hapo!!kama vipi mgawane eneo!!mfano kule sud kivu, kuna sehemu inaitwa FIZI, na sehemu nyingi za UVIRA, kuna wanyamulenge wengi tu toka RWANDA, walienda kule miaka mingi, kwa ajiri ya malisho ya mifugo, leo hii na wao wanataka eneo kuwa ni la kwao?!!ndio mizozo hiyo ya kila leo.ile operation aliyoiendesha jk miaka ile alishaliona hili!!
 
Kagame unaweza kukuta yeye ndio yuko behind ya hiki kifo ila kwa kushirikiana na wajanja wenzake wamewapa fdrl msala ili ipotezwe kabisa duniani
Kwani mkuu hawa FDRL hawana mahusiano mazuri na PK?
Wahutu toka lini wakawa na mahusiano mazuri na kagame
Sikuwa nafahamu kama ni wahutu, it make sense.. inawezekana
Democratic forces of liberation of rwanda,nadhani kirefu cha fdrl ni hivi kama niko wrong wakuu wenye kujua zaidi watanisahihisha
Taarifa ni nyingi ila kuna hali mbaya ya ki usalama huko Congo RD
 
Ni jambo jema kwa upande wangu.
Hao ndio wanachochea vurugu DRC isitulie ili wakwapue maliasili....sasa acha nao waonje chungu ya kupigwa risasi za mbavu ili ndugu zao huko Ulaya na Marekani akili ziwakae sawa.
Yaani kinachoshangaza ni kwamba majeshi ya UN yapo, raia wanauawa kwa kukatwa mapanga na vikundi vya waasi ,na matukio hayazuiliwi labda kwa kuwa ni balozi wa Italy UN watachukua hatua.
 
Shida ya Congo mali imegeuka laana.
Mkuu sidhani kama mali ndio tatizo kwenye jimbo la KIVU - kinacho endelea pale kuna nchi zina fund waasi na kuwapa silaha, ajenda ya siri ni kutaka Jimbo la KIVU lijitenge baadae lijiunge na Taifa watakalo taka - ni plan za muda mrefu hizi.

Ukiangalia kijuu juu unaweza kufikiri wanagombania mali - hii si kweli hata kidogo, mbona hatusikii maugomvi gomvi Shaba Provinces ie Kolwezi na Lubumbashi?
 
Back
Top Bottom