Balozi Seif Iddi na Waziri Nahodha jibuni hoja hizi za Uamsho | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Balozi Seif Iddi na Waziri Nahodha jibuni hoja hizi za Uamsho

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Makaimati, May 18, 2011.

 1. Makaimati

  Makaimati JF-Expert Member

  #1
  May 18, 2011
  Joined: Apr 4, 2011
  Messages: 462
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Balozi Seif Iddi na Waziri Nahodha jibuni hoja hizi za Uamsho

  May 18, 2011 by zanzibardaima

  Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara ya Kiislamu Zanzibar

  Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara ya Kiislamu ya Zanzibar imetoa taarifa rasmi leo hii kuhusiana na masuala matatu makubwa yanayohusu hatima ya Zanzibar kwa sasa: kuchomwa kwa moto mabanda ya wafanyabiashara huko Pwani-Mchangani, mwenendo wa serikali ya Umoja ya Kitaifa na maoni ya Wazanzibari kuelekea Muungano. Hoja inayoibuliwa na Uamsho ni kuwa, pana upotoshaji mkubwa wa makusudi unafanywa na watu kuhusiana na hayo yote matatu, ambao ni mbaya kwa mustakabali wa Zanzibar. Zanzibar Daima inaichapisha taarifa hiyo kwa imani kwamba watu wanapaswa kuambiwa ukweli kuhusiana na masuala haya na kwamba hapa kuna wahusika wanaopasa kuwajibika.
  JUMUIYA YA UAMSHO NA MIHADHARA YA KIISLAMU
  للجنة الدعوة الإسلامية
  THE ASSOCIATION FOR ISLAMIC MOBILISATION AND PROPAGATION


  P. O. Box 1266
  Tel: +255 777 419473/434145
  E-Mail: jumiki@hotmail.com

  MKUNAZINI – ZANZIBAR


  TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI 18/05/2011

  Shukrani zote anastahiki Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehma. Rehma na amani zimshukie kipenzi chetu, Mtume Muhammad (S.A.W.) na ahli zake na jamaa zake na walio wema katika Uislamu.


  Kutokana na matukio yaliyojitokeza katika nchi na ambayo yanaweza kuleta mgawanyiko na chuki na kuiingiza katika mgogoro usio wa lazima, Jumuiya ya UAMSHO imeona nayo ichukuwe nafasi kuelezea uoni wake juu ya hayo yaliyojiri.

  Kimsingi, kuna matukio matatu yaliyotokea Zanzibar ambayo sasa yanaonekana kuwa gumzo Zanzibar na Bara: kwanza, suala la kuchomwa moto kwa mabanda ya biashara huko Pwani Mchangani; pili, suala la Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar chini ya mfumo wa Umoja wa Kitaifa na, tatu, maoni ya Zanzibar kuhusu Mswada wa Mapendekezo ya Marekebisho ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.  1. TUKIO LA PWANI MCHANGANI

  Suala la tukio la Pwani Mchangani la kuchomwa moto mabanda ya wafanyabiashara linapotoshwa kwa makusudi na watu wasioitakia kheri Zanzibar.


  Kwanza, si kweli kama mabanda hayo yaliyochomwa ni 70 kama livyoripotiwa na baadhi ya vyombo vya habari, idadi halisi ni 29.


  Pili, wamiliki wa mabanda hayo si Wabara kama inavyoelezwa. Ukweli ni kuwa 27 kati yao ni ya Wazanzibari na mawili tu ndio ya Wabara.


  Tatu, si kweli kuwa tukio hilo ni la kisiasa, bali ni la kijamii, baada ya malalamiko ya wananchi kulalamika kutokana na vitendo vya ubakaji, umalaya, ulevi, mauaji na biashara ya unga katika eneo hilo.


  Nne, si kweli kwamba tukio hili linahusiana na suala la kuvunja Muungano, kwani baada ya malalamiko hayo na kuthibitishwa na vyombo husika, serikali za mitaa ziliwataka wafanya biashara hao kuondoka katika eneo hilo ifikapo tarehe 01/05/2011. Sasa je, serekali za mitaa zilitaka kuuvunja Muungano?


  Tano, si kweli kuwa Wabara wanafukuzwa au kunyanyaswa Zanzibar. Ukweli ni kuwa wapo wafanyabiashara wengi katika maeneo mengi ya Zanzibar, ukiwemo Mji Mkongwe, Marikiti Kuu Darajani wakifanya shughuli mbalimbali, zikiwemo kuuza njugu, matunda na bidhaa nyengine za mikononi mitaani mwetu, na kuna wanaofanya kazi za kulima mashambani. Mbona hawa hawajabughudhiwa? Jibu ni kuwa hawajafanya vitendo au biashara za uhuni, unga, ulevi, n.k.

  Hata ile hoja kuwa eti Wazanzibari wapo kila sehemu Bara, lakini hawabughudhiwi, haina mashiko. Maana suali ni Wazanzibari gani wanaofanya biashara ya ulevi, unga, ubakaji, ukahaba, halafu serikali ikawaachia kwa kisingizio cha Muungano?


  Sita na mwisho kuhusiana na hili, maswali ya nani amechoma na kwa nini amefanya hivyo yako mahakamini. Ni busara kuiwachia mahakama iamuwe kwa mujibu wa sheria.


  Masikitiko yetu makubwa na yenye masuala mengi bila jawabu, ni kauli ya Waziri wa Mambo ya Ndani, Mhe. Shamsi Vuai Nahodha, kukurupaka na kusema kuwa hawa waliochoma ni wahalifu, wanataka kuvunja Muungano na yeye, kama waziri, atahakikisha waliohusika wanachukuliwa hatua. Sasa suala kuhusu hawa wafanyabiashara kharamu, ambao wanachi na vyombo vya serikali vimeamua wahame, mbona hawahakutaja sababu zilizopelekea kupewa amri ya kuhama?


  Kauli za Mhe. Nahodha zimewachukiza Waislamu na Wazanzibari na wameanza kumtafsiri kuwa naye ni miongoni mwa wasioitakia mema Zanzibar.

  Tunawasihi Waislamu na wananchi kwa jumla kutokubali, katika kipindi hichi, kupokea fitna za kutaka kuwagawa na kupandikiza chuki baina yetu.

  Pia tunaiomba serikali kuchukuwa khatua zinazofaa kwa gazeti la NIPE HABARI kutokana na taarifa zake za kuhatarisha amani ya nchi za tarehe 13-19 Mei 2011, kama habari iliyopewa nafasi ya mbele UZANZIBARI, UZANZIBARA SASA WANUKIA ZANZIBAR. Ni taarifa zinazo weza kulitia taifa katika khatari ya vita vya kikabila na kidini.


  2. SERIKALI YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR CHINI MFUMO WA UMOJA WA KITAIFA

  Kumeanza kujitokeza watu kutaka kujenga fitna ili Wazanzibari waanze chuki na viongozi wao na kuidhoofisha serikali na kuirejesha nchi ya Zanzibar katika matatizo yale ya nyuma.


  Kidogo tukumbushe angalau watu wajielewe tunapotoka na tulipo sasa: Kwa miaka 46, kuanzia 1961 hadi 2005, Zanzibar imeshaingia katika chaguzi sita zinazohusisha vyama vingi vya siasa, lakini matokeo ya chaguzi zote hizo ni kudhalilika kwa Waislamu, dini yao na utamaduni wao. Hakuna uchaguzi wowote wa vyama vingi ambao umepita Zanzibar bila ya kuwacha athari mbaya kwa Wazanzibari. Matokeo yake ni kuwa kila uchaguzi mmoja unapofanyika, huwa msingi umechimbwa kwa jengo la mateso na mfarakano kwa uchaguzi ujao.


  Kwa mfano, chuki ya utumwa na ubwana, na Uarabu na Uafrika iliyopandikizwa kwa makusudi katika uchaguzi wa pili wa Juni 1961, ilipelekea Waislamu zaidi ya 70 kuuliwa huku watoto wa Kiislamu katika kijiji cha Bambi, wakiteketezwa kwa moto.

  Uchaguzi wa 1995 uliofanyika baada ya miaka zaidi ya 30 tangu Mapinduzi ya 1964 na kufutwa kwa vyama vingi, haukupunguza chochote katika madhila ya Waislamu wa Zanzibar, isipokuwa kuongeza.fitna ya Upemba na Uunguja iliyopaliliwa na taasisi za dola na matokeo yake yakawa ni kuwafanya Waislamu wa nchi hii waangaliane kwa misingi ya maeneo wanayotoka, na sio kwa Mungu Mmoja wa Haki wanayemuuamini na kumuuabudu. Badala ya kusimama na kalima tukufu ya "Laa Ilaah Illallah, Muhamadarasuulullah", Waislamu wa Zanzibar wakawa wanasimama na kauli za Upemba na Uunguja, Uarabu na Uafrika na ubwana na utumwa!

  Chaguzi za mwaka 2000 na 2005 mambo yakawa ni yale yale. Tena majeshi yakamwagwa mitaani yakiwa na silaha za kivita. Rais wa wakati huo wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ambaye pia ni Amiri Jeshi Mkuu, Benjamin Mkapa, alipoulizwa na waandishi wa habari sababu za kupeleka majeshi na vifaru Zanzibar, naye aliwauliza kulikuwa na sababu gani kwa Wamarekani kupeleka wanajeshi Iraq!


  Kwa hivyo, nchi ya Waislamu ya Zanzibar ikawa imevamiwa na majeshi ya kigeni kama vile Iraq ilivyokuwa imevamiwa na Marekani. Matokeo yake ikawa ni muendelezo wa kile Rais Jakaya Kikwete alichokuja kukiita "mpasuko" wa Zanzibar.

  Hata baada ya matokeo ya chaguzi hizo na matokeo kutangazwa, Waislamu wakawa wakifuatwa majumbani na misikitini kupigwa na kudhalilishwa kupita kiasi. Matokeo yake, makundi ya vijana wa Kiislamu

  wakaanza kuhama visiwa hivi na kukimbilia ughaibuni, ambako wameselelea hadi leo. Miongoni mwa athari za vijana hao wa Kiislamu wa Kizanzibari kuselelea ugenini, ni kupoteza maadili ya dini yao na hivyo kuudhoofisha Uislamu.


  Kwetu sisi, huu ni mpasuko baina ya Waislamu ambao mashiko yake hayako katika Uislamu lakini ambao athari zake zinawapata Waislamu wa Zanzibar. Tunaamini kwamba Zanzibar inapigwa vita kwa sababu ya Uislamu wake.

  Tukumbuke kulijitokeza taasisi za kigeni Jumuiya ya Madola na pia kamati ya vyama vya siasa vyote vilishindwa kuziba mpasuko huo. Hii imetokana na kuwa wengine hawakuwa na nia nzuri na Zanzibar.

  Baada ya madhara yote haya, ambayo yamegharimu maisha ya watu, mali kupotea na mateso ya kila aina, Wazanzibari wenyewe wenye uchungu na nchi yao, wakaona huku inakoelekea Zanzibar ni kubaya na wa kuionea huruma Zanzibar ni Wazanzibari wenyewe.

  Mhe. Amani Karume na Mhe. Maalim Seif wakaamua kuzika yale yote tuliyoyaeleza kwa ufupi. Yakaja Maridhiano, na nia ni kujenga Zanzibar mpya yenye amani utulivu umoja na maendeleo. Sote tukakubali kufuta tafauti zetu na kujenga umoja na tukaahidi kushirikiana na viongozi kujenga Zanzibar mpya yenye maendeleo. Na hilo litafanikiwa kwa kuwepo serikali ya umoja, wengi wa Wazanzibari wakawafiki hilo.

  Sasa matunda ya Maridhiano tumeanza kuyaona katika Uchaguzi Mkuu 2010, namna ya amani utulivu ulivyotawala. Hata baada ya matokeo, Wazanzibari wote walisherehekea kwa pamoja. Hakuna aliyepingwa, kubakwa, kuuliwa wala kuharibiwa mali. Haya ndio maamuzi ya Wazanzibari.


  Sasa kumeanza kujitokeza watu kutaka kuidhoofisha juhudi hii yote, kwa kisingizio cha kuwa serikali iliyopo haina la maana. Wameanza kuwakashifu viongozi wa juu kuwa waregevu. Hawa tunawahisabu ni maadui wa Zanzibar. Na upo wasisiwasi kuwa baadhi ya viongozi wa Bara hawakupendezewa na hali hii, na wengine wakataka kuwafurahisha kwa vitendo na kauli ili waonekane wao wema.au bora kuliko wengine.

  Na hii imetutia wasiwasi zaidi baada ya Afisa wa Ubalozi wa Marekani aliyeko Zanzibar, kuanza kupita kuhoji watu kuhusu uwoni juu ya serikali na tukio la Pwani Mchangani. Hatua ya afisa huyu inaweza kusababisha mgawanyiko. Tuko macho na hatua za ya afisa huyo na tukibaini kuna uchochezi au fitna hatutoweza kumvumlia.


  Tunatamka wazi, hatuko tayari kumnyamazia kiongozi au yoyote awe wa nje au ndani kutaka kuleta fitna na mgawanyiko miongini mwetu.


  Suala la ugumu wa maisha na kupanda kwa bei za bidhaa muhimu, serikali inalielewa na tunaamini Rais wa Zanzibar na Baraza lake wako makini kulitafutia ufumbuzi, huku tukiamini mabadiliko yatapatikana.

  Si kweli kwamba serikali haina la maana inalofanya. Wanaosema hivyo wanataka kujenga fitna kwa Wazanzibari waanze kuichukia serikali yao. Tunasema nafasi hiyo haipo tena Zanzibar. Wito wetu kwa Wazanzibari ni kuwa tuwe macho na maadui!


  3. MUUNGANO

  Kumekuwa na kauli nyingi tokea Kamati ya Bunge kuja Zanzibar kukusanya maoni kuhusu Rasimu ya Marekebisho ya Katiba na Wazanzibari wakaonesha msimamo wao kuhusu mustakbali wa nchi yao kwa kuukataa katakata mswada huo.

  Imekuwa ni kosa mpaka viongozi wa Dini wakaitwa wahuni. Mengi yamesemwa na hoja mbali mbali zinatolewa kulazimisha Wazanzibari kuukubali Muungano. Tunasema, miaka 47 ya kudumu kwa Muungano ni kwa heshima na ustahamilivu wa Wazanzibari. Na kwa muda wote wamezibwa watu midomo kuhoji au kukosowa kuhusu Muungano. Tunasema karne hizo zimekwisha.


  Muungano huu tokea kuundwa kwake umekuwa na kasoro nyingi na kuundiwa tume 21 na bado kasoro zipo pale pale.

  Nasaha zetu ni kuwa iko haja kujadiliwa upya Muungano na pande zote mbili; na kushauriwa Watanganyika na Wazanzibari kuhusu mfumo wa Muungano wanaoutaka. Kinyume na hivyo kunaweza kukazuka mgogoro mkubwa na unaoweza kuleta uvunjifu wa amani


  MWISHO

  Tunatowa wito kwa serikali ya Zanzibar kulitatuwa tatizo la wafanyabiashara wa Jua Kali ambao kwa muda wa miezi minne sasa maduka yao yamefungwa. Ingawa shauri lao lipo mahakamani, serikali ifikirie njia ya kuwaokowa wafanyabiashara hao ili kuondosha dhana potofu na maadui wakapata njia ya kuitia sumu jamii.


  WABILAH TAUFIQ
  AZZAN KHALID HAMDAN
  NAIBU AMIRI (JUMIKI)
   
 2. a

  abdulahsaf JF-Expert Member

  #2
  May 18, 2011
  Joined: Aug 31, 2010
  Messages: 859
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0


  Written by Stonetown (Kiongozi) // 18/05/2011 // Habari, Kitaifa // 6 Comments

  [​IMG]
  Shukrani zote anastahiki Mwenyezi Mungu mwingi wa rehma.Rehma na amani zimshukie kipenzi chetu Mtume (S.A.W.) na ahli zake na jamaa zake na waliowema katika Uslamu.
  Kutokana na matukio yaliojitokeza katika nchi na ambayo yanaweza kuleta mgawanyiko,chuki,na nchi kuingia katika mgogoro usio wa lazima,jumuiya ya UAMSHO imeona ichukuwe nayo nafasi kuelezea uoni wake juu ya hayo yaliojiri.
  Kimsingi kuna matukio matatu yaliotokea Zanzibar ambayo sasa yanaonekana kuwa gumzo Zanzibar na Bara.
  Kwanza. Suala la kuchomwa moto kwa mabanda ya biashara huko pwani mchangani
  Pili. Suala la serikali ya S.M.Z chini ya mfumo wa umoja wa kitaifa.
  Tatu. Maoni ya Zanzibar kuhusu mswada wa mapendekezo ya marekebisho ya katiba.
  1. Suala la tukio la pwani mchangani la kuchomwa moto mambanda ya wafanya biashara linapotoshwa kwa makusudi na watu wasioitakia Zanzibar kheri.
  2. Sikweli kama mabanda hayo yaliochomwa ni 70. kama livyoripotiwa na baadhi ya vyombo vya habari, idadi ni 29.
  3. wamiliki wa mabanda hayo si wabara kama inavyo elezwa 27 ni ya wazanzibar na mawili tu ndio ya wabara.
  4. sikweli kua tukio hilo ni la kisiasa bali ni la kijamii baada ya malalamiko ya wananchi kulalamika kutokana na vitendo vya ubakaji,umalaya,ulevi,mauaji, biashara ya unga,
  5. si suala la kuvunja muungano kwani baada ya malalamiko hayo na kuthibitishwa na vyombo husika serikali za mitaa iliwataka wafanya biashara hao kuondoka katika eneo hilo ifikapo tarehe 01/05/2011 wawe wameondoka katika eneo hilo sasa je serekali za mitaa zilitaka kufunja muungano?
  6. sikweli kuwa wabara wanafukuzwa au kunyanyaswa Zanzibar ,wapo wafanya biashara wengi mji mkongwe marikiti wauza njugu,wanaofanya kazi mashambani za kulima mbona hawa hawajabughudhiwa? Jibu hawajafanya vitendo au biashara za uhuni unga,ulevi, nk.
  Na hii hoja ya kuwa wazanzibari wapo bara mbona habughudhiwi suala ni wazanzibar gain wanaofanya biashara ya ulevi,unga ubakaji,ukahaba,halafu serikali ikawaachia kwa kisingizio cha muungano?
  7. suala nani kachoma na kwanini kachoma liko mahakamini tuiwachie mahakama iamumuwe kwa mujibu wa sheria.
  Masikitiko yetu makubwa na yenye masuala mengi bila jawabu ni kauli ya waziri wa mambo ya ndani mh:Shamsi Vuai Nahodha kukurupaka na kuwa hawa waliochoma ni wahalifu ,wanataka kufunja muungano na yeye kama waziri atahakikisha waliohusuka wanachukuliwa hatua.sasa suala kuhusu hawa wafanya biashara kharamu,ambao wanachi na vyombo vya serikali vimeamua wahame,je mbona hawa hakutaja sababu zilizopelekea kupewa amri ya kuhama?
  Kauli za Mh:Nahodha zimewachukiza waislamu na wazanzibar na wameanza
  Kumtafsiri kuwa ni miongoni mwa wasioitakia mema Zanzibar.
  Tunawasihi waislamu na wananchi kwa jumla kutokubali katika kipindi hichi kupokea fitna za kutaka kuwagawa na kupandikiza chuki baina yetu.
  Pili tunaiyomba serikali kuchukuwa khatua zinazo faa kwa gazeti la NIPE HABARI, kutokana na taarifa zake za kuhatarisha amani ya nchi za tarehe 13-19 mei 2011 kwa taarifa zake zilizopewa nafasi ya mbele UZANZIBARI,UZANZIBARA SASA WANUKIA ZANZIBAR. Ni taarifa zinazo weza kulitia taifa katika khatari ya vita vya kikabila na dini,
  Pili: suala la serikali ya S.M.Z. yenye kufuata mfumo wa umoja wa kitaifa.
  Kumeanza kujitokeza watu kutaka kujenga fitna ili wazanzibar wanze chuki na viongozi wao na kuidhofisha serikali na kuirejesha nchi ya Zanzibar katika matatizo yale ya nyuma
  Kidogo tukumbushe angalau watu wajielewe tunapo toka na tulipo sasa
  Kwa miaka 46.kuanzia mwaka 1961 hadi mwaka 2005, Zanzibar imeshaingia katika chaguzi sita zinazohusisha vyama vingi vya siasa, lakini matokeo ya chaguzi zote hizo ni kudhalilika kwa waislamu,dini yao na utamaduni wao.Hakuna uchaguzi wowote wa vyama vingi ambao umepita Zanzibar, bila ya kuwacha athari mbaya kwa wazanzibari.matokeo yake ni kuwa kila uchaguzi mmoja unapofanyika huwa msingi umechimbwa kwa jengo la mateso na mfarakano kwa uchaguzi ujao.
  Kwa mfano, uchaguzi wa pili wa juni 1961, chuki ya utumwa na ubwana,na Uarabu na Uafrika iliyopandikizwa kwa makusudi,ilipelekea waislamu zaid ya 70 kuuliwa huku watoto wa kiislamu katika kijiji cha bambi wakateketezwa kwa moto kwenye tanuri la mbata katika kijiji cha bambi.
  Uchaguzi wa 1995 uliofanyika baada ya miaka zaidi ya 30 tangu mapinduzi ya 1964 na kufutwa kwa vyama vingi,haukupunguza chochote katika madhila ya waislamu wa Zanzibar,isipokuwa kuongeza.fitna ya upemba na uunguja ilipaliliwa na taasisi za dola na matokeo yake yakawa ni kuwafanya waislamu wan chi hii waangaliane kwa misingi ya maeneo wanayotoka na sio kwa Mungu Mmoja wa Haki wanayemuuamini na kumuuabudu. Badala ya kusimama na kalima tukufu ya laa ilaah illallah,muhamadarasuulullah, waislamu wa Zanzibar wakawa wanasimama na kauli za upemba na uunguja,uarabu na uafrika na ubwana na utumwa!
  Uchaguzi wa mwaka 2000 na 2005 mambo yakawa ni yale yale. Tena majeshi yakamwagwa mitaani yakiwa na silaha za kivita. Rais wa wakati huo wa Tanzania, ambaye ni Amiri jeshi mkuu,Benjamin mkapa, alipoulizwa na waandishi wa habari sababu za kupeleka majeshi na vifaru Zanzibar,naye aliwauliza kulikuwa na sababu gain kwa wamarekani kupeleka wanajeshi iraq! Kwa hivyo nchi ya waislamu ya Zanzibar ikawa imevamiwa na majeshi ya kigeni kama vile iraq ilivyokuwa imevamiwa na marekani. Matokeo yake ikawa ni muendelezo wa kile Rais Jakaya kikwete alichokuja kukiita “mpasuko” wa Zanzibar.
  Hata baada ya matokeo ya chaguzi hizo na matokeo kutangazwa, waislamu wakawa wakifuatwa majumbani na misikitini kupingwa na kudhalilishwa kupita kiasi. Matokeo yake, makundi ya vijana wa kiislamu wakaanza kuhama visiwa hivi na kukimbilia ughaibuni,ambako wameselelea hadi leo, Miongoni mwa athari za vijana hao wa kiislamu wa kizanzibari kuselelea ugenini ni kupoteza kwa maadili ya dini yao na hivyo kuudhoofisha Uislamu.
  Kwetu sisi huu ni mpasuko baina ya Waislamu, ambao mashiko yake hayako katika uislamu lakini athari zake zinawapata waislamu wa Zanzibar.tunaamini kwamba Zanzibar inapigwa vita kwa sababu ya Uislamu wake.
  Tukumbuke kulijitokeza taasisi za kigeni jumuiya ya madola na pia kamati ya vyama vya siasa vyote vilishidwa kuziba mpasuko huo.hii imetokana na wengine hawakuwa na nia nzuri na Zanzibar
  Baada ya madhara yote haya ambayo yamegharimu maisha ya watu,mali kupotea na mateso ya kila aina, wanzanzibar wenyewe wenye uchungu na nchi yao wakaona huku inakoelekea Zanzibar ni kubaya na wakuionea huruma Zanzibar ni wenyewe.
  Mh: Amani Karume na Mh: Maalim Seif wakaamua kuzika yale yote tulioyaeleza kwa ufupi yakaja maridhiano, na nia ni kujenga Zanzibar mpya yenye amani utulivu umoja na maendeleo.sote tukakubali kufuta tafauti zetu na kujenga umoja na tukaahidi kushirikiana na viongozi kujenga Zanzibar mpya yenye maendeleo. Na hilo litafanikiwa kwa kuwepo serikali ya umoja,wengi wa wazanzibari wakawafiki hilo.
  Sasa matunda ya maridhiano tumeanza kuyaona katika uchaguzi mkuu 2010 namna ya amani utulivu ulivyo tawala na hata baada ya matokeo wote wazanzibari walisherehekea kwa pamoja. Hakuna aliyepingwa,kubakwa,kuuliwa,wala kuharibiwa mali.haya ndio maamuzi ya wazanzibar.
  Sasa kumeanza kujitokeza watu kutaka kuidhofisha juhudi hii yote kwa kisingizio cha kuwa serikali iliyopo haina la maana.na kuanza kuwakashfu viongozi wa juu kuwa waregevu. Hawa tunawahisabu ni maaduwi wa Zanzibar. na upo wasisiwasi kuwa baadhi ya viongozi wa bara hawakupendezewa na hali hii na wengine wakataka kuwafurahisha kwa vitendo na kauli ili waonekane wao wema.au bora kuliko wengine. Na hii imetutia wasiwasi zaidi baada ya afisa wa ubalozi wa marekani alioko Zanzibar kuanza kupita kuhoji watu kuhusu uwoni juu ya serikali na tukio la pwani mchangani.hatua ya afisa huyu,inaweza kusababisha mgawanyiko, tuko macho na hatua za ya afisa huyo, na tukibaini kuna uchochezi au fitna hatuto weza kumvumlia.
  Tunatamka wazi hatuko tayari kumnyamazia kiongozi au yoyote awe wa nje au ndani
  Kutaka kuleta fitna na mgawanyiko miongini mwetu
  Suala la ugumu wa maisha kupanda kwa bei bidhaa,serikali inalielewa na tunaamini Rais wa Zanzibar.na baraza lake wako makini kulitafutia ufumbuzi,huku tukiamini mabadiliko yatapatikana,
  Si kweli kwamba serikali haina la maana inalofanya wanaosema hivyo wanataka kujenga fitna kwa wazanzibar waanze kuchukia serikali yao.
  Tunasema nafasi hiyo haipo tena Zanzibar.
  Wito wazanzibar tuwe macho na maaduwi
  Suala la Tatu : Kuhusu Muungano
  Kumekuwa na kauli nyingi tokea kamati ya bunge kuja Zanzibar, kukusanya maoni kuhusuru rasimu ya marekebisho ya katiba. Na wazanzibar wakaonesha msimamo wao kuhusu mustakbal wa nchi yao, na kuukataa mswada huo,
  Iekuwa ni kosa mpaka viongozi wa Dini wakaitwa wahuni,
  Mengi yamesemwa na hoja mbali mbali zinatolewa kulazimisha wazanzibari kukubali Muungano.tunasema miaka 47 ya Muungano huu umedumu kwa heshima na ustahamilivu wa wazanzibar.na kwa muda wote wamezibwa watu mdomo kuhoji au kukosowa kuhusu Muungano, tunasema karne hizo zimekwisha.
  Muungano huu tokea kuundwa kwake umekuwa na kasoro nyingi na kuundiwa tume 21 na bado kasoro zipo pale pale.
  Nasaha zetu iko haja kujadiliwa upya muungano na pande zote mbili na kushauriwa watanganyika na wazanzibar kuhusu mfumo wa muungano wanaoutaka,kinyume na hivyo kunaweza kukazuka mgogoro mkubwa na unaoweza kuleta uvunjifu wa amani
  Mwisho
  Tunatowa wito kwa serikali ya Zanzibar kulitatuwa tatizo la wafanya biashara wa jua kali ambao kwa muda wa miezi mine maduka yao yamefungwa, ingawa shauri lao lipo mahakamani.serikali ifikirie njia ya kuwaokowa wafanya biashara hao ili kuondosha dhana potofu na maaduwi wakapata njia ya kuitia sumu jamii.
  WABILAH TAUFIQ
  …………………………..
  AZZAN KHALID HAMDAN
  NAIBU AMIRI(JUMIKI)
   
 3. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #3
  May 18, 2011
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Nadhani ni taarifa kwa waislam.
   
 4. Speaker

  Speaker JF-Expert Member

  #4
  May 18, 2011
  Joined: Aug 12, 2010
  Messages: 6,357
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  shiit,eti zimechomwa 29?
  so that is nothing to you?
   
 5. Speaker

  Speaker JF-Expert Member

  #5
  May 18, 2011
  Joined: Aug 12, 2010
  Messages: 6,357
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  sure,ipelekwe jukwaa la dini kule
   
 6. tanga kwetu

  tanga kwetu JF-Expert Member

  #6
  May 18, 2011
  Joined: May 12, 2010
  Messages: 2,163
  Likes Received: 1,122
  Trophy Points: 280
  bolded and colored phrases=Zanzibar ni nchi ya kiislam na wakristo wanakuwa grouped 'wananchi wengine' then i can smell further discrimination baada ya kuvunja muungano kama ule wa Sudan yaani wazanzibar wakristo kutokuwa na chao. kama zanzibar inanyanyswa kutokana na uislam wake basi waislam ni dhaifu kupita maelezo na mnaongozwa na matumbo badala ya akili. walioshika dola ni CCM so wanaowanyanyasa ni CCM yet Mufti wenu yuko bize kuitetea CCM-so low!! Zanzibar tata sana!! ham'bebeki wala hampendeki-KWENDENI ZENU MCHINJANE!!
   
 7. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #7
  May 18, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  ni yaleyale ya kusema sikuiba VX bhana, niliibla GX.... its crime!!!

  aniwei mie hata kusoma hilo tangazo sina muda, naangalia comments tu za waliosoma

  tunahangaishana bure wakati muungano hauna maana
   
 8. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #8
  May 18, 2011
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Hii hatari mazee!
   
 9. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #9
  May 18, 2011
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160

  Nimesoma yote!

  Kuna waislam na waislam wa Zanzibar! Chuki za Kidini na chuki zaidi ya Muungano

  Kama Kawaida waislamu kulalamika pasipo hata na sababu

  Haya endeleeni Kulia lia na UAMSHO

  Onyo: Msilete mambo ya Ugaidi, Al Qaeda na Ahmed Khalfan Ghailani ambaye yuko jela.
   
 10. M

  Mbwazoba Member

  #10
  May 18, 2011
  Joined: May 5, 2011
  Messages: 93
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ujinga kabisa huu, eti sio 70 ni 29 tu, nyooo hiyo sio kitu kwako wewe mjinga kabisaaaaaaaaaaaa...yaani unataka kuhalarisha uhalifu huo wa waislamu wa kuijchukulia sheria mkononi? pum.....vu kabisa wewe, au ndio mnatetea wazenji wenzenu wa bara...yaani tukianzisha sisi huku mtaisoma tu, mm naomba muungano ufe halafu muone nyie mashetani wakubwa kabisa, kwa hiyo tuamini kuwa wazenji ni ruksa kuuana?
  usiropoke hapa..na huo ujinga wenu wa kataarifa ka kijinga.
   
 11. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #11
  May 18, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  yanini malumbaano, yanini manenoo
  najiweka pembeeni, naepuka msongamano
  bora nituliee, nipate changu na miee
  bora nituliee, haya yasinirudiee

  Mkuu it aint worth it, kama mtu hataki mwache, hakuna haja ya hata kumsikiliza hoja zake kwani conclusion yake huwa moja tu, HATAKI!!!
   
 12. Felixonfellix

  Felixonfellix JF-Expert Member

  #12
  May 18, 2011
  Joined: Feb 16, 2010
  Messages: 1,680
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  SMZ siku hizi mnasemewa ati!!!!!!!!!!
   
Loading...