Amefariki mchana wa leo, Hospitali ya Taifa - Muhimbili baada ya kuugua kwa muda mrefu.
Kila nafsi itaonja mauti - naam, sisi ni mavumbi, na mavumbini tutarudi
Pia soma
Tanzania inalia kifo cha mwanafalsafa, mtaalamu wa sheria na mwanadiplomasia maarufu, Profesa Costa Ricky Mahalu, aliyeaga dunia katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete jijini Dar es Salaam.
Alikuwa na umri wa miaka 77.
Mmoja wa familia yake alithibitisha kwa gazeti la The Citizen kwamba Prof Mahalu alifariki kwa amani hospitalini.
Alizaliwa Julai 9, 1948, katika Kijiji cha Katunguru, Wilaya ya Sengerema, mkoani Mwanza (eneo lililo sasa ni Mkoa wa Mwanza). Prof Mahalu aliunda taaluma ndefu katika nyanja za elimu, diplomasia na huduma za umma.
Alianza elimu yake katika wilaya yake ya asili kabla ya kuhudhuria Shule ya Upili ya Kibaha kwa masomo ya O-Level na baadaye Shule ya Upili ya Mkwawa kwa masomo ya A-Level.
Mnamo 1971, alipata mafunzo ya kijeshi ya msingi katika Kambi ya Jeshi la Taifa Makutupora, Dodoma kabla ya kujiunga na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), ambapo alihitimu shahada ya kwanza ya sheria (LLB) mwaka 1974.
Mwaka mmoja baadaye, alijiunga na UDSM kama mhadhiri msaidizi katika Fakulti ya Sheria. Kati ya 1976 na 1978, alisomea shahada ya uzamili ya sheria huku akiendelea kufundisha.
Mnamo 1979, Prof Mahalu alisafiri hadi Hamburg, Ujerumani, kwa ajili ya masomo ya uzamivu na kupata PhD ya Sheria mwaka 1983. Aliporudi Tanzania, alipandishwa cheo kuwa mhadhiri mkuu katika UDSM.
Taaluma yake ilipanuka kimataifa aliporudi Ujerumani mwaka 1990 kama mhadhiri kabla ya hatimaye kuteuliwa kuwa profesa wa sheria katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Prof Mahalu pia alihudumu kama Mkurugenzi wa Elimu ya Juu kati ya mwaka 1992 na 1996, akichangia katika utengenezaji wa sera na usimamizi wa sekta ya elimu ya juu nchini.
Mnamo Oktoba 1996, alijiunga na Wizara ya Mambo ya Nje, kuashiria mwanzo wa taaluma yake ya diplomasia. Aliteuliwa Ujerumani kama msaidizi wa balozi wa Tanzania kabla ya hatimaye kuwa Balozi wa Tanzania nchini Italia kutoka mwaka 2000 hadi 2006.
Zaidi ya diplomasia, Prof Mahalu aliendelea kuchangia katika elimu ya sheria, akiwemo mhadhiri katika Chuo Kikuu cha St. Augustine, Tanzania.
Katika maisha yake yote, alitambulika sana kwa kujitolea kwake katika kukuza taaluma ya sheria na huduma za umma nchini Tanzania.
Prof Mahalu atakumbukwa kama mwanafalsafa wa heshima, mwanadiplomasia mwenye uzoefu na mwalimu mwenye dhamira aliyesaidia kuunda elimu ya sheria na uwakilishi wa kimataifa kwa Tanzania.
Costa Ricky Mahalu ni nani?
Profesa Costa Ricky Mahalu alizaliwa Julai 9, 1948 katika Kijiji cha Katunguru, Wilaya ya Sengerema, Mkoa wa Geita. Baada ya kumaliza elimu ya msingi, Mahalu aliendelea na masomo ya sekondari katika Shule ya Upili ya Kibaha, ambapo alimaliza kiwango cha ordinary level kabla ya kujiunga na Shule ya Upili ya Mkwawa.
Mnamo 1971, alijiunga na Kambi ya Jeshi la Taifa Makutupora huko Dodoma kwa mafunzo ya kijeshi kabla ya kuendelea na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) ambako alihitimu shahada ya sheria mwaka 1974.
Mnamo 1975, Mahalu aliajiriwa na UDSM kama mhadhiri msaidizi katika Kitivo cha Sheria. Alisomea shahada yake ya pili ya sheria kuanzia 1976 hadi 1978 huku bado akifundisha chuoni. Mnamo 1979, alienda Hamburg, Ujerumani Magharibi, ambapo alipata shahada ya uzamili (PhD) mwaka 1983. Baada ya hapo alirudi UDSM na kupandishwa cheo hadi mhadhiri mkuu.
Mnamo 1990, alienda Ujerumani tena na kuajiriwa kama mhadhiri, lakini alirudi UDSM baada ya mwaka mmoja na kuteuliwa kuwa profesa wa sheria. Baada ya mwaka mmoja na nusu kazini, aliteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Elimu ya Juu, nafasi aliyoshikilia kuanzia 1992 hadi 1996.
Mnamo Oktoba 1996, alihamishwa kwenye Wizara ya Mambo ya Nje, na baadaye kutumwa Ujerumani kama msaidizi wa balozi. Mnamo 1999, aliteuliwa kuwa balozi wa Tanzania nchini Italia, ambapo alihudumu kuanzia 2000 hadi 2006.
Profesa Mahalu pia alifundisha sheria katika Chuo Kikuu cha St Augustine cha Tanzania.
====
Mahalu alikuwa na leseni au usajili wa uwakili namba 477 yaani namba yenye digit au tarakimu tatu. Huyu ni mmoja wa walimu wakongwe wa sheria nchini wa rika la Prof Issa Gulamhussein Shivji, Prof Gamaliel Mgongo Fimbo, Prof Kanywanyi na Prof Leonard Paul Shaidi.
Prof Mahalu aliwafundisha pale Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Kitivo cha Sheria, miaka ya themanini akina Prof Chris Peter, Prof. Asha Rose Mtengeti-Migiro, Prof Zebron Gondwe, Prof Jwani Mwaikusa, Prof. Ibrahim Hamisi Juma, Prof. Luitfried Mbunda, Prof. Palamagamba John Kabudi, Prof. Bonaventure Rutinwa, Dr. Sengondo Mvungi, Dr. Masumbuko Roman Mahunga Lamwai, Dr. Ringo Willy Tenga, Dr. Harrison Mwakyembe, na wahadhiri wengine waliotufundisha sisi wa vizazi vya miaka ya tisini na elfu mbili ambao ni majaji, mahakimu na mawakili wa leseni zenye namba za tarakimu nne (four digits roll numbers).
Prof. Mahalu alibobea katika sheria za kimataifa na ndio maana alipokuwa balozi katika nchi za Ulaya alikowahi kuishi enzi akisoma na kufundisha, alifanya vizuri katika diplomasia. Aliiheshimisha Tanzania hasa katika mahusiano na Vatican, makao makuu Kanisa Katoliki lenye hadhi ya Serikali, wakati akiwa Balozi wetu nchini Italia. Ndio maana sikushangaa mnamo tarehe 09.03.2026 habari za kifo chake zilipotangazwa pia katika vyombo vya habari vya Vatican hususan Vatican News.
Prof. Mahalu amewasaidia vijana wengi wasomi wa sheria kwa kuwafadhili, kuwatia moyo na kuwapa fursa ya kazi akiwemo binti yangu Dkt. Norga Alloyce Komba, aliyesoma shahada ya kwanza na ya pili ya sheria katika chuo kikuu alichokianzisha kikiwa pia na kozi za uongozi cha Bagamoyo ingawa sasa hakipo tena. Prof. Mahalu alikuwa ni Msomi Makini, Muungwana, Mpole, Mwema, Mkarimu, Mnyenyekevu, Muadilifu, Mzalendo na Mcha Mungu.
Wanafunzi wengine wa Prof. Mahalu ni kaka zangu wangoni Prof. N. N. N. Nditi, Prof. Florens Luoga, Dr. Wilbert Kapinga, Dr. Mapunda Senior, na Dr. Mapunda Junior. Pia kuna yule msomi mwenye akili sana, Robert Makaramba (rtd Judge) niliyekuta sifa zake za kitaaluma shule ya Sekondari ya Mzumbe ("O" Level & "A" Level) kwa kufaulu masomo yote ya arts na science.
BWANA ALIMTOA PROFESA MAHALU,
BWANA AMEMTWAA PROFESA MAHALU,
JINA LAKE LIHIMIDIWE.

- Rais Magufuli amrudishia Ubalozi Prof. Costa Mahalu baada ya kushinda kesi ya uhujumu uchumi
- (Docs): Siri ya Kesi ya Mahalu: Ununuzi wa Jengo la Ubalozi Italia
- Benjamini Mkapa atinga mahakamani kutoa ushahidi kesi Ya Balozi Profesa Costa Mahalu
- Profesa Costa Mahalu aibwaga serikali kortini