Balozi mstaafu apata pigo kortini | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Balozi mstaafu apata pigo kortini

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by Rutashubanyuma, Jul 6, 2011.

 1. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #1
  Jul 6, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,305
  Likes Received: 418,551
  Trophy Points: 280
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: contentheading, width: 100%"]Balozi mstaafu apata pigo kortini
  [/TD]
  [TD="class: buttonheading, width: 100%, align: right"] Send to a friend [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: createdate"] Tuesday, 05 July 2011 20:46
  [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]

  Daniel Mjema,Moshi
  MAHAKAMA Kuu ya Tanzania imemuamuru Balozi wa zamani wa Tanzania nchini Msumbiji, Abubakar Nkya kuilipa Kampuni ya Benandys iliyokuwa ikiendesha mgahawa wa Coffee Bar wa mjini Moshi fidia ya zaidi ya Sh 1.2 bilioni.

  Uamuzi huo ulitolewa Ijumaa iliyopita na Jaji Kipenka Mussa wa Mahakama Kuu kitengo cha ardhi kufuatia kesi ya msingi iliyofunguliwa mwaka 2005 na Kampuni ya Benandys Ltd dhidi ya Balozi Nkya na mkewe,Sophia Ibrahim.

  Balozi Nkya aliwahi pia kuwa Mkuu wa Itifaki Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wakati wa uongozi wa Serikali ya awamu ya tatu.Kiini cha mgogoro huo ni hatua ya Balozi Nkya ambaye alikuwa mpangaji katika nyumba ya Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) kuikodishia Benandys mgahawa wa kisasa wa Coffee Bar, lakini Balozi Nkya akaufunga ghafla Februari 24, 2005.

  Benandys ikiwatumia mawakili mashuhuri Dar es Salaam, Cresencia Rwechungura na Jamhuri Johnson ilifungua kesi ya madai namba 2/2005 ikilalamikia kitendo cha Balozi Nkya kuvunja mkataba huo wa kibiashara.

  Kwa mujibu wa hati ya madai iliyowasilishwa mahakamani, licha ya kuwa na mkataba hai wa uendeshaji wa mgahawa huo, lakini walishangaa asubuhi ya Februari 24 walipofika katika mgahawa huo kukuta makufuli mapya milangoni.

  Kampuni hiyo inayomilikiwa na Mtanzania Ian Moshi anayemiliki vitega uchumi kadhaa Dar es salaam, Arusha na nchini Afrika Kusini ililalamikia kupata hasara kutokana uamuzi huo na mali zilizokuwamo ndani kuharibika.

  Akitoa uamuzi wa kesi hiyo, Jaji Mussa alisema malalamiko ya Benandys ni ya msingi hivyo alimuamuru Balozi Nkya na mkewe kulipa kampuni hiyo Sh500,000 kila siku kuanzia Februari 24,2005 alipovunja mkataba hadi siku ya hukumu hiyo.Kimahesabu tangu kipindi hicho hadi sasa ni karibu siku 2,300 ambazo zinafanya kuwa malipo hayo ya hasara ya kibiashara yafikie Sh1.15 bilioni.Mgahawa huo ulikuwa ukitoa huduma kwa watalii na Watanzania, Internet na uuzaji wa vitabu.

  Halikadhalika Jaji Mussa alimuamuru Balozi Nkya na mkewe kulipa fidia ya Sh50 milioni, kulipa gharama za kesi na pia kuifidia kampuni ya Benandys mali zilizokuwmo ndani zinazofikia thamani ya Sh200 milioni kwa viwango vya bima.


  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]

   
 2. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #2
  Jul 6, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,305
  Likes Received: 418,551
  Trophy Points: 280
  Kuna walakini mkubwa wa hii hukumu......................................madai ya Tshs 500, 000/= kwa siku ni lazima yandamane na ushahidi wa ulipaji kodi na kuwa hiyo siyo faida ambayo wadai ndiyo waliyokuwa wanastahili kulipwa..............................huwezi kulipwa turnover bila ya kuondoa gharama za uendeshaji wa kuipata hilo.......................it is a huge miscaariage of justice na wahusika wapaswa kufungua shauri la rufaa kupingwa tuzo ambazo hazizingatii ushahidi, hali halisi na n.k
   
Loading...