Game Theory
JF-Expert Member
- Sep 5, 2006
- 8,546
- 847
unafiki uliozidi kipimo kutoka kwa balozi wetu Mrs Maajar. alidai hatowabuagua watu lakini ukiwa mfadhili wa CCM basi atachma mafuta all the way ili sura yake ionekane tuu
Kama mtakumbuka mwezi April (10th of April) I believe kulitokea misiba 2 Reading. Marehemu Peter Gachuma na Thomson Msigwa walifariki kwenye ajali ya gari huko Mwanza.
Baada ya wiki moja (I think April 20th) familia ya Peter Gachuma na jamaa wengine waliokuwa wanasali nao kanisa moja walifanya misa maalum ukumbi wa 79 London Road, Reading kumuombea marehemu na pia kutoa shukrani kwa ushirikiano walioupata.
Katika misa ile hakukuwa na MUWAKILISHI wala SALAMU za rambirambi kutoka Ubalozini. Misa iliendelea na kumalizika salama salimini, msiba ukafungwa rasmi.
Siku na wiki zikapita, jana kukawa na misa nyingine ya kumuombea marehemu na hasa kwa familia ya Gachuma kutoa shukrani tena, pale pale ukumbi wa 79 London Road, Reading ambapo Mzee Gachuma mwenyewe (Baba wa marehemu Peter) kutoka Mwanza naye alikuwepo. Guess what Balozi Mwenyewe (Mrs Majaar) na Mumewe nao walikuwepo. All the way from London kuja kuhudhuria misa ya msiba uliotokea a months and a half ago ambao hawakutuma wala samu za rambirambi.
Sasa unaweza kujiuliza unafiki hapo upo wapi; Mzee Gachuma ni tajiri mkubwa Mwanza kwa sababu ya hisa zake Coca Cola na business nyingine na pia mfadhili mzuri wa CCM. Balozi Maajar hakujali msiba ulipotokea bali pale tu mfadhili wa CCM alipotua mjini ndipo akajitokeza kuonyesha sura. Kwa hili amenichosha kupita kipimo.