Balozi Juma Mwapachu atangaza kurejea CCM...

hatuwataki hata waje na mabilioni ya dola
 
hivi mwapachu ni nani vile?
 
Siasa ni sayansi!

Ukikosea formula utapata solution ya ajabu!

Mafuriko ya kutengeneza yaliwafanya wakawa vipofu kifikra!

Msanii alifanya kazi yake iliyosababisha baadhi kukumbwa na mafuriko ya kutengeneza!

Kufanya kosa sio kosa, kosa ni kurudia kosa!

Ukweli hutumia ngazi kuwafikia walengwa!

Ukweli umeanza kuwafikia!

By the way. Mambo ya kuhama hama vyama wawaachie vijana. Wewe umezeeka ukiwa ndani ya chama halafu baadaye unatuambia eti chama kimepoteza mwelekeo au kimekosa pumzi!

Wazee wa aina ya Juma Mwapachu ni hatari sana katika ustawi wa Taifa kwa sababu kwao tumbo ni kila kitu. Wako tayari hata kuua ili washibishe tumbo lao.

Watu kama Mzee Warioba au Butiku hawaho ndani ya CCM kwa sababu CCM ni nzuri sana, la hasha. Wako ndani ya CCM kwa sababu heshima yao wameipata ndani ya CCM.

Kwenye utawala wa Rais Magufuli tutaona na kusikia mengi!
 

Nchi hii bado sana. Mzee huyu anafanya sarakasi ili siku isogee.
 
duuuu kweli lowasa aliitisha ccm haswaaa,hili jemedari la kisiasa tz ni wakukumbukwa na kuigwa,ila ndo basi tena cdm imeimarika ajabu na zaid ya yote piga ua hapa harudi mtu hicho chama alaaaa.magu aendelee na maigizo 2020 sisi tunamteketeza kama kawa
 
Naona lile shirika la Regional Aviation analoendesha mtoto wake pale Arusha ndilo limemfanya huyu mzee kurudi mbio CCM... Baada mtoto wake ana kesi kibao kule mahakama kuu ya Arusha za kulangua wafanyakazi wa hiyo Kampuni...
 
mambie aendapo awasalimie,cdm ni dini ya pili ndani ya watz sasa,piga ua haturudi nyuma,cdm ni vijana na vijana ndo taifa,cdm ni wasomi na wasomi ndo dira ya nchi hatutorudi nyuma mapambano daima
 
Ndio wanasiasa wa wetu hao
 
Nina mashaka makubwa kama huyu mzee ndiye kaandika hii lisala. Kama hajaandikiwa basi hana marafiki wazuri wa kumshauri. Ni aibu Kabisa.

Check hizi sentensi:

"Nililewa mahaba ya Lowasa, nililewa ahadi ya Lowasa kunipa uwaziri wa mambo ya Nje. Niliamini mafuriko ya Lowasa ambayo yakanifanya niamini kabisa anachukua nchi. Tulikubaliana na wenzangu kwamba wiki mbili za mwisho tuihame CCM kwa wimbi kubwa ili kuitikisa na kuitoa madarakani. Lakini baadhi wakaogopa na hadi sasa wengine wamebaki CCM na wana vyeo."

"Niliamua kulifanya jambo kubwa ili kumsaidia Lowassa. Na sasa nimeamua kulifanya jambo kubwa ili Magufuli ajue sasa niko naye kwasababu sitaki shughuli zangu na za washirika wangu zikwamishwe na Serikali kwasababu tu huko nyuma niliamua kumsaidia swahiba wangu."

Dah nimesikitaka sana na haya maneno. Sana tu, Sana tu, Sana tu, Sana tu, sana tu. Hawa ndiyo wanasiasa wetu. Dahhhhhhhh
 
2020 ni mbali sana. maisha ni magumu, ni wachache wenye kuvumilia....
 
Hii nchi haina uzalendo, kama mtu anaweza hama Chama kwa sababu ya cheo mtu huyo hawezi kujitenga na ufisadi, hatakiwi kupokelewa tena na Chama msaliti kama huyo.
 
Haya maelezo kama maogizo vile. kama ya mtoto wa shule
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…