Balozi Dr. Slaa uso kwa uso na wabunge 14 wa CHADEMA kwenye msiba wa mdogo wake

gost

JF-Expert Member
Dec 31, 2012
275
135
Balozi wa Tanzania nchini Sweden, Dkt. Wilbroad Slaa akiteta na Mbunge wa Arusha Mjini -Chadema ndugu Godbless Lema kwenye mazishi ya mdogo wake Francis Peter Qamara.

Mazishi hayo yamemkutanisha na na Wabunge na Viongozi wa CHADEMA.

Slaa.jpg
 
Ni kujipendekeza tu
Mtu waliomwita msaliti,Dr Mihogo,Samsoni na kila baya kumuombea.Kweli chadema wamefulia

..inawezekana marehemu, mdogo wake Dr, alikuwa ni mwana-chadema.

..pia ktk masuala ya kifo, wanasiasa huweka tofauti za kiitikadi kando.

..Utakumbuka Mzee Kingunge msiba wake ulihudhuriwa na viongozi na wanachama wa vyama mbalimbali vya siasa nchini.
 
Mkuu ni lazima tukiri kwa kweli.
Kukubali kukipoteza hiki kichwa ndio imekuwa kifo cha CHADEMA.
Na kwa mwenendo ninaouona kwa sasa, wacha tuendelee kumsingizia JPM na Polepole tu, lakini ukweli tulijiua wenyewe 2015.
Chama kwa sasa kimebaki na washangilia kukamatwa kwa Bombadier zetu tu na kushabikia ACACIA tu.
 
..nakubaliana na wewe kwa 50%.

..kwasababu sidhani kama aina ya siasa alizokuwa akiendesha Dr.Slaa zingeruhusiwa ktk zama hizi.

..kama TL kamiminiwa risasi 30+, hudhani kwamba Dr.Slaa angeshambuliwa kwa silaha nzito zaidi kama mabomu au maguruneti?

..
 
Back
Top Bottom