Balozi Ally Karume anamjibu mama Samia Suluhu kuhusu nafasi namba mbili ya Tanzania

Huu muungano hata siuelewi...ngoja akirudi Mwalimu Nyerere anaweza lkutoa ufafanuzi!

Mwl Nyerere amesharudi, alirudi November 2015 kwa mbwembwe haswa, ila kwa jina la Dr John Pombe Joseph Magufuli ambaye ndiye Rais (tena) kwa sasa. Viwanda vyote vilivyozikwa na awamu ya tatu na nne pamoja na mashirika yote ya umma yanarudi na mifano ipo(Reli, Ndege). Tunaimani kuwa nyumba zote zitarudishwa na ili aweza kukamilisha kazi hii ni lazima huyu Mwl Nyerere II aendelee kupiga kazi mpaka 2035 kwa ruksa ya kura za Wananchi.
 
Balozi anashushua huyo..nakumbuka mahojiani yake na niliwahi kukutana nae Ile bar ya CCM Zanzibar pale..he's funny and smart, Ana exposure ya kutosha na anakitaka kitu Cha u-Rais znz kwa udi na uvumba'

Umeanza vizuri ila mwishoni umeharibu kwa kusema kuwa nae pia anauhitaji mno Urais wa Zanzibar. Hana shida wala nia hiyo na hili nina uhakika nalo kwa 100%.
 
Mkuu miaka yote Maaalim seif anashindda uchaguzi zenj.Hiyo nimeambiwa na mtu mkubwa kabisa ccm

Eti umeambiwa!! yaani hujayaona ila unasikia ya uswahilini, umbeya na vitina!! Maalim hajawahi kupata ushindi Visiwani Zanzibar tangu 1995, ni porojo za wale waliopinduliwa na kukimbia nchi Januari 1964. Period. Waambie wakajifunze kwa yaliyompata Shah kule Iran 1979!!Period.
 
UONGO iko kama huu wako, Unadaki tu maisha ya watu kama kwamba huna pesa ya kula na kunywa pombe

Ally Karume chapombe hasa hata chai huwa hanywi hudamkia kwenye pombe yeye Ni masaa 24 pombe kichwani.Kumnukuu kwa lolote Ni kumwuonea sababu muda mwingi anakuwa kalewa njwiiii
 
Balozi ALI KARUME ampa ukweli Samia Suluhu , alipotoa kauli yeye ndio number mbili hana shida ya urais wa Zanzibar.

Asema Mzee Karume ndio alikuwa number mbili yeye amebaki number mbili inaoyelea hewani, kwani 2015 hakupata kura za kutosha kutoka kwa Wazanzibari kama kupata kura nyingi za Wazanzibari Mzee Duni ndio aliepata kura nyingi za Wazanzibari ndie angepwaswa kuwa Makamo wa Rais lakini mfumo huu hewa na sisi tunacheza ngoma inayotumaliza Wazanzibari.

Amesema Mzee Karume aliheshimika na kukubalika na Mzee Jumbe wengine kwenye muungano kwa vile wanaposafiri popote duaniani walikuwa wanapata itifaki zinazostahili kwa Rais wa Zanzibar.

Leo unajishebedua kuwa wewe number mbili anasema kuwa Wazanzibari hawakutaki wamekukataa.


Kujua Makamu wa Rais, Mama Samia Suluhu alichoongea, soma

,
Pale Mwangalizi wa Uchaguzi wa Zanzibar Ndugu Alli Karume anapokiri waziwazi kwamba CCM iliangukia pua hii inamaanisha nini ?
 
Watu kwanza watafute mzanzibar halisi ni nani haswa.
Ni yule aliyezaliwa Bara na wazee kutoka Bara baadae akahamia Zanzibar, akapewa kitambulisho cha ukaazi cha Zanzibar na kupiga kura katika chaguzi za Zanzibar na za Tanzania.
 
Balozi ALI KARUME ampa ukweli Samia Suluhu , alipotoa kauli yeye ndio number mbili hana shida ya urais wa Zanzibar.

Asema Mzee Karume ndio alikuwa number mbili yeye amebaki number mbili inaoyelea hewani, kwani 2015 hakupata kura za kutosha kutoka kwa Wazanzibari kama kupata kura nyingi za Wazanzibari Mzee Duni ndio aliepata kura nyingi za Wazanzibari ndie angepwaswa kuwa Makamo wa Rais lakini mfumo huu hewa na sisi tunacheza ngoma inayotumaliza Wazanzibari.

Kwa upeo wa busara za Balozi Karume, ana maana kwamba watu wa Dar na Mbeya kama hawakumpigia kura za uraisi Magufuli basi Magufuli sio raisi wao bali ni Raisi wa kanda ya Ziwa waliompigia kura kwa wingi.

Labda pia ndio mentality ya Magufuli - na ndio maana Dar wanaweza kubomolewa nyumba kupanua barabara, na Mwanza hawatabomolewa.
 
Huyo balozi ndiye "baba mzazi" wa shangazi Fatuma eeeeeeeeeeeee naona kama wanashabihiana
 
Back
Top Bottom