Mwanahabari Huru
JF-Expert Member
- Mar 9, 2015
- 14,243
- 34,903
Andaandika Kada mtiifu wa CCM Bollen Ngetti
RAIS wangu Magufuli, laiti kama ungekubali ushauri wangu kwako kupitia "pale" kwamba ukubali kurudisha na kustawisha utawala bora kama nilivyoeleza, fedheha na aibu hizi za kina Gavana Makonda & co zisingetokea.
Kitendo cha Gavana Makonda kumtuhumu Mbowe kushiriki biashara ya ngada, kumkamata, kumpekua na kumkuta na makaratasi na Kisha yeye (Mbowe) kuwafungulia kesi wateule Wako, nao kuamua kuingia mitini kukwepa Mahakama na sasa nd...io wanaosakwa ni aibu, ni fedheha na pigo kwa utawala wa nchi. Kwamba inatokea simba anamfukuzia swala kwa ajili ya mlo na ghafla yule swala anageuka na kuanza kumfukuza simba! Ni maajabu ya dunia Tanzania.
Taarifa niliyonayo ni kwamba Mahakama imeapa kulinda heshima yake kwa gharama yoyote. Bunge linakuvutia pumzi mwezi Aprili. Rais wangu, mzaha mzaha hutungua usaa. Bunge linajipanga, linajisuka kuangusha Serikali yako. Namuonea huruma PM Majaliwa uliyemuambia, "hukuzaliwa Waziri Mkuu". Kwa nini nchi ikaye kwenye tension watu wasijue kesho yao?
Rais wangu mpendwa, binafsi ninakupenda kweli! Lakini nakuonea huruma kuwa umezungukwa na wanafiki wasiotaka kukuambia reality on the ground. Kwa sasa huna option zaidi ya kuruhusu utawala bora unaoheshimu Katiba na Sheria. Ni hapo nchi itapona.
Usichukie umma mpana kwa wapiga dili wasiozidi 20 kwa watu 50 milioni. Mungu akupe ujasiri kuupokea ushauri huu wa hekima. Wakigoma kukuambia mimi ninakutonya. Tendeaneni haki mnunue amani maana kinyume cha utawala bora ni machafuko!
[HASHTAG]#UzalendoKwanza[/HASHTAG]!