Balaa ni zito mchepuko kashika mimba

Balaa ni zito mchepuko kashika mimba

Yaani demu anapata mimba halafu mchizi anachanganyikiwa kiasi kwamba inabidi atulizwe?? Heheheh huyo muhuni anafeli sana.

[emoji1][emoji1][emoji1]aloo
 
Amuoe mchepuko. Aachane na huyo fiance. Naona deep kasema mwanaume msimamo. Fiancee angeshika mimba huyo jamaa angeoa??? Ili kuonesha responsibility mwanaume abebe jukumu lake ipasavyo. Mwanaume una mwanamke na mmeshaamua kuianza safari. Unataka kuiga watu wenye ndoa za miaka 20 au 10...smh

Hakuna ndoa apo. If he cheats b4 marriage..he will always cheat

Yeah sure exactly
 
Mwambie asipaniki.
Atulie. Mwanaume hapaswi kupanic. Tumeumbwa kuhimili mihemuko.

Huyo side chiki ampe matumizi tu na kulea hiyo mimba.

Asithubutu kushauri atoe hiyo mimba au kumkimbia.

Kwa huyo mke wake litajibika mbele kwa mbele. Akigundua akaleta vagi atampiga chini anaoa mama kijacho.

Atakuja kunishukuru baadaye.

Yeah mkuu hiyo good idea
 
Acha huu ushauri mkuu.
Nina ushuhuda mmoja matata Sana
Anayehitaji atanifuata inbox.
Lakini usithubutu kutaka kutoa mimba ambayo ndio imeshatungika.
Kama uwezo wa kulea unao Lea hiyo mimba.

Tupe ushuhuda mkuu watu wajifunze mengi
 
Hakuna balaa lolote hapo jamaa amuoe huyo mchumba wake kimyakimya mambo mengine yatajiseti mbele kwa mbele mbona mimi nina mchumba na ndoa mwakani nimepiga mimba watu wawili na mmoja ni mke wa mtu na niko poa tu nimekula mikausho mikali.

[emoji23][emoji23][emoji23]aaah we jamaa gaidi sana
 
Habar wana JF.
Natumaini wazima?
Niende kwenye mada bila kupoteza muda.

Leo bhana mida ya mchana nilipokea simu kutoka kwa rafiki yangu wa karibu sana ambaye huwa tunashirikiana mambo mengi mbalimbali. Akaniambia ana maongezi na mimi muhimu sana, nikamwambia sawa hakuna shida ila nipo kazini na yeye akasema yupo kazini, ila akitoka kazini kwake atakuja tuonane nikamwambia sawa.

Basi mida ya jioni hivi kwenye saa 11 akanipigia, nikamwambia bado nipo ofisini kuna kazi naimalizia ila unaweza kuja, akasema sawa nakuja. Basi hapo kweli baada ya muda akafika kazini kwangu nikampokea kwakuwa muda wa kazi ulishaisha na wafanyakazi walishaondoka mimi ndiyo nilibakia namalizia kazi zangu. Nikamkaribisha tukae tuongee anieleze nini shida.

Ndiyo akaanza kunieleza, kiukweli jamaa yangu huyu ana mazito na kipengele kigumu sana. Ishu ni kwamba kwanza yuko na mchumba ambaye tunamjua na washa posana kila kitu bado kuona tu karibuni. Sasa shida jamaa alikuwa na mchepuko ambaye anatoka naye ukiachana na mchumba wake. Sasa kilichotokea kwa bahati mbaya mchepuko kashika mimba na baada ya kuelezwa jamaa kamchukua kaenda naye hospital kumpima, majibu imekuja positive kitu kimenasa.

Sasa jamaa kachanganyikiwa vibaya mno, kiukweli hayuko sawa mpaka namuonea huruma. Yuko overstressed na nimejaribu sana kumtuliza lakini bado hayuko sawa na haelewi afanye nini. Kila achokifanya anaona hakiendi, kwa mtu asiyejua hili ukikaanae anazuga tu yuko fine lakin kiuhalisia hayuko sawa.

Wakuu tushauriane mawazo tujue tunamsaidije kijana mwenzetu kwa ushauri tu.

Mungu awabarki karibuni sana [emoji120]

Alitakiwa achanganyikiwe kwa kuwa na mchumba na mchepuko kwa wakati mmoja na sio kwa mchepuko kuwa na mimba

Mwambie aache mchumba ambaye hana mimba ili aoe mchepuko wenye mimba maana kumwacha ni kutelekeza mama wa mtoto wake pamoja na mwanae wa damu
 
Si ndio matokeo ya umalaya au alitaka ashike homa!!!
 
Back
Top Bottom