Balaa ni zito mchepuko kashika mimba

Balaa ni zito mchepuko kashika mimba

knows

JF-Expert Member
Joined
Nov 9, 2021
Posts
1,453
Reaction score
2,239
Habar wana JF.

Natumaini wazima?

Niende kwenye mada bila kupoteza muda.

Leo bhana mida ya mchana nilipokea simu kutoka kwa rafiki yangu wa karibu sana ambaye huwa tunashirikiana mambo mengi mbalimbali. Akaniambia ana maongezi na mimi muhimu sana, nikamwambia sawa hakuna shida ila nipo kazini na yeye akasema yupo kazini, ila akitoka kazini kwake atakuja tuonane nikamwambia sawa.

Basi mida ya jioni hivi kwenye saa 11 akanipigia, nikamwambia bado nipo ofisini kuna kazi naimalizia ila unaweza kuja, akasema sawa nakuja. Basi hapo kweli baada ya muda akafika kazini kwangu nikampokea kwakuwa muda wa kazi ulishaisha na wafanyakazi walishaondoka mimi ndiyo nilibakia namalizia kazi zangu. Nikamkaribisha tukae tuongee anieleze nini shida.

Ndiyo akaanza kunieleza, kiukweli jamaa yangu huyu ana mazito na kipengele kigumu sana. Ishu ni kwamba kwanza yuko na mchumba ambaye tunamjua na washa posana kila kitu bado kuona tu karibuni. Sasa shida jamaa alikuwa na mchepuko ambaye anatoka naye ukiachana na mchumba wake. Sasa kilichotokea kwa bahati mbaya mchepuko kashika mimba na baada ya kuelezwa jamaa kamchukua kaenda naye hospital kumpima, majibu imekuja positive kitu kimenasa.

Sasa jamaa kachanganyikiwa vibaya mno, kiukweli hayuko sawa mpaka namuonea huruma. Yuko overstressed na nimejaribu sana kumtuliza lakini bado hayuko sawa na haelewi afanye nini. Kila achokifanya anaona hakiendi, kwa mtu asiyejua hili ukikaanae anazuga tu yuko fine lakin kiuhalisia hayuko sawa.

Wakuu tushauriane mawazo tujue tunamsaidije kijana mwenzetu kwa ushauri tu.

Mungu awabarki karibuni sana [emoji120]
 
Kawaidatu aache mbwemwe
JamiiForums-2066188776.jpg
 
Mwambie akatoe posa pia kwa side chick halafu amuoe side chick, avunje ule uchumba wake wa mwanzo na huyu mwanamke wa mwanzo

Mkuu soi rahsi kama unavofikiria
 
[emoji23]

Mkojo wa mjamzito: Biashara nyingine ya siri isiyojulikana na wengi
 
Sioni Tatizo,

Wanaume wengi tu wamezaa kabla ya kuoa rasmi, hicho Ni kipimo Cha Upendo wa fiance wake kwake.

Kama kweli fiance anahitaji ndoa na jamaa, kamwe hatayumbishwa na Hilo.

Cha muhimu jamaa asionyeshe unyonge, fiance atampanda kichwani.

Asimamie kwamba kaamua kumuoa yeye na sio uyo side chick, Kama hawezi aachie ngazi side chick avishwe shella.

Mwanaume msimamo bhana[emoji4]
 
Sioni Tatizo,
Wanaume wengi tu wamezaa kabla ya kuoa rasmi, hicho Ni kipimo Cha Upendo wa fiance wake kwake.

Kama kweli fiance anahitaji ndoa na jamaa,kamwe hatayumbishwa na Hilo.

Cha muhimu jamaa asionyeshe unyonge, fiance atampanda kichwani.

Asimamie kwamba kaamua kumuoa yeye na sio uyo side chick, Kama hawez aachie ngazi side chick avishwe shella.

Mwanaume msimamo bhana[emoji4]

Yeah mkuu nikweli kabsa
 
Watu acheni comment za kinafiki . Sikiliza mwambie huyo jamaa yako sijui wewe atafute MISO kwisha habari au vinginevyo achague moja kuvunja uchumba na huyo mchumba wake abaki na side chick au ajinyonge huyo rafiki yako. Inshu ndogo kama hiyo anachanganyikiwa nini

Sent from my SM-J111F using JamiiForums mobile app

Mkuu unge fikiria kwa makin lakin
 
Mi nilijua kakua kumbe ni shu ndogo hivyo.
Ukipanda wakati wa masiku ujue kuna palizi na mavuno.
Wa kumshauri hapa ni masanja amtafute

[emoji16][emoji16][emoji16] hayaa bhana
 
Back
Top Bottom