Bakora Zatembea Kwa Wanawake Wanaovaa Suruali nchini Sudan | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Bakora Zatembea Kwa Wanawake Wanaovaa Suruali nchini Sudan

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Akili Unazo!, Jul 14, 2009.

 1. Akili Unazo!

  Akili Unazo! JF-Expert Member

  #1
  Jul 14, 2009
  Joined: Feb 18, 2009
  Messages: 2,793
  Likes Received: 2,460
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
  Tuesday, July 14, 2009 6:38 AM

  Mwandishi maarufu mwanamke wa Sudan anakabiliwa na bakora 40 baada ya kutuhumiwa kuvaa nguo zilizo nje ya maadili huku wanawake wenzake wengine 10 wameishatandikwa bakora kila mmoja kwa kuvaa suruali kama wanaume

  Lubna Ahmed al-Hussein ambaye huandikia gazeti la mrengo wa kushoto la Al-Sahafa la nchini humo wakati huo huo akifanya kazi pia kwenye kitengo cha habari cha Umoja wa mataifa nchini humo alikamatwa jijini Khartoum wiki iliyopita kwa kuvaa nguo ambazo ni maalumu kwa wanaume.

  Akielezea mkasa wake Lubna alisema kuwa alikuwa kwenye mgahawa julai 3 mwaka huu wakati polisi walipofika na kuamuru wanawake waliokuwa wamevaa suruali wawafuate kituo cha polisi.

  "Walinichukua mimi pamoja na wanawake wengine 12 wakiwemo wasudan wakristo"

  "Siku mbili baadae, wanawake 10 kati yao walitandikwa bakora 10 kila mmoja kwenye kituo cha polisi" alisema Lubna.

  Wanawake watatu waliobakia akiwemo Lubna walifunguliwa mashtaka kwa mujibu wa sheria za Sudan kwa kufanya kitendo kilicho nje ya maadili ya jamii kwa kuvaa nguo zisizofaa.

  Kama wakipatikana na hatia basi wataadhibiwa bakora 40 kila mmoja.

  "Nataka watu wajue nini kimetokea" alisema Lubna.

  Lubna alisema kuwa hajui kesi yake itatajwa lini mahakamani.
   
 2. RealTz77

  RealTz77 JF-Expert Member

  #2
  Jul 14, 2009
  Joined: May 18, 2009
  Messages: 742
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  kwa nchi kama Sudan ni sahihi, avaae kama wao wanavyovaa si yupo kwa wenye tamaduni zao?
   
 3. Akili Unazo!

  Akili Unazo! JF-Expert Member

  #3
  Jul 14, 2009
  Joined: Feb 18, 2009
  Messages: 2,793
  Likes Received: 2,460
  Trophy Points: 280
  Mkuu tamaduni zetu zinaruhusu mwnamke kuvaa suluari au wanalazimisha na uwesternized matters.
   
 4. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #4
  Jul 14, 2009
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Huyu al-Bashir akamatwe na kushtakiwa, haya mambo yataisha menyewe!
   
 5. B

  Babuyao JF-Expert Member

  #5
  Jul 14, 2009
  Joined: Jun 6, 2009
  Messages: 1,734
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  Lakini Sudan ina mchanganyiko wa tamaduni. Kaskazini waarabu ambao wengi wao ni waislamu. Kusini ni weusi ambao wengi wao ni wakristo na watu wanaofuata dini za asili. Kwa hiyo kuwachapa kwa kutumia sharia law sidhani kama ni sahihi katika jamii yenye mseto wa tamaduni na imani tofauti za dini. Wamevunja utamaduni wa nani? Upi ambao ni kipimo cha tamaduni zote za Sudan? Kwa sababu wenngi wa wale waliopigwa viboko si waislamu. Ni wakristo na wale wa dini za asili kutoka kusini ambao hawafungwi na sheria law.
   
 6. Babylon

  Babylon JF-Expert Member

  #6
  Jul 14, 2009
  Joined: Feb 5, 2009
  Messages: 1,338
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Inawezekana sababu kubwa ni joto kwani suruwali za mbano kama hizo zina athari kubwa kwa kina mama in a long run,labda ndio kuwahami wasije wakuathirika kama walivyo athirika wengi katika ulimwengu wa tatu (Usimlaumu Dobi Kaniki ndio Rangi Yake)
   
 7. F

  Froida JF-Expert Member

  #7
  Jul 14, 2009
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 7,900
  Likes Received: 1,328
  Trophy Points: 280
  Lini Dunia hii watakuwa huru mbaya sana wanaume hao ni mama zetu
   
 8. Babylon

  Babylon JF-Expert Member

  #8
  Jul 14, 2009
  Joined: Feb 5, 2009
  Messages: 1,338
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Mbona upo kigeu geu Mkuu kwa yale makubwa aliyowafanyia binadamu wenziwe Rais wa nchi hii anasema asipelekwe mbele ya sheria huku mkimunga mkono, kwa hili la kuvaa nguo ashitakiwe haifai mkuu hisia za kibinafsi ndio zinazoleta maafa katika jamii .yote tisa cha mtu mavi lakini huyo mama amejaliwa shuzi ,wasichana wengi hapa Bongo wanahaha nawao wafufurike kama hivyo.any way she`s looking good from behind.
   
 9. Kituko

  Kituko JF-Expert Member

  #9
  Jul 14, 2009
  Joined: Jan 12, 2009
  Messages: 9,366
  Likes Received: 7,002
  Trophy Points: 280
  nguo za mwanume ni zipi na za mwanamke ni zipi, mimi sijawahi kuona sehemu yoyote inayosema kwamba hizi ni nguo za wanawake na zile za wanaume, kama wanawake wanavaa kanzu na wanaume pia wanavaa na kama wanawake wanavaa vilemba hata wanaume pia wanavaa, sasa iweje wanawake wakivaa suruali inakuwa issue.

  hapa ndio kuna unafiki mkubwa sana kwa waislamu duniani, wanapiga kelele sana kuhusu palestina kuwa wanaonewa na wayahudi na wamarekani, lakini wanavyoonewa wa Sudani ya kusini kulazimishwa kufuata sharia kwao ni sawa tu, na lazima tukumbuke pia kama wayahudi walivyovamia Palestina ni sawa na waarabu walivyovamia SUdani (NUbi), kwa wanaofahamu kiarabu wanaweza nkutupa maana ya neno Sudan.

  Sasa hiyo issue ndio tunaisubiri Tanzania wakti waislamu wengi watakapoikana dini yao katika hizo mahakama ya kadhi
   
 10. K

  Kidatu JF-Expert Member

  #10
  Jul 14, 2009
  Joined: Jun 11, 2008
  Messages: 1,491
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Haya wenzetu waislamu naona sasa mtatuambia na chupi ni vazi la mwanamke/ mwanamume.
   
 11. R

  Rwabugiri JF-Expert Member

  #11
  Jul 14, 2009
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 2,777
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Huu ni uonevu, hivi kungekuwa na winter wangekuwa wanayasema hayo? utavaa sketi utembee juu ya barafu?
   
 12. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #12
  Jul 15, 2009
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,843
  Likes Received: 270
  Trophy Points: 180
  unafiki mtupu huo ni kudhalilisha wanawake tu na wala si eti dini si mtaona hiyo mahakama yenu ya kadhi ikija
   
 13. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #13
  Jul 15, 2009
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Yule Dada wa Kimasri aliye uawa kule Ujerumani kwa kuvaa kwake hijab, hatukusikia ukilalamika!
   
 14. Mateso

  Mateso JF-Expert Member

  #14
  Jul 15, 2009
  Joined: Aug 6, 2008
  Messages: 240
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Hiki kitajatokea kwetu baada ya mahakama ya kadhi kuanzishwa.Wanawake wa kiislamu wajiandae kutokuvaa tena suruali kukwepa hizo bakora.
   
 15. Kiruke cha Ibwe

  Kiruke cha Ibwe Member

  #15
  Jul 15, 2009
  Joined: Jun 26, 2009
  Messages: 69
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 15
  Jamani hii issue ya mavazi sahihi na yasiyo sahihi kweli ni tata! Kwakweli sijui nichukue mrengo gani lakini mi nafikiri mavazi sahihi ni yale ambayo mtu yuko comfortable akivaa.
   
 16. Kyakya

  Kyakya JF-Expert Member

  #16
  Jul 15, 2009
  Joined: Apr 24, 2009
  Messages: 397
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35

  Yule aliuwawa na wahuni tu. Lakini hii ni issue ya nchi nzima
   
 17. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #17
  Jul 15, 2009
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  ndugu zangu msikurupe kuanza kulaumu uislam. Hebu someni vizuri hiyo mada especially hapo nilipoweka wekundu.

  Wao watamuhukumu kwa mujibu wa sheria zao na wala sio sheria za kiislamu.

  Acheni kuchukia uislam bila kuwa na hoja makini
   
 18. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #18
  Jul 15, 2009
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  mbona kenya na uganda zipo mahakama za kadhi lakini hao hayajatokea?.

  Mbona zanzibar ipo mahakama ya kadhi mbona hayo hayajatokea?

  Tuacheni kasumba za kikoloni za kuendekeza udini. Kumbuka kasumba hizo zililetwa na waingereza. Wao walitumia divide and rule system katika kuitawala east africa. Kule kenya na uganda ambako kulikuwa na makabila machache walitumia ukabila kuwagawa na kuwatawala.

  Tanganyika kulikuwa na makabila mengi sana alitumia udini kututawala.

  Sasa wengi wameathiliwa na hizo ni athari za utawala wa kiingereza ndani ya tanzania, kenye na uganda.

  kenya- ukabila, uganda - ukabila, tanganyika - udini
   
 19. N

  Ndivyo Ilivyo JF-Expert Member

  #19
  Jul 15, 2009
  Joined: Mar 10, 2008
  Messages: 243
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Nyinyi watu mna matatizo kweli! Msiunganishe masuala ya Utamaduni (Mila) na masuala ya dini. Nenda katika dini -inasema mtu avae nguo inayositiri mwili-Jee suruali haisitiri? haijafunika sehemu zinazotakiwa kufunikwa? Sasa ugomvi uko wapi? Hayo ya Sudan ni ya Utamaduni wao. lakini hata US kule wako waislamu na wanavaa tu suruali.
   
 20. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #20
  Jul 15, 2009
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,316
  Likes Received: 1,785
  Trophy Points: 280
  Huko ni kudhalilishana kusiko na mpango.
   
Loading...