BAKITA, Kwanini wasiitwe Zeruzeru?

MZIMU

JF-Expert Member
Apr 29, 2011
4,057
1,371
Nimekua nikisumbuliwa sana na hili jina Albino wakati tangu nazaliwa karibia nusu karne sasa, Neno sahihi la kiswahili ni Zeruzeru. Sijaona ubaya wa neno hilo jamani. Albino sio neno la kiswahili, ni neno la kingereza.

Swali langu, ni kwanini BAKITA = BARAZA LA KISWAHILI TANZANIA, Wamekaa kimya tu kwa upotoshaji huu mkubwa sana.
 
Moderator Kero hii nimeiweka jukwaa hili ili kila mtu aione.

Nimekua nikisumbuliwa sana na hili jina Albino wakati tangu nazaliwa karibia nusu karne sasa, Neno sahihi la kiswahili ni Zeruzeru. Sijaona ubaya wa neno hilo jamani. Albino sio neno la kiswahili, ni neno la kingereza.

Swali langu, ni kwanini BAKITA = BARAZA LA KISWAHILI TANZANIA, Wamekaa kimya tu kwa upotoshaji huu mkubwa sana.

Mkuu hata mimi nakubaliana na mawazo yako. Neno zeruzeru sio matusi wala sio la kebehi.
 
Absolute vyombo vya habr navyo vinachangia kutuharibia kiswahl,pia soon utashangaa kipofu watamuita blind
 
Tatizo hapo ni kwamba hawa ndugu zetu hawapendi na hawataki kuitwa zeruzeru...

Kwao kuitwa zeruzeru ni kuwanyanyapaa...hivyo kutokana na ulemavu wao huo imeonekana ni busara kuwaita kwa jina wanalolitaka "albino"

Kwa maana nyingine, tatizo hapo ni utumwa fikra....kwao kuitwa albino ni rahisi kutambuliwa na jumuiya za kimataifa na pengine wanadhani kwa kutumia jina hilo itakuwa rahisi kupata huruma na misaada toka nje....

Hayo ni mawazo yangu baada ya nami kujiuliza kwa muda mrefu na pia baada ya kumuuliza rafiki yangu mmoja ambaye ni albino kwa nini nisikuite zeruzeru...alikasirika sana na karibu tuvunje urafiki.

Tafakari
 
Kiwete, kipofu, Zeruzeru, Kiziwi, Bubu,Kichaa, Mguu Mbovu, Mkono Mbovu n.k. Haya yote ni Maneno halali kabisa ya kiswahili, chakushangaza sasa hivi kumezuka mtindo wa watu wenye aina hizo za ulemavu kuyakataa majina hayo na kujipachika majina ya kiingereza eti, Albino, na wengine eti wanazunguka Mbuyu eti, Mlemavu wa Mguu badala ya Kiwete n.k

Huu ni ujuha si vinginevyo. Mwishowe hata watoto watakataa kuitwa watoto, wadai haki zao na wao waitwe Children.
 
Kilicho wajaa watanzania ni ukasumb wa kujifanya wanafanya utozishaji wa lugha nyingine katika lugha yetu.
 
Kumbe wengi huwa mnakereka kama mie, eti wanaita mlemavu wa ngozi, sasa sijui nikiwa nina tatizo la ngozi la kuzaliwa nalo inakuaje. Wanaharakati ndio wanaharibu mambo yote kwa kuwa lile ndio jina sahihi kabisa kama linavyotamkwa kwa kithungu Albino na kiswahili ni zeruzeru. Kikubwa kama binadamu tunatakiwa tumtambue kwa jina lake ila tunapowaelezea kama kundi maalumu kutokana na tatizo lao inabidi tuseme zeruzeru au kiwete (kinachofanyika ni kusema tafsiri ya maneno yale yale ambayo wanayakwepa na ndio maana Nyerere aliwahi kusema ukitukanwa kwa kiswahili unakasirika lakini tusi lilelile likitolewa kwa lugha ya wenzetu huonyeshi kukasirika japo umelielewa)
 
Kwakweli hili ni tatizo, Hawa wanaharakati wanapotosha jamii na cha ajabu vyombo vya habari navyo vipo kimya na hushabikia upotoshwaji huo. Isije ikafika mahala, mtu kuitwa mwanamume pia ni kosa. Ikabidi aitwe Man. Na mwanamke aitwe Woman. Maana kumuita Mwanamke itakua umemdhalilisha.
 
Kutawaliwa ni kubaya sana. Na naona tunazidi kuzama kwenye fikra za kitumwa kadiri hiki kinachoitwa maendeleo kinavyokuja. Hunifurahisha sana ustaadh Andanenga yeye husema yeye ni kipofu na watu waache kuzunguka mbuyu na kutoa tafsiri ya ulemavu wake et i" mwenye ulemavu wa macho" au "asiyeona"
 
Zeruzeru ni tafsiri ya Kiswahili ya albino. Tatizo ni kwamba neno hili linaonekana halijakaa sawa (politically incorrect) na linaonekana kuwakebehi watu wenye aina hii ya ulemavu wa ngozi, lakini huu ni ujinga uliokithiri ambao unadidimiza Kiswahili. Pia vipofu inasemekana wamekataa kuuitwa hivyo na wanataka waitwe wasioona. Viziwi walikataa mapema kuitwa wasiosikia kwa sababu neno hili lina maana nyingine ambayo si nzuri sana.
 
Mimi naona ALBINO ndio kama halijakaa sawa. Ndio hayo ya SLAVERY MENTALITY.
 
HAya bwana mambo yataenda hivi;

 • watoto-watu wenye umri pungufu
 • wazee-wenye umri uliopea
 • watu wazima-umri wa kati
 • vilema-majeruhi wa kudumu
 • wanawake-wazalisha "watoto"
 • Wanaume -wasababishi "watoto"
 • na upuuzi mwingineo.!
 
HAya bwana mambo yataenda hivi;

 • watoto-watu wenye umri pungufu
 • wazee-wenye umri uliopea
 • watu wazima-umri wa kati
 • vilema-majeruhi wa kudumu
 • wanawake-wazalisha "watoto"
 • Wanaume -wasababishi "watoto"
 • na upuuzi mwingineo.!

Umenena vema. Na hiyo ndio maana yake. Maana Nchi hii imekua na mambo ya ajabu ajabu sana.
 
Kama neno kiwete nalo siku hiz linazunguushwa mpaka basi dah bakita wanzingua hawana msimamo
 
Kama neno kiwete nalo siku hiz linazunguushwa mpaka basi dah bakita wanzingua hawana msimamo

Jana nimesikia itv viziwi wanawaita walemavu wa masikio

Inasikitisha sana. Hakika ni upotoshwaji mkubwa. Hawa watu waelemishwe na hilo ni jukumu la BAKITA na serekali, Sio kubadilisha maneno sahihi ya kiswahili, kwani dunia nzima watu hao wapo na wanatambuliwa kwa lugha za nchi zao na sio kutumia lugha za kigeni.
 
Back
Top Bottom