Bakhresa achangia bajeti $800k

Bakhresa achangia bajeti $800k

Inawezekana kabisa,keshapewa tenda ya kuendesha mradi wa treni,hapa jijini Dar.

Kwa kuwa nakumbuka jana,waziri wa uchukuzi, Dr Mwakyembe,alitangaza kwenye bajeti yake kuwa,serikali ina mpango WA kubinafsisha,mradi wa treni,jijini Dar.

Kwa mtindo wa serikali hii,ingawa waziri Mwakyembe,ametuambia kuwa kampuni 14,zimebid tenda hiyo,upo uwezekano mkubwa kuwa Bakhresa,keshajibiwa na kuambiwa keshapewa tenda hiyo,hata kabla kikao cha tender board hakijakaa!!

kama anaweza hakuna ubaya
 
Hamna jema, jee we mjomba yako amechangia shs ngapi? Acheni majungu? Any way wee umechangia shs ngapi kijini kwenu?
 
Hongera kwa uzalendo wako ndugu Bakhresa,endelea na moyo huo huo na mwenyezi Mungu akuzidishie.
 
Ni kampuni ya SSB imechangia wizara ya uchukuzi USD800,000 ili mabehewa ya treni yatengenezwe.

Anastahili pongezi.

Source: TBC jana.

==================
Ufafanuzi zaidi
==================
Kaona wahusika na reli hamnazo inabidi aokoe jahazi. Miaka yote kujenga mabarabara tuuu reli hamna kitu; hivi hayo matrilioni ya bajeti ya miundombinu yangeingizwa kwenye reli mwaka huu tupumzike kutafuna kupitia mabarabara badala yake tununue vichwa vya treni na mabehewa tungepata vingapi? si tungemaliza tatizo milele na ajira kibao kupatikana lakini wapi mapesa yanapenyezwa tu kwenye mawizara yenye urahisi wa kuyatafuna na ajira ni kwa vibosile
 
Hata madonors wanaotoa misaada huwa wanasema misaada yao ifocus wapi kwa hiyo sio kitu cha ajabu,tumshukuru tu manake keshatupiga bao

Huyu jamaa atakua mgeni katika mambo hayo, hajui kua hata WB/IMF/ADB kabla ya kutoa msaada wanaambiwa lengo la msaada husika.
 
Ikitokea kakwepa kodi mbele ya safari, hivi mtamkamata huyu?
Ni kweli shirika la reli halina fedha kama hizo kwa ajili ya kukarabati vyombo vyake?
Tukisema Serikali inajitia yenyewe mfukoni kwa Bakresa tutakuwa tunakosea?
 
wampe nchi tuu aindeshe kibiashara serikali ya ccm imeshashindwa kuiendesha hii nchi
 
KWA MARA YA KWANZA KATIKA HISTORIA YA TANZANIA!
Na huenda ni kwa mara ya mwisho...!

HAINISHANGAZI Taarifa hii, PELELEZA UMILIKI WA JENGO/KIWANJA Kilochopo pale TAZARA ambayo sasa hivi ndio kiwanda cha BAKHRESA kilihamaje toka serikalini mpaka kwake????????????????????????????????
 
Anatafuta misamaha ya kodi huyu maana ni nadra kwa mtu kufanya hivo bure
badala ya kusaidia yatima na wasiojiweza anazidi kuwaongezea mafisadi wa ccm ulaji. huu jamaa nahsi hata product zake zitakua ccm ccm
 
nikijaribu kulinganisha na "The great bagamoyo project" wangemega dola bilioni 1 tu zingeweza kununua vichwa 2500 maana dola laki8 vichwa viwili, milioni moja 2.5 zidisha mara 1000, sasa vipaumbele vyetu viko wapi? mbona tunafukuza upepo? si tungesubiri basi huo mradi wa bagamoyo na hiyo reli ya bagamoyo? kweli CCM HAINA DIRA WALA MWELEKEO, mimi sina chama lakini hawa jamaa mambo wanayofanya yanatia kichefuchefu sana, swali kwa zemarcopolo hivi CCM hakuna mwenye akili?
 
Kwa kweli Bakhresa kafanya jambo la maana, lakini kwa serikali yetu hii sikivu, pesa zitaishia kwenye matumbo ya watu. nashauri bora angenunua treni zake mpya kabisa akazileta zifanye biashara.
 
Kama hamna namna nyingine basi tumshukuru

Huyu ana lake jambo, si bure. Hakuna kitu cha bure wakati wowote. Anaandaa ujio wa masultani toka Oman ambao tuliwavurusha huko Zanzibar 1964.

SSB anatumia mlango wa nyuma kutawala nchi.Tusione ajabu ikulu siku moja kuwa chini ya rais mwarabu (kama ilivyo kule Loliondo). Naitahadharisha serikali isiruhusu watu kuingia kwa mlango wa nyuma, wasijue kuwa siku moja watatokea mlango wa mbele, hapo tutakuwa tumechelewa na tutakosa mtu wa kumlaumu.Naishauri serikali ifunge gavana kwa kutoruhusu ilani za CCM ambazo zimefunga mikataba ya hovyo hovyo. Hatimaye tutatokaje humo?

NAWASILISHA.
 
Bora apewe tu, sisi tunahitaji huduma nzuri

wa tanzania tufunguke macho huyu jamaa halipi kodi ya mapato anaebisha akagoogle "top ten tax payeer campany in tanzania" ukipata majibu ya hapo changieni mada vizuri
 
Back
Top Bottom