Bajeti yetu iko tayari, kwanini tuwasubiri Kenya na Uganda tusome pamoja tarehe 11 Juni? Wabunge watalipwa posho bila kufanya kazi?

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,978
141,995
Jana Spika Ndugai amesema pamoja na kwamba bajeti yetu imewahi kukamilika bado itatulazimu kuwasubiri " Wenzetu" wa Kenya, Rwanda na Uganda ili tuzisome kwa pamoja tarehe 11 June.

Maana yake ni kwamba wabunge wataendelea kuwepo Dodoma wakiisubiri hiyo tarehe ya " pamoja " kisha wataendelea kuwepo wakisubiri tarehe ya kuvunja bunge ambayo ni 19 June.

Hii imekaaje wakuu....kuna ulazima wa kusubiriana nyakati kama hizi?

Maendeleo hayana vyama!
 
INAWEZEKANA NDIZO TARATIBU WALIZOJIWEKEA ILA NAHISI TAMKO LAWEZA TOKA CHATO MUDA WOWOTE
 
Napendekeza waende karantine siku 14 ili wajicheki afya zao kwa muda huu wa kusubiria ili kama wana maambukizi ama lah

Pia muda huo wote napendekeza POSHO zao zitumike kununua vifaa kinga na Tiba kwa ndugu zetu watabibu na wagonjwa wa Corona.
 
Bwashee shida ya nyie vijana was CCM hamsomi.Kazi yenu kuungajuhudi tu. In hivi, kwa mujibu was Mkataba wa Ushirikiano wa Jumuia ya Afrika Mashariki, hizi nchi zinashirikiana katika masuala kadhaa ya ya kodi, hususan lile la Common External Tariffs (CET) ambayo ni kodi inayotozwa kwa bidhaa zote zinazoagizwa kutoka nje. No lazima kodi hizi zifanane kwa nchi zote. Makubaliano ya vuwango vya CET huwa yanafikiwa kutokana na vikao vya mawaziri wa fedha vinavyofanyika wiki kadhaa kabla ya bajeti. Maana yake ni kwamba lazima bajeti zisomwe siku moja. Ikiwa zitasomwa siku tofauti, wafanyabiashara wa nchi ambayo itachelewa kusoma bajeti yake watapata faida. Nadhani sasa umeelewa bwashee!
 
johnthebaptist, sikujua wewe uko dhaifu kiasi hiki!!!!!!!
 
Hao mawaziri wa fedha watakutania wapi na lini?

Au ni video conference?
 
Hahahaaaa....... Nazungumzia nyakati hizi bwashee!

Nyakati za Corona.
Hata kama-ndiyo utaratibu tuliojiwekea na inafanyika hivyo miaka yote. Hivi hata kama ni corona wachumbe wanataka kufunga ndoa wanaenda kila mtu kwa wkati wake na tunaita hiyo ndoa?
 

ingekuwa mawazo ya upinzani yanakubalika yaingie, ili walete mawazo mapya, ingekuwa kuikosoa bajet iliyoletwa na serikali ni moja na uzalendo, basi hadi leo kungekuwa na mtanange bungeni..

Sijui hofu yako ni nini, wakt bajeti imepita bila kupingwa huku unaijua kabla haijapelekwa bungeni.
 
Hata kama-ndiyo utaratibu tuliojiwekea na inafanyika hivyo miaka yote. Hivi hata kama ni corona wachumbe wanataka kufunga ndoa wanaenda kila mtu kwa wkati wake na tunaita hiyo ndoa?
Mbona ratiba ya awali ilionyesha bunge kufungwa 31 May?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…