Bajeti ya kuwamaliza wasilokuwanacho | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Bajeti ya kuwamaliza wasilokuwanacho

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Nelembe, Jun 18, 2012.

 1. N

  Nelembe Member

  #1
  Jun 18, 2012
  Joined: Jun 18, 2012
  Messages: 7
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wana JF; Hebu fikirieni; Bajeti iliyosomwa imepandisha Gharama za Mawasiliano ikiwa ni pamoja na Simu za Mkononi za Mchina ambazo Mlalahoi amenunua kwa kubangaiza elfu mojamoja zikafika 25,000/= akanunua ili imusaidie kusaka Tonge. Bajeti imeongeza PAYE kwa wafanyakazi ambao kila wakilia na kuomba nyongeza ya Mishahara inapanda kwa kuongezwa Shilingi Elfu kumi tu. Mafuta ya taa ambayo kule vijijini ndiyo umeme unaowasaidia Babu/Bibi zetu wasing'atwe na Ng'e bei haikamatiki kwa kuwa eti Watawala wa Nchi hii wanahofia kwamba Wafanyabiashara watachakachua Petrol na Diesel kwa kuongeza Mafuta ya taa! Mfanya Biashara anayeuza hadi Millioni tatu (3,000,000/=) kwa siku moja hadaiwi kodi. Mshahara wa Mfanyakazi anayepata Shilingi Millioni Mbili tu (2,000,000/=) kwa Mwezi PAYE anayotozwa kwa kila mwezi ni zaidi ya laki Sita (600,000/=). Wanaochota Madini kule kwenye Migoti na kurusha kwenye Ndege zao kwenda kwa Wazungu Bajeti imewaacha wapumuzike! Je hivi siyo kweli kwamba waandaaji wa Bajeti hii wanafikiria kwa kutumia Makalio?
   
Loading...