Bajeti ya gari za mkononi

KndNo1

JF-Expert Member
Oct 26, 2021
627
2,023
Gari za kununua mikononi kulingana na bajeti yako na kupata best bang kwa hela yako..!

2-5M
Corolla/Sprinter
.. Gari simple na ngumu..
GX 100..ukipata yenye 1G Matumizi ya mafuta yatakuwa juu kidogo.. Ila hautakuwa mnyonge barabarani..!
Vits.. Ukipata ya 3 doors hapa ujiandae kukunja siti ili watu kupita nyuma..!

5-15M
IST
.. Hii sifa zake zinafahamika..!bei imechangamka..!
Premio..imebalance matumizi ya mafuta, Performance na Comfortabilty..
Suzuki Escudo 1st Gen.. Hii inakubali mateso.. Unaweza bebea hata majani ya ng'ombe..
Rav4 1st Gen.. Hii kitu aisee ni hatari..ipo comfortable zaidi ya Escudo na performance yake ipo vizuri.. Ngumu sana kukwama.. Matairi yote inapush..!
Subaru Forester 1st & 2nd Gen.. Huyu naye hatari zaidi..hiyo Symmetrical All Wheel Drive ni hatari mno..tafuta yenye engine ya Ej20 kavu..!

15-30M
Prado 90 series
aka Mchaga..pata diesel engine KZ au KD japo bei ipo juu..
Prado 70 series aka Landcruiser ii.. Gari ina shape nzuri ya box.. Mbele ina diff.. Jitahidi upate yenye 1KZ.. Sababu ya 2L au 3L ni underpowered kulinganisha na gari..!

Usinunue gari za watu watano kama Harrier au Rav4 kwa bei unayoweza pata kitu ngangari zaidi..!

30-55M
Prado 120 series
.. Kama kawaida tafuta diesel..!upate yenye tank capacity 180lts..!
Landcruiser 100 Series.. Ukipata ya 1HDFTE.. Kama auto iwe Zigzag.. Manual nzuri zaidi..!
 
Nina million 5 nahitaji gari kupanda milima na mabonde, kupita kwenye lami na rough road bila shida
 
Back
Top Bottom