Bajeti ya elimu 2012/13 itamaliza changamoto hizi? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Bajeti ya elimu 2012/13 itamaliza changamoto hizi?

Discussion in 'Jamii Photos' started by MziziMkavu, Aug 13, 2012.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Aug 13, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,613
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
  Habari Mwanalibeneke wa Mtaa kwa Mtaa,


  Naomba kushea na Wadau hoja hii kwa Wizara ya Elimu.


  BAJETI ya elimu itasomwa bungeni siku ya Jumatatu, 13 Agosti. Wakati bajeti ya Elimu inasubiriwa kwa hamu na wadau na hasa wapenda maendeleo ya Elimu, Baadhi ya maeneo nchini bado yanakabiliwa na changamoto kubwa sana hasa hali mbaya ya miundombinu, ukosefu wa vyumba vya madarasa na majengo ya shule ambayo yamesababisha baadhi ya shule kuweka madarasa ya nyasi kama shule ya msingi Selous na Mkapa zilizopo wilayani Namtumbo, Shule ya msingi Silabu iliyoko wilayani Korogwe, Shule ya msingi Misunkumilo ya wilayani Nkasi, na baadhi ya shule wilayani Muleba.


  Hali ya elimu imezidi kuwa mbaya kila kukicha, kiasi kwamba hata watu hudiriki kuuliza kama shule hizo zipo nchini, hasa wakiangalia juhudi na kelele nyingi zilizopigwa juu ya mchango mkubwa wa MMEM na MMES kuwa zimefanya kazi kubwa sana kuboresha mazingira ya kujifunzia hasa miundombinu ya shule. Swali Je, shule hizi ziliachwa wapi na mipango hii? Je bajeti ya elimu ya 2012/2013 itatatua baadhi ya changamoto za elimu nchini?na kuondokana na majengo haya yasiyo rafiki kwa mwanafunzi na mwalimu?


  Mwana blog, Hebu angalia jinsi ambavyo wanafunzi huko Tanga, Rukwa, Kagera na Ruvuma wanavyojifunza kwenyesehemu zinazokatisha tamaa: Watatoka?
  [​IMG]
  [​IMG]
  [​IMG]
  [​IMG]
  [​IMG]
  [​IMG]
  [​IMG]
  [​IMG]

  Bajeti ya elimu 2012/13 itamaliza changamoto hizi? ~ MTAA KWA MTAA
   

  Attached Files:

  • 1 (3).jpg
   1 (3).jpg
   File size:
   100.1 KB
   Views:
   42
  • 2.JPG
   2.JPG
   File size:
   97.2 KB
   Views:
   32
  • 3.JPG
   3.JPG
   File size:
   82.9 KB
   Views:
   25
  • 4.JPG
   4.JPG
   File size:
   132.2 KB
   Views:
   16
  • 5.JPG
   5.JPG
   File size:
   98.4 KB
   Views:
   24
  • 6.JPG
   6.JPG
   File size:
   109.1 KB
   Views:
   19
  • 7.JPG
   7.JPG
   File size:
   138 KB
   Views:
   23
  • 8.JPG
   8.JPG
   File size:
   86.3 KB
   Views:
   23
  • 9.jpg
   9.jpg
   File size:
   128.4 KB
   Views:
   30
 2. MadameX

  MadameX JF-Expert Member

  #2
  Aug 13, 2012
  Joined: Dec 27, 2009
  Messages: 7,847
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  Tutafika hata kwa kutambaa
   
 3. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #3
  Aug 13, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Mambo madogo hayo. Nyerere miaka 24 hakuyamaliza, na Mwinyi na Mkapa waliyakuta na wameondoka hawakuyamaliza.

  Nna uhakika muarubaini wa hayo ni Kikwete na kwa uwezo wa Allah atayamaliza, kwani shule zilizopo kwa WINGI wakati wake na idadi kubwa ya wanafunzi kuanzia primary, secondary, vyuo vikuu na vyuo vya ufundi hazijawahi kutokea kwa kwa yeyote wa kabla yake na alianza kwa kujenga sasa anaziboresha na kunapoongezeka idadi ya watoto mpaka wanakosa shule patajengwa zingine.

  Kikwete anastahili sifa kwa kuwezesha idadi kubwa sana ya wanafunzi kuongezeka katika shule na vyuo vyote.

  Inabidi na wananchi tutoe ushirikiano wa kuziboresha shule na masomo kwa kujitolea japo masaa machache kwa mwezi kuzitembelea na kujuwa vipi matatizo yao tunayoweza kuyatatua bila kungoja bajeti za serikali. Maharusi na vifo wa kwanza kuchangishana. Ikija michango ya maendeleo kama hii ya kuboresha shule kila mmoja anaingia mitini.

  Na Watanzania nae muache kuzaana sana, mtakosa huduma muhimu kwa wakati.
   
 4. m

  mabwepand Member

  #4
  Aug 13, 2012
  Joined: Jul 16, 2012
  Messages: 84
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 15
  mkuu nimekusoma ila sijakupata vizuri huwezi niambie kipindi cha awamu ya kwanza na ya nne zinafanana kabisa ni ngumu tena kipindi hiki mm naamini ni mbaya tena mbaya kabisa elimu yetu mkuu wangu,mathalani mtu unaaza darasa la kwanza na unamaliza hadi chuo ujatoka nje ya tarafa yako unategemea nn kama tarafa yenu wote ni wajinga utakuwa mjinga tu,na kule ambapo wana fursa nzuri lazima watakuacha,kiakili,kimaisha.Huwezi compare uwezo wa mwalimu wa Dar,Arusha kiufundishaji na yule mwalimu wa Tandahimba,Nachingwea ambapo hakuna darasa wala Choo ufundishaji wake utakuwa tofauti kabisa na walimu wa mjini japokuwa wamesoma chuo kimoja wamekata tamaa.
   
 5. Philipo Kidwanga

  Philipo Kidwanga Verified User

  #5
  Aug 13, 2012
  Joined: Jul 12, 2012
  Messages: 2,063
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  huo muongezeko wa wanafunzi wanaokwenda sekondari halafu hawajui hata kuandika majina yao kwa kweli kikwete ameweza.
   
 6. Ngangasyonga

  Ngangasyonga JF-Expert Member

  #6
  Aug 13, 2012
  Joined: Sep 13, 2010
  Messages: 456
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  We need strong changes!!
   
 7. Z

  ZeMarcopolo JF-Expert Member

  #7
  Aug 14, 2012
  Joined: May 11, 2008
  Messages: 13,589
  Likes Received: 480
  Trophy Points: 180
  Ushahidi wa kushuka kwa elimu huu hapa...
  elimu imeshuka....JPG
   
 8. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #8
  Aug 14, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,613
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
   
 9. Gwangambo

  Gwangambo JF-Expert Member

  #9
  Aug 14, 2012
  Joined: Jun 30, 2012
  Messages: 3,655
  Likes Received: 85
  Trophy Points: 145
  Zomba unapenda kutia watu hasira, nimechoshwa na ban.
   
 10. Philipo Kidwanga

  Philipo Kidwanga Verified User

  #10
  Aug 14, 2012
  Joined: Jul 12, 2012
  Messages: 2,063
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  nahisi kuna wakati akili za baadhi ya wenzetu huenda matembezini.
   
Loading...