Bajeti ya chaguzi ndogo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Bajeti ya chaguzi ndogo

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by kalou, Oct 4, 2011.

 1. kalou

  kalou JF-Expert Member

  #1
  Oct 4, 2011
  Joined: Aug 22, 2009
  Messages: 4,364
  Likes Received: 986
  Trophy Points: 280
  Baada ya kampeni kubwa sana zilizofanyika igunga mimi nimebaki na swali moja la msingi, hivi kama kila miezi mitatu kuwe na uchaguzi wa mbunge mmoja kwa sababu mbunge awe amefariki au amevua gamba, shughuli za maendeleo zitafanyika kweli?

  Tumeona mawaziri,wabunge wa vyama mbali na hata watumishi wa serikali kuacha majukumu yao ya kila siku na kutumia muda wao wote kwenye kampeni.

  Mimi nafikiri kuwepo na sheria za kusimamia chaguzi ndogo kama hizi,ku limit viongozi wa kichama wanaoweza kushiriki ili kuruhusu shughuli nyingine za kimaendeleo ziendelee.

  Pia budget za kampeni ziwe na kikomo,...kumbuka hao wananchi wanaofanyiwa mbwembwe kwenye kampeni ni masikini,wanachohitaji na kiongozi safi na si mengineyo..
   
 2. Ibrah

  Ibrah JF-Expert Member

  #2
  Oct 4, 2011
  Joined: Mar 22, 2007
  Messages: 2,721
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 145
  unajihangaisha bure. sheria zipo tena very clear na wasimamizi pia wapo, lakini nani amfunge paka kengele?

  Labda useme SASA TUNAHITAJI KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI KWENYE CHAGUZI.
   
 3. Kigarama

  Kigarama JF-Expert Member

  #3
  Dec 21, 2011
  Joined: Apr 23, 2007
  Messages: 2,479
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Kwa sababu haiwezekani kwa sasa kubadili sheria inayovipa vyama udhibiti wa wanachama wao wanaochaguliwa kushika nyiadhifa za Udiwani na Ubunge, ni lazima ili kuliokoa taifa taifa letu tutunge sheria ambayo itavilazimisha vyama vikifanya maamuzi ya ovyo dhidi ya wanachama wake na kusababisha kufanyika kwa chaguzi ndogo, chama husika kibebe gharama za uchaguzi husika.

  Wengi wetu tunaweza kuwa hatujui kama sheria ya kumvua uanachama mbunge au diwani haihusiki kwa nafasi ya Rais. Rais hata chama chake kikimvua uanachama yeye ataendelea kuwa Rais. Sheria hiyo itapunguza maamuzi ya pupa, kukomoana na kutishana yaliyokithiri ndani ya vyama vyetu vya siasa.

  Kama Tendwa alichokisema ni cha kweli basi uchaguzi mdogo mmoja unagharimu mpaka shilingi Bilioni 19. Hizi fedha nyingi sana kuendesha uchaguzi ambao mwisho wa siku kunatokea uchakachuaji. Hizo fedha fedha zinatosha kabisa kujenga barabara ya lami kwa viwango vya kimataifa yenye urefu wa Kilomita 20.
   
 4. M

  Marytina JF-Expert Member

  #4
  Dec 21, 2011
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 7,037
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 145
  acha uzuzu hela ya CCM ,NCCR,CDM ni za umma
  itumike hela ya nccr bado ni umma
  tendwa alitakiwa asema katiba yetu ni mbovu
   
 5. Kigarama

  Kigarama JF-Expert Member

  #5
  Dec 21, 2011
  Joined: Apr 23, 2007
  Messages: 2,479
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Samahani nimeihariri kidogo niweze kuijibu!!

  Kwanza elewa hata fedha za mishahara ya wale wanaolewa pombe na kumalizia mishahara yao bar ni za umma, lakini mtu akishalipwa mshahara wake huwezi kumpangia jinsi ya kuutumia hata kama mshahara huo unatokana na fedha za UMMA. Zuzu ni yule anayeshindwa kutofautisha Nyakati na Mahali.

  Kama fedha za vyama ni za Umma hebu fikiria Serikali inatumia Bilioni 19 kwa chaguzi ndogo vyama vya siasa vinatumia bilioni 6 ni nini tofauti. Kama vyama vitazuiwa kutuingiza kwenye chaguzi za kijinga kama ule wa igunga ambao mtu mmoja kwa maslahi yake binafsi akaliingiza taifa zima kwenye gharama ambazo hazina msingi kabisa.

  Wakati serikali inaomba fedha za kujengea vyoo kwenye shule wanazosoma watoto wetu kwa kisingizio kwamba haina fedha, serikali hiyo hiyo inatumia mabilioni ya fedha kwenye chaguzi ambazo mwisho wa siku haziongezi chochote cha maana zaidi ya kuongeza wadai posho bungeni
   
 6. Jumakidogo

  Jumakidogo R I P

  #6
  Mar 3, 2012
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 1,859
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Chaguzi ndogo hugharimu pesa nyingi sana kwani kila chama hutaka kuonesha makucha yake kuwa kinakubalika na wananchi kuliko kingine, hapo ndipo ubabe wa kutangaziana nani mwenye pesa zaidi huanza. Badala ya kutumia gharama kubwa kwa ajili ya chaguzi ndogo ni bora majimbo yangekuwa yanakaa wazi mpaka uchaguzi mkuu na nafasi ya ubunge kukaimiwa na baraza la madiwani. Ukijumlisha pesa inayotumika katika kampeni na gharama inazotumia serikali katika kuandaa uchaguzi, utaona kuwa inatosha kabisa kuandaa bajeti ya kusukuma maendeleo katika jimbo. Lakini kinachotokea ndiyo hicho. Fedha nyingi kupotea, muda, vurugu za hapa na pale. Mwisho anayechaguliwa akiingia bungeni kitu cha kwanza ni kuuchapa usingizi ukumbini.
   
 7. Nzowa Godat

  Nzowa Godat JF-Expert Member

  #7
  Mar 3, 2012
  Joined: Jun 15, 2011
  Messages: 2,630
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 160
  Wanasiasa wangekuwa na mawazo safi kama ya kwako nji hii ingepiga hatua kwenda mbele.
   
 8. m

  mageuzi1992 JF-Expert Member

  #8
  Apr 5, 2012
  Joined: Apr 9, 2010
  Messages: 2,512
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Mipango siku zote ni kitu cha muhimi. Swala la bajeti ni swala nyeti na muhimu kila mwaka tunakuwa na bunge la bajeti kwa ajili ya mwaka wa fedha unaofuata. Katika bajeti kila wizara hutangaza bajeti yake na vipaumbele vyake. Wizara ya sheria na katiba nayo hufanya hivyo hivyo. Mathalani swala la uchaguzi mkuu. Nimeamua nitangulize muongozo huo ili nilete swali langu sasa. Tumeshuhudia chaguzi ndogo nyingi zikitokea je wahusika wa wizara husika hulitambua hili
   
 9. Jackbauer

  Jackbauer JF-Expert Member

  #9
  Apr 5, 2012
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 5,920
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  yapata mwezi mmoja na siku chache tangu tumalize misukosuko ya mgomo wa madaktari juu ya maslahi yao na ya wagonjwa.

  Moja ya sababu za serikali kushindwa kutoa maslahi bora kwa madaktari ni ukosefu wa fedha au tuseme fedha haikutengwa kwenye bajeti inayoendelea ili kukidhi madai ya madaktari.
  Sababu hii(uwezo mdogo wa serikali kifedha) pia imetajwa kuwa ni chanzo cha huduma mbovu mashuleni na mahospitali ya serikali....LAKINI......

  Kamwe hatujawahi kusikia kuna ukosefu wa fedha katika kufanya chaguzi ndogo.

  Je tumetenga kiasi gani katika kuendesha chaguzi ndogo?
  Leo hii kila mgombea aliyeshindwa akiamua kupinga matokeo itakuaje?

  Tuhurumieni walipa kodi!
   
 10. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #10
  Apr 5, 2012
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Mkuu huo ni uthibitisho tosha kwamba nchi inaendeshwa kiholela, na ndio maana hata ile loooooooong session ya bunge kujadili bajeti inaweza kuwa ni utaratibu tu!!!!!!!!!!! Mazoea at it's best.
   
Loading...