Hivi Tanzania haiwezi KABISA kuandaa bajeti na kuendesha nchi bila kutegemea VILEVI (POMBE) na SIGARA????? NI AIBU SANA MAANA TUNA MALIASILI NYINGI SANA ZINAZOTOSHA KUENDESHA NCHI BILA YA KUHITAJI VILEVI. Kazi tunayojua ni kuuza wanyama/madini kwa kutegemea mrahaba wa 3% na ufisadi tu. Ni aibu
Kuna mtaalamu mmoja aliwahi kuishauri serikali baada ya kufanya feasibility Study. Madini ambayo yameshagunduliwa na kuchimbwa nchi hii yanaweza kuiendesha nchi hii bila kutegemea misaada na kuifanya iwe kama S. Africa baada ya miaka 20.
Nacho ni kitu kidogo ni serikali kuwa na hisa katika migodi YOTE ya madini SERIKALI 41% na WAWEKEZAJI 59%. Ndivyo S. Africa walivyofanya na ndivyo Botswana wanafanya. Pamoja na hizo hisa, serikali itaendelea pia kutoza kodi kwenye migodi hiyo madini, kama inavyofanya sasa.
Lakini kwa mtindo huu wa kutegemea mrahaba wa 4% na KODI TU, tena kodi nyingine zinapewa misamaha na nyingine kodi zinakwepwa kwa declare mapato pungufu, hata ardhi yote ya Tanzania iwe dhahabu hakuna amendeleo yeyote ya maana tutakayopiga kulingana na utajiri.
Hao wanaojiita First Class Economist akina Mwigulu Nchemba wamesoma nini? Huu ukweli dhahiri shairi, kwanini hawauoni?. Uchumi gani wamesoma hawa akina Mwigulu Nchemba?
Hata hiyo gas ilyogunduliwa kwa wingi as far as Serikali itaendelea kutegemea mirahaba na kodi. hakuna kitu tukachopata kama SERIKALI haitataka kuwa na hisa kwenye Gas.
Nyerere allitegemea VILEO NA SIGARA kwasababu hakuchimba madini yetu, lakini hawa viongozi wa siku hizi pamoja na kuchimba madini yetu bado wanaendelea kutegemea SIGARA na VILEO, UJINGA MTUPU! Sijui kwanini nilizaliwa kwenye nchi ya watu wajinga kama hii ..! Hata kama ni UZALENDO umenishinda kwasababu ya UJINGA wa viongozi wetu.
Leo ni nchi ya TATU Afrika kwa kuuza dhahabu nyingi duniani, lakini pia ni nchi ya tatu DUNIANI kwa ombaomba baada ya Iraq na Afghanistani. In simple language ni nchi ya KWANZA ombaomba barani Afrika, hata Somalia imetuzidi. This is a SHAME.