Bajeti imekosa mvuto?

Bajeti imekosa mvuto?

johnmashilatu

JF-Expert Member
Joined
Sep 16, 2010
Posts
1,037
Reaction score
1,250
Nimejaribu kufuatilia katika maeneo na vyanzo mbalimbali kuhusu mwitikio wa wananchi juu ya bajeti ya serikali ya mwaka 2025/2026, nimebaki nikijiuliza, bajeti haina mvuto? Au wananchi wamekata tamaa kufutilia huo mpango mkuu wa serikali?

Sio katik media au vijiweni, mjadala.kuhusu bajeti iliyosomwa jana, haupewi kipaumbele. Karibu kuchunguza ni wangapi walitenga muda kufuatilia bajeti hiyo?×

Hata katika social media, issue inayojadiliwa ni ongezeko la deni la taifa lakini masuala.mengine yaliyotajwa hayapewi kipaumbele, hata issue ya u-simba na yanga iliyochomekwa haijaweza kuwavuta watu.

mambo yamebadilika. Katika bajeti za awamu zilizopita, media zilitenga muda wa kutosha, zikaleta wachambuzi huru kujadili kabla na baada ya kusomwa kwa bajeti, sasa kimetokea nini?

Nimeona maeneo mengi watu wakiendelea kutazama.vipindi vingine katika TV wakati waziri mwenye mbwembwe akiwasilisha bajeti hiyo.

Sina uhakika wa nini kimepelekea hali hiyo, lakini ukiangalia hali inavyokwenda wananchi wanalitazama.bunge na serikali kama vyombo vyenye kuwakandamiza, visivyojali maslahi yao na badala yake mipango na mikakati yao.ni kwa manufaa ya wenye madaraka.

Unategemea nini kwa mwananchi mwenye mtoto aliyekosa hela ya matibabu au anayesoma chini ya mti kwa kukosa raslimali huku, bungeni wakijadili wabunge wapewa namba maalum au wake zao wapewe VIP treatment?
 
Back
Top Bottom