Bajeti Ijayo ya Tanzania ni Trilion 11 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Bajeti Ijayo ya Tanzania ni Trilion 11

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by MziziMkavu, Jun 3, 2010.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Jun 3, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,607
  Likes Received: 4,599
  Trophy Points: 280
  SERIKALI ya Tanzania imepanga kutumia Shilingi trilioni 11.1 katika bajeti ya mwaka ujao wa fedha 2010/11. Bajeti hiyo imeongezeka shilingi trillion 1.6 ukilinganisha na ya mwaka jana wa fedha.

  Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Waziri wa Fedha na Uchumi , Mustapha Mkulo, alisema kati ya fedha hizo, zinazotarajiwa kukusanywa ni Sh trilioni 6 ambazo ni za mapato ya ndani na Sh trilioni 2.8 misaada na mikopo kutoka kwa wahisani mbalimbali.

  Alisema pia kati ya fedha hizo, Sh trilioni 1.1 ni mikopo ya ndani, Sh bilioni 983.7 mikopo ya masharti ya kibiashara na Sh bilioni 30 ni mapato kutokana na ubinafsishaji.

  Mkulo alisema katika bajeti hiyo, kilimo, huduma za jamii kama elimu, afya na maji, ardhi na umwagiliaji, miundombinu ambayo ni reli, bandari, viwanja vya ndege na nishati ndio vitapewa vipaumbele.

  Bajeti hiyo inatarajiwa kutumia Sh trilioni 7.8 kwa matumizi ya kawaida na Sh trilioni 3.2 kwa matumizi ya maendeleo.

  Hata hivyo, alisema Serikali itaendelea kutumia mikopo nafuu na kuanzia mwaka ujao itatumia mikopo ya kibiashara kwa ajili ya kugharimia bajeti yake.

  Aidha, alisema kwa mwaka wa fedha 2010/11 Serikali inatarajia kukusanya mapato ya ndani yasiyopungua Sh trilioni sita, sawa na asilimia 17.3 ya pato la Taifa ikilinganishwa na mapato ya asilimia 16.4 ya pato la Taifa ya mwaka jana.

  Pia alisema Serikali inatarajia kukusanya Sh bilioni 1.7 kutoka kwenye vyanzo vya halmashauri ambapo pia imelenga kuendeleza mfumo wa makusanyo ya mapato ya ndani, kuimarisha usimamizi na udhibiti wa makusanyo, kuchukua hatua za kupunguza misamaha ya kodi, kutenga fedha kwa ajili utekelezaji wa kaulimbiu ya Kilimo Kwanza.
   
 2. Augustine Moshi

  Augustine Moshi JF-Expert Member

  #2
  Jun 3, 2010
  Joined: Apr 22, 2006
  Messages: 2,210
  Likes Received: 310
  Trophy Points: 180
  Bajeti ya Tanzania ni danganya toto tu! Ona kwa mfano wanasema kati ya fedha zilizotengewa Wizara ya Elimu ya Juu, Sayansi na Teknolojia katika bajeti ya mwaka jana, ni asilimia 60 tu ndio zilitolewa kweli wizarani! (Angalia magazeti ya leo hapo ippmedia.com).

  Kwenye bajeti kama ya Wizara ya Elimu ya mwaka jana ukiweka pembeni 40% ya bajeti ni kwamba unatenga shilingi bilioni 440 kwa matumizi unayojua mwenyewe!

  Bajeti ambayo haina chombo huru cha kuhakiki utekelezaji wake ni pachanga la watoto wadogo. Katika hali tuliyo nayo ya kutawaliwa na wachotaji wa fedha za uma, kikao cha bajeti Dodoma ni matumizi mabaya ya fedha. Ni cha kuhadaa umma!
   
 3. Augustine Moshi

  Augustine Moshi JF-Expert Member

  #3
  Jun 5, 2010
  Joined: Apr 22, 2006
  Messages: 2,210
  Likes Received: 310
  Trophy Points: 180
  2nd June 2010

  Warns Communications ministry over unimplemented recommendations

  The Parliamentary Committee for Infrastructure Development has withheld approval of the 2010/11 Communications, Science and Technology budget proposal because some of the previous recommendations have not been implemented.

  Briefing journalists in Dar es Salaam yesterday, Chairman Mohamed Misanga said his committee had instructed officials from the ministry to furnish it with documents from the Treasury to substantiate certain reports but this had not been done.

  "Unless they bring the documents to us in Dodoma next week we will not approve the budget. As a committee, we are not going to reject their budget proposal in totality but the committee is dissatisfied with the way the ministry acted on the committee's recommendations," Misanga said.
  He noted that despite President Jakaya Kikwete's directive that the ministry allocate 1.0 per cent of its budget for research, it had not done so.

  The committee chairman said research was a cross-cutting issue that touched various ministries but fell under the Ministry of Communications, Science and Technology and the Tanzania Commission for Science and Technology (Costech) was its overseer.

  "We instructed the ministry to check the element of research from other ministries and bring to us a report that the 1-per cent goal has been attained and up to now the figure is 0.001 per cent," he said.
  Misanga cited the issue of physical addresses as another area that the ministry had failed in implementing a study to establish who was where, an exercise he said was relevant to the issuance of national identity cards.

  Another recommendation made by the committee was for the ministry to speed up the installation of the national telecommunications backbone that would reduce the cost of mobile phones, but the ministry did not give any satisfactory implementation report.

  "Mobile phones are now a necessity and not a luxury for the majority of Tanzanians and any intervention that will reduce the cost is worth pursuing," he explained.

  However, Misanga appealed to the government to make sure the budgets approved by Parliament were remitted in full for smooth implementation of projects.

  He said the Ministry of Communications, Science and Technology told his committee that for the 2009/10 financial year, only 60 per cent of the approved budget was received.

  SOURCE: THE GUARDIAN
   
 4. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #4
  Jun 5, 2010
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,605
  Likes Received: 6,173
  Trophy Points: 280
  Mzee mzima umepotelea wapi?

  Nishawahi kusema bajeti yetu haina hata umuhimu au ukweli wa "mchezo wa redio" au hadithi za "Mama na mwana'

  Angalau mchezo wa redio na hadithi vinaweza kuwa na "moral of the story" watu wakajifunza.Hizi bajeti ni hogwash. Kwanza Mkulo kashatuonyesha kwamba serikali yenyewe haijui mapato na matumizi.

  Nina suspect kuna kina Bernard Madoff huko wanachonga mahesabu yaonekane yapo wakati watu wanajichotea tu bila mpango.
   
 5. luhota

  luhota Member

  #5
  Jun 6, 2010
  Joined: May 16, 2010
  Messages: 27
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
   
Loading...