bajeti home hazipangiki, mshahara kiduchu

Felixonfellix

JF-Expert Member
Feb 16, 2010
1,672
182
Salamu wana Jf
Jamani hamjamboo????????
Lipo jambo moja naomba kupata mawazo kutoka kwa wadau
Hivi wengine mnawezaje kuishi kwa mshahara wa serikalini????
Unajua huwa najiuliza mara nyingi maana karibia kila mwisho wa mwezi lazima niwe nadaiwa hasa dukani. Achilia mbali karo za shule kwa watoto na wasaidiwa
Hizi laki mbili kwangu imekuwa ni tatizo kweli.
Rejea thread ya Firstlady1 alipong’amua kuwa kweli wanume tuna kazi nzito maana tunakabiliwa na msululu wa mambo mengi kutimiza maandiko
Hebu jamani nisaidieni maana bujet najitahidi kupanga lakini hazipangiki
Pato laki mbili
Matumizi- chakula, kulipa chumba, nauli, pamba za waifu atoke kama wengine, umeme, maji, simu,n.k
Hebu tusaidiane jamani
 
mkuu.... hizo laki mbili mbona hata mtu mmoja hazitosi kwa mahitaji hayo uliyoorodhesha japo kwa kifupi?............ hahah......embu kama unaweza jifunze ka taaluma ka ufisadi mkuu...... kanalipa sana siku hizi bongo................

unajua tz kuna miujiza mingi sana na mmojawapo ndio huu.................
 
Jibu ni biashara. Tafuta kamtaji, fanya utafiti, fungua biashara otherwise madeni hayataisha. Maisha ni kuhangaika ndugu yangu.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom