Bajeti 2016/2017 imebakiza miezi mitatu muda wake uishe,je imeleta mabadiliko huko kwenu?

iparamasa

JF-Expert Member
Nov 14, 2013
13,437
14,924
Bajeti hii imebakiza miezi mitatu imalizike.

Ilikuwa ni bajeti ya trilioni 29,je katika maeneo mbalimbali nchini kwetu kuna kitu kinachofanana na trilioni 29?

Trilioni 29 zimebadili taifa/mkoa/wilaya/mtaa wako?

Kama imetuachia "hewa" pia sema tu

Tupia jibu lako hapa
#achamanenoonyeshaviwanda
 
Huwezi ukaendesha nchi kwa makusanyo ya kodi trilioni 12 hadi 15 huku ukidai bajeti ni 29 trillion. Mbaya zaidi hii Serikali ilivyo na usiri mkubwa hatutajua katika bajeti ya 29 trilioni 2016/2017 kiasi halisi cha pesa kilichotolewa ni kipi.

Wengi tulisema ile budget ikitekelezeka hata kwa 40% ni muhali....

Kelele za sifa zilikua nyingi but hadi bidget inakwenda mitamboni halmashauri hazijapokea fungu lolote la maendeleo.......
 
labda mabadiliko ya kuwekana ndani na kukomoana, kwan mafuta ya gari za polisi si yanatumia hela ya bajeti
 
Hiyo budget ingekuwa imetekelezeka hata nusu ungesikia majigambo. Kwa ujumla hapo mwanzoni nadharia ilikuwa kubwa ila uhalisia kwa sasa uko wazi ndio maana unaona jazba ikishika kasi. Makusanyo ya kodi yamepungua maana iligeuzwa kukusanya kodi ni kama uhasama hivi.

Yale maneno ya nchi hii ni tajiri na inaweza kuwa Donor country yameyeyuka. Anyway tutoe muda kama wanavyosisitiza lakini kwa mwendo huu sioni uwezekano wa kuwa na bajeti inayotekelezeka wangalau nusu.
 
Mimi sijaona kama kweli mwaka wa bajeti umeisha mmh nimekumbuka kuna uwanja wa ndege nauona hapa jirani
 
Back
Top Bottom