Bahari Beach, Dar: Yaliyojiri kwenye mkutano wa vyama 15 vya Siasa kupinga Muswada wa vyama vya Siasa

Matapeli tu ya kisiasa yataishia kutoa tamko koko
Wakiambiwa uchaguzi kesho wote wanasambaratika kila chama kinasimamisha mgombea
 
Ukisikia siasa za viini macho ndio kama hizi, wakati watanzania wanahitaji katiba ya JMT iliyo bora na inayo endana na mfumo wa vyama vingi vya siasa , nyinyi mnakuja na muswada wa marekebisho ya sheria kwenye vyama vya siasa.
Msajili anashangaza umma wa watanzania kuwa sheria inayo rekebishwa itatoa Uhuru kwa vyama vya siasa kujiendesha kwa mapana zaidi sasa swali ni hili.

Kama kwa sasa katika katiba ya JMT hakuna kipengele kinacho zuia vyama vya siasa kufanya mikutano ya hadhara, Je ni kweli kuwa kwenye marebisho hayo mtaruhusu mikutano ifanyike ?

Nasema hivyo kwa sababu ni wazi kabisa na sheria inasema kuwa ili vyama vya siasa vipate fursa ya kukuwa nilazima vifike kwa wananchi na kunadi Sera zao ili kwamba kama wananchi wakizifurahia na kuona kuwa ni bora na zina wafaa kwa mstakabali wa maendeleo ya taifa basi hawana budi kuziunga mkono.

Swali lingine, kama kwa sasa umewanyima wananchi Uhuru wa kuangalia bunge live ili waweze kuona jinsi gani wawakilishi wao walio wapatia ridhaa ya kuingia bungeni na kuwakilisha hoja zao kwenye chombo nyeti kwa ajili ya mustakabali wa maendeleo yao katika maeneo wanako toka, na hii ingewafanya waweze kuwahukumu vizuri kwenye sanduku la kura mara ambapo muhula wao unapo kwisha na kurudi kuomba kura kwa wananchi.

Msajali baada ya kuja na Sera za kuvitetea vyama vya siasa ambavyo yeye kwake vina mruhusu kuingia sebuleni tu kwa ajili ya maongezi, sasa anataka aingie jikoni aone aina ya mapishi na wanakula nini, badala ya kukaa sebuleni kwa ajili ya maongezi, sasa anataka aingie na chumbani ili aone wanavyo lala.

Ifike mahali viongzi wetu hawa walio pewa dhamana tena kwa vipindi vifupi kama hivi waelewe na ndivyo ilivyo kuwa tunapo zungumzia siasa moja kwa moja tuna gusa uchumi wa wananchi , tunapo ongelea siasa moja kwa moja unagusa maendeleo ya wananchi.

Ifike mahali waachane na siasa zinazo tuletea aibu kwenye jumuia za kimataifa.

Ifike mahali watambue mchango wa vyama vya siasa kwa maendeleo ya taifa letu. Kwani kama sio hivyo vyama watanzania tunge juaje habari za IPTL, ESCROW, MAKINIKIA,, 1•5 Tr, manunuzi mabaya yaliyo fanyika kwenye ununuzi wa vichwa vya treni . nk.

Hakuna ubishi kwamba sehemu kubwa ya maendeleo tunayo yaona yakifanyika kwa sehemu kubwa yamepata msukumo kutoka kwenye vyama shindani.

Na wala sidhani kuwa nidhambi kama viongozi wetu watavitumia vyama hivi shindandani kama jicho lao la ziada kwa kuibua mambo ambayo yana litafuna taifa letu. Na hivi ndivyo kwa kiasi kikubwa vimeibua mchwa walio kuwa wakitafuna taifa letu kimya kimya.

Kama taifa tulianza kupiga hatua nzuri za kidemokrasia, lakini kwa hili linalo taka kufanyika ni ukweli usio pingika kuwa tuna shika kasi tena kubwa sana ya kurejesha nchi yetu kwenye giza totoro, ambako wezi wa Mali za umma wataiba hata bila ya kukemewa, unategemea nini kwa wabunge wa CCM ambao wao kila kitu kwao ni ndiyoooo, wabunge ambao wameshiriki kupitisha hata baadhi ya sheria ambazo baadae zimeonekana kuwa ni mwiba mchungu kwa nchi yetu.

Hebu chonde chonde tushirkiane kujenga Tanzania yetu bila ya kufanyiana figisu figisu ambazo hazina tija.na ukumbuka msemo Rais mtaafu unao sema akili za kuambiwa ongeza na za kwako.
 
Uwanja mpana wa democracy ndo kitu ninachokililia kila siku. ....CCM wenzangu mwenyekiti wang waachie nao uwanja hawa upinzan ni wepesi sana kama tunavowafikilia
 
Mada ni nzuri sana, naomba ui edit kwa kuwacha line moja kwa kila paragraph ili mtu isimchanganye. Well dilivered!
 
Habari wakuu,

Nitawaletea Yanayojiri kwenye Mkutano na Waandishi wa Habari utakaofanyika leo Jumapili, Desemba 9, mwaka huu, kuanzia saa 5 asubuhi, katika Hoteli ya Bahari Beach Ladger Plaza, jijini Dar es Saalm.

Katika mkutano huu, Vyama vya siasa 15 kupitia Viongozi Wakuu, vitatoa tamko la pamoja kuhusu Mswada wa Mabadiliko ya Sheria ya Vyama vya Siasa uliowasilishwa hivi karibuni na Serikali bungeni, wakati wa Mkutano wa 13 wa Bunge la 11, jijini Dodoma.

#UhuruWaKufanyaSiasa.

=====

UPDATES

1200hrs: Bado viongozi hawajafika. Tunawasubiri hapa waseme walichonacho
View attachment 961633

1300hrs: Viongozi wanawaingi.

Vyama vinavyoshiriki mkutano huu ni

ACT, CUF, UPDP, DP, CCK, CHADEMA, CHAUMA, NCCR, NLD na ADC.

1305HRS:
View attachment 961482
Hashimu Rungwe anaongea kwa niaba ya wengine.

Anasema;

Tunaitumia siku hii muhimu ya uhuru kwani ndo historia ya nchi inakumbukwa.

Siku kama ya leo miaka 57 iliyopita, sisi kama taifa tuliweza kuwaondoa wakoloni ambao walikuwa wanatunyima uhuru wa kufanya Siasa na kujiamria mambo yetu wenyewe.

Tunafanya hivyo baada ya kuona mkoloni mweusi anataka kuturudisha enzi za ukoloni.
View attachment 961495
Uhuru wa kufanya siasa unaenda kuhodhiwa na dola. Na Sheria ya vyama vya siasa inafanya shughuli za kiasiasa kuwa jinai.

Tunaanza safari ya kulinda uhuru wetu kama vyama vya siasa na kamwe hatutokubali uhuru huu upokwe

Mataifa mengi yamekuwa na vurugu baada ya kunyimwa uhuru wa kufanya siasa. Sisi hatutaki tufike huko ndo maana tunadai huu uhuru

Tunaomba watanzania wote watuunge mkono katika kuzuia sheria hii kandamizi ambayo inaweza kuingiza taifa kwenye vurugu kubwa.

Tunapinga huu mswaada sababu unakiuka katiba ya ya nchi ya kuwa na uhuru wa kufanya siasa

Mswaada huu, vyama vya siasa hawakushirikishwa vyema

Hata pale tulipotoa maoni yalitupiliwa mbali na hayajatokea kabisa kwenye mswada.

Mswada huu ukipitishwa na kuwa sheria kamili unakwenda kifanya siasa kuwa kosa la jinai.

Msajili wa vyama vya siasa amejipa mamlaka makubwa sana, anaweza kufukuza, kusimamisha mwanachama wa chama cha siasa ndani ya chama chochote.

Msajili ni mlezi na si kuwa na mamlaka ya usimamizi ndani ya chama.

Kabla hata sheria kutungwa na bunge, msajili alishatunga kanuni na kuziwakilisha kwa vyama vya siasa, Hii ni kulizarau bunge.

Kamwe hatuwezi kuwa sehemu ya kulidharau bunge letu

Natoa wito kwa bunge letu lifanye kazi zake kwa nguvu ya mamlaka yake.

Maneno tunayopinga kwenye mswada huu;

Mswada unaua msingi wa sheria wa kuundwa kwa vyama vya siasa 1992 ya Demokrasia ya vyama vingi nchini.

Msajili sio msajili tena bali mdhibiti wa vyama vya siasa.

Kifungu cha nne kinafanyiwa marekebisho ambayo yanageuza msajili wa vyama vya siasa kuwa mdhibiti

Udhibiti wa wa wanachama ni wa vyama wenyewe kupitia katiba ya chama chao sio msajili.

Mswada umejaa mambo ya kijinai unaofanya kazi za siasa kuwa jinai wakati ni haki ya katiba. Wameweka adhabu ya kifungo au faini.

Kifungu namba tatu kilichofanyiwa marekebisho, kinatoa mamlaka kwa msajili kuingilia uchaguzi wa chama wakati yeye sio mwanachama.

Inadhibiti vyama kuwa na mahusiano na mashirika, vyama kutoka nje ya mchi.

Mswada unampa mamlaka makubwa msajili, kwamba taarifa zote za mwenyekiti wa chama apewe msajili.


Msajili wa vyama vya siasa, amewekewa kinga ya kutoshitakiwa mahakamani.


Msajili kapewa mamlaka ya kuingilia uteuzi wa wagombea ndani ya vyama.

SALUM MWALIMU

Ukiharibu siasa, unaharibu maisha ya wananchi. Hii ni kutaka kutimiza yale wanayosema kuumaliza upinzani nchini kabla ya 2020. Walianza kurubuni watu wetu, sasa wanataka kutudhibiti kwa sheria. Sisi tunataka siasa za ustaarabu.
View attachment 961517
Kifungu kinachomtaka msajili kuwa na taarifa na kuomba vibali vya. kutoa mafunzo na semina kwa wanachama wao. Anatakiwa aambiwa kinachoenda kufundishwa, mfadhili wa mafundisho nakinachofundishwa ndani ya chama. Hapo ndo atoe kibali cha mafunzo. Kuwajengea uwezo viongozi hadi uwe na kibali cha msajili

Msajili hashitakiwi kwa atakachokifanya. Hii na baada ya kukivuruga CUF akashitakiwa sasa wamemuwekea ulinzi.

Sura ya 8d. Msajili napewa mamlaka ya kukielekeza chama chochote kifanye marekebisho ya katiba yake na ndani ya miezi sita anaweza akakifuta

Msajili anaweza akaamua nini kiwekwe kwenye katiba ya chama cha siasa

Sura 18. Sheria inasema chama kikiwa na hati chafu kwenye ukaguzi, msajili atazuia ruzuku kwa miezi 6

21e. Msajili anaweza mvua uanachama chama chochote. Hapa anawalenga viongozi wa vyama vya kisiasa. Mswada unasema Waziri ataweka kaununi za namna gani avuliwe uanachama. Waziri ni CCM na Msajili anateuliwa na Mwenyekiti wa CCM.

Mwenyekiti wa ACT Wazalendo Yeremia Maganja anasema Tunapingana na Mswaada huu.

Mwenyekiti wa CCK Anasema tunapingana na mswaada huu.

Katibu mkuu wa CHADEMA anasema tunapinga marekebisho ua mswada ya vyama vya siasa kwani unapingana na katiba pia msajili anatuchagulia viongozi.

Joram Bashange naibu katibu mkuu wa CUF. Anasema CUF inapinga mswada huu na marekebisho yake. Anasema sheria hii wameikopi kutokwa sheria ya Rwanda ya mwaka 2013

Jojia Mtikila mwenyekiti wa DP nasema kwamba chama chake kinapingana naa mswada huu. Anasema ameshiriki kuandaa tamko hili. Ofisi ya msajilinimewekwa kudhibiti upinzani. Tunapinga hiki kitu

Benard Mng'ongo wa NCCR anasema sisi kama chama tulipeleka mapendekezo kabla lakini hayakufanyiwa kazi. Hatukubaliani na mswada huu, tunapinga. Mtu mmoja amepewa mamlaka wa kubadilisha katiba ya chama chochote.

NLD nao wameshiriki ila wapo kweye mkutano mkuu.

Mwenyekiti wa UPDP Dovutwa anasema;

Nmeshiriki na chama changu katika hatua zote za kuanda tamko hili lililosomwa. Tunapinga na hatutaki mswada huu.

AbdallahMohamed aliyemuwakilisha katibu mku wa ADC kwa kupinga mswaada ulioletwa na Serikali. Huu mswada unalija kunyonga Demokrasia. Jambo hili hatukubaliani nalo. Wafanye marekebisho lakini si kwa namna hii. Sisi ni wawakilishi wa watanzania walio wengi. Hatuungi mkono mswada huu kwa vyovyote vile. Hatuukubali.

ZITTO KABWE ANASEMA;

Mzee Rungwe kasoma tamko kwa niaba yetu. Tunapingana na mswada huu.

Bunge likashatunga sheria ndo mamlaka ya kutunga kanuni hukaa. Lakini kama mlevyoelezwa, mswada huu hata kwenye mamlaka ya bunge haujaanza kujadiliwa, kanuni zilikuwa zimeshaandaliwa.

Hivyo ni dhahili, Serikali ya CCM kuna kitu iliahakipanga.

Mbegu iliyopanda miaka ya 90 kutaka mfumo ya demokrasia ya vyama vingi imee tena.

Kwenye mswada huu, Msajili anaweza kuamka asubuhi na kusema chama hiki kifute au mwanachama huu sio wa chama fulani.

Tusiione hii demokrasia ukadhani ilikuja tu, kuna watu walipambana na wengine washatangulia mbele ya haki na wenfine bado wapo ni waze. Wakina Komu, Mbatia, Mbowe kipindi cha vuguvugu la vyama vingi, walikuwa wanafunzi wa Serikali za Wanafunzi. Sisi ACT tutawapa ushirikiano wa kutosha. Mswada huu ni hatari

adolf hitler alifanya kitu kama hiki. Kilichotokea kila mtu anajua. Tuungane kupinga mswada huu.

MASWALI;

Mashinji anajibu Kuhusu Luzuku

Ni kwaajili ya kukuza demokrasia nchini

Kizuia mamruki wa nje kuja nchini.

Sheria iliyopo ni bora kuliko mapendekezo yanayopendekezwa. Vyama vya siasa kila mwaka vinakaguliwa. Huu mswada unalengo wa kidhibiriti luzuku. Inampa mamlaka mtu mmoja kutoa maamuzo bila kushirikisha mtu yoyote.

Watu wanamshambulia Mbowe na Luzuku ya CHADEMA. Lakini anayehusika na Luzuku ni mimi katibu mkuu na wasaidizi wangu.

JE KUNA MSWASA MBADALA?

Rungwe anajibu;

Sheria tuliyonayo ni nzuri ilitungw a mwaka 1992, ni nzuri wala haina matatizo. Hii sheria mpya wameicopy kwenye nchi yenye matatizo. Sisi watanzania tuna maadili yetu na utamaduni yetu. Hii iliyoletwa haifai kabisa. Tutapinga hii, tuendelee na ya zamani. Huyu msajili ni sawa na msajili wa makampuni. Kapewa mamlaka makubwa.

JE, MBONA VYAMA VINGINE HAVIPO?

Rungwe anajibu.

Sisi tumewawakilisha, wengine watakuja tuunvane nao. Hii ni hiyari ya mtu. Sisi tulio hapa tunapinga huu mswada.

HUKO NYUMA MLIUNGANA MKAISHIA KATIKATI, VIPI LEO?
Bashange anajibu. Mchakato wa kutunga sheria hii ulianza 2013 ukafeli, ukaja 2017 wakatunga sheria yenye vifungu 71 ilivyofika bungeni wakaviondoa. Safari hii wameleta sheria ya Rwanda wakachomekea kwenye sheria ya 2017. Tunapopata nguvu ya kuungana, mtikisiko unakiwa mkubwa. Vyama vipo 18 ukiondoa CCM. Tunaungana sasa kutokana na yaliyo mbele yetu. Kwanini mdhibiti asiwe na mamlaka? Mwenye matatizo kwenye fedha za Serikali ni CCM sio Mbowe wala CUF.

Hakuna chama kunachofadhiliwa kama CCM. China inamwaga fesha CCM mbona haulizwi?

Sheria iliyopo inajitosheleza. Malawi, kenya, zimbambwe na rwanda. Kenya tume ya taifa ya uchaguzi ndo nateua msajili. Kwetu msajili anayeuliwa na mwenyekiti wa CCM. Ofisi ya Msajili ipo chini ya Waziri mkuu kada wa CCM. Hii sheria haifai. Imekuja kuua vyama vya upinzani.

MAONI YENU JE, YALIFUTWA?

Mwalimu anajibu. Baraza la vyama vya siasa tulikutana januari, tuliletewa msada tuupitishe tukakataa. Tukaweka utaratibu wakirudo kwenye baraza ili kila chama kitoe maoni yake kutoka vyam vya siasa. Hilo halikifanyika. Juzi tuliambiw asheria na kanuni zipo na walitaka tupitishe. Tulikataa pia. Vyama siasa hatujapewa fursa ya kutoa mawazo.

Mwandishi anauliza eti kwanini tumekuja kupinga. Hapa hatujaja kupinga bali tumekuja kiwapa nyie ili muweze kusikiliza mupokea na kuhabarisha umma. Tunatimiza wajibu wetu.

Zitto anajibu swali la Waliotunga mswada hui ni watu gani?
View attachment 961610
Waliotunga mswada huu ni mbumbu wa mdhibiti wa fedha za Serikali.

Sheria imasema ukipata hati yenye mashaka eti unafutiwa luzuku. Kama ni hivyo Serikali ilitakiwa ifutiwe Luzuku sababu 70% Wizara zinapata hati zenye mashaka.

Sheria hii inazua vyama kupata fedha kutoka kwa wafadhiri wa nje. Sheria iliyopo iliweka utaratibu namna gani hela hiyo itawekwa wazi kwa CAG.

Serikali yenyewe inapata msaada kutoka nchi za nje. CCM inapaka fedha kutoka CHINA. Sasa hivi wanachama wa CCM wanaenda china kwenye mafunzo. Katibu mkuu wa CCM Bashiru alienda china kwenye mafunzo. Ukumbi wa CCM umejengwa na china hata chuo cha ukombozi kinajengw ana china. Busara ya kawaida inakataa juu ya huu mswada. Mswada huu haupaswi kujadiliwa ndani ya bunge wala kisogelea ukumbi wa bunge.
View attachment 961618
View attachment 961651


TAMKO LA VYAMA VYA SIASA VYA ACT-WAZALENDO, ADC, CCK, CHADEMA, CHAUMA, CUF, DP, NCCR-MAGEUZI,NLD NA UPDP-KUHUSU MUSWADA WA MAREKEBISHO WA SHERIA YA VYAMA VYA SIASA 2018.

# UHURU WA KUFANYA SIASA.

1.0 UTANGULIZI

Ndugu wanahabari,

Sote tunafahamu uwepo wa Muswada wa Marekebisho ya Sheria ya Vyama vya Siasa ambao umesomwa Bungeni tarehe 16 Novemba, 2018.

Toka ilipoingia madarakani, Serikali ya awamu ya tano imejipambanua vyema isivyo kuwa muumini wa demokrasia, sheria na hata Katiba ya nchi yetu. Rais Magufuli akiwa mkoani Singida katika mkutano wa Chama chake alitoa zuio la vyama vya siasa kufanya mikutano ya hadhara.

Pamoja na ukweli kuwa zuio hili ni kinyume cha Katiba na Sheria za nchi yetu, ambayo inatoa haki kuunda vyama vya siasa na kutoa uhuru wa vyama hivyo kunadi sera zake kwa wananchi wakati wowote vitakapoona inafaa. Tunaendelea kupinga zuio hili.

KWANINI SIKU YA UHURU!

Tumeitumia Siku ya Uhuru kutoa tamko hili kwani Siku muhimu kwa Taifa letu pamoja na utawala wa awamu ya tano kuendelea kufuta Sherehe za uhuru ambazo duniani kote nchi hutakiwa kuikumbuka siku hii kwani ndio taifa linakuwa limezaliwa, ndio historia ya kuwa nchi inapokumbukwa.

Siku kama ya leo miaka 57 iliyopita sisi kama taifa tuliweza kumwondoa mkoloni ambaye alikuwa akitunyima uhuru wetu wa kufanya siasa na kujiamulia mambo yetu, tunaitumia siku hii kwa sababu tunaona hatari ya 'mkoloni mweusi' kurejea na hivyo inatulazimu kumpinga kama tulivyofanya miaka 57 iliyopita!

Tumeiita siku ya kudai 'uhuru wa kufanya siasa' katika taifa letu kwa sababu sheria inayopendekezwa na Serikali inaenda kuondoa kabisa uhuru wa kufanya siasa katika taifa letu na uhuru huo sasa unaenda kuhodhiwa na dola, na inafanya shughuli za kisiasa kuwa jinai.

Tumeanza rasmi safari ya kuudai uhuru wetu kama vyama vya siasa wa kufanya shughuli za kisiasa na kamwe hatutakubali uhuru huu upokwe na dola, na ni jambo la hatari sana kwa Taifa kuruhusu uhuru huu kupokwa kwani historia inaonyesha kuwa mataifa mengi yamekuwa na vurugu kwa sababu ya watu kunyimwa uhuru wa kufanya siasa na hivyo kuamua kuudai uhuru huo kwa njia za vurugu, sisi hatutaki taifa lifikie huko ndio maana tumeamua kuudai uhuru huu kabla haujapokwa na kuliingiza taifa katika matatizo.

Tunatoa mwito kwa Watanzania wote wanaoipenda nchi hii bila kujali rangi, dini, kabila na itikadi zao watuunge mkono katika kuizuia sheria hii kandamizi na ambayo inaweza kuliingiza taifa katika vurugu kubwa siku za usoni.

3.0 SABABU ZA KUIPINGA SHERIA HII

Mosi, muswada huu unakiuka Katiba ya nchi inayotoa uhuru wa kujumuika na kuunda vyama vya siasa.

Pili, vyama vya Upinzani kama wadau muhimu na wahusika wakuu havikushirikishwa vyema katika mchakato wote wa kuandaliwa kwa muswada huu. Hata pale tulipotoa maoni yetu, bado Serikali imeyatupilia mbali na hayatatokea kabisa katika muswada huu.

Tatu, muswada huu ukipitishwa na kuwa Sheria kamili unakwenda kufanya shughuli za kisiasa kuwa kosa la jinai hapa nchini. Tunaona kauli ya Rais kuzuia shughuli za vyama vya siasa hususani vyama vya upinzani ikitengenezewa sheria kinyemela.

Nne, Msajili wa vyama vya siasa amejipa mamlaka makubwa sana kwa kiwango hata cha kuwa na uwezo wa kuingilia maamuzi ya ndani ya vyama vya siasa na kufukuza/kusimamisha wanachama wa vyama vya siasa. Msajili wa vyama vya siasa anapaswa kuwa mlezi wa vyama vya siasa na si kujigeuza na kuwa mamlaka ya usimamizi (Regulatory Authority).

Sita, Kabla hata sheria kutungwa na Bunge tayari Msajili wa vyama vya siasa ameshatunga kanuni na kuziwakilisha kwenye kikao cha kamati ya uongozi ya Baraza la Vyama vya siasa, huku ni kulidhrau Bunge kwamba halitaweza kubadilisha kipengele chochote cha sheria hii, kamwe hatuwezi kuwa sehemu ya kulidharau Bunge letu.

Tunatoa wito kwa Bunge letu, bila kugawanywa na tofauti za kiitikadi na vyama lifanye kazi yake vyema likilinda kwa wivu mkubwa mamlaka yake.

4.0 MAENEO MAHUSUSI TUNAYOYAPINGA KWENYE MUSWADA HUU.

4.1 Muswada umeleta marekebisho mengi ambayo yanaua msingi wa kutungwa kwa Sheria ya Vyama vya Siasa Na. 5 ya mwaka, 1992. Msingi wa Sheria ya Vyama ya mwaka 1992 ulikuwa ni kuweka utaratibu wa uwepo wa vyama na mfumo wa vyama vingi lengo likiwa ni kuwezesha ujenzi wa demokrasia ya vyama vingi nchini.

4.2 Muswada unampa mamlaka makubwa Msajili wa vyama vya siasa, sio tena Msajili wa vyama bali ni Mdhibiti wa Vyama vya siasa. Kifungu cha 4 kinafanyiwa marekebisho ambayo yanamgeuza Msajili wa vyama vya siasa Mdhibiti (Regulator) wa vyama. Msajili wa vyama vya siasa hapaswi kuwa na madaraka ya kudhibiti vyama. Madaraka ya kudhibiti vyama ni ya wanachama wenyewe wa vyama kupitia Katiba ya kila chama.

4.3 Muswada umejaa adhabu za kijinai na hivyo unafanya shughuli za Vyama kuwa jinai wakati ni haki ya kikatiba. Vifungu vipya vyote vimeweka adhabu ya faini au kifungo au vyote hata kwa mambo madogo kama vile kukosea taarifa au Msajili akitaka kujua taarifa za vikao vya chama.

4.4 Kifungu cha 3 ambacho kinafanyia marekebisho kifungu cha 4 cha sheria ya Vyama vya siasa kinatoa mamlaka kwa Msajili wa vyama vya siasa kuingilia mfumo wa uchaguzi wa ndani ya Chama na kuamua nani awe kiongozi wa chama, wakati yeye sio mwanachama wa chama husika.

4.5 Kifungu cha 5 kinatunga kifungu kipya cha 5A ambacho kinatoa sharti juu ya elimu ya uraia/mafunzo ya kujenga uwezo yanayotolewa na taasisi au mtu aliyesajiliwa nchini au nje ya nchi kabla ya kufanya hivyo anatakiwa kuomba kibali kwa msajili wa vyama vya siasa, kimsingi lengo ni kuvithibiti vyama kuwa na mahusiano na mashirika au taasisi za kimataifa katika kuvijengea uwezo vyama kwa njia ya mafunzo.

4.6 Muswada unampa mamlaka makubwa Msajili wa vyama kutaka taarifa yoyote kutoka kwenye Chama au Kiongozi wa Chama. Mamlaka haya ni jumuishi. Rejea kifungu kipya ya 5B cha muswada, na asipopewa hata kama ni taarifa za siri chama husika wanachama na viongozi wanakabiliwa na adhabu ya faini na kifungo.

4.7 Kifungu kipya cha 6A (3) kinaingilia utaratibu wa Katiba za Vyama kwa kutoa sharti kuwa Mkutano Mkuu au Kamati Kuu visikasimu mamlaka yake kwa vyombo vingine ndani ya chama. Hii ni aibu kwani hata Bunge lenyewe huwa linakasimu mamlaka yake kwa kamati mbalimbali za Bunge na kuzipa mamlaka ya kufanya maamuzi kwa niaba ya Bunge zima.

4.8 Kifungu kipya cha 8D (2) kinampa mamlaka Msajili kuamuru Chama kufuta au kurekebisha kifungu chochote cha Katiba yake, Msajili ataamuru vyama kuwa na katiba zinazofanana kwani amepewa mamlaka hayo.

4.9 Kifungu kipya 8E kinazuia Vyama kuwa na kikundi cha Ulinzi, kifungu hiki ni kibaya kwa sababu ulinzi ni jukumu la kila mtu kwa mujibu wa Katiba yetu.

4.10 Kifungu kipya cha 11C kinampa Waziri dhamana ya kutunga Kanuni za Vyama kuungana (coalitions) ni lazima Sheria iweke misingi mikuu ili kumzuia Waziri kutunga Kanuni mbovu kama tulivyoona kwenye suala la mafao ya wafanyakazi.

4.11 Kifungu cha 21E kinampa Msajili mamlaka ya kumsimamisha/kumfukuza Mwanachama wa Chama cha siasa. Lengo hapa ni kuwaondoa viongozi wa vyama ambao wanaikosoa Serikali kwani msajili akimsimamisha uanachama na uongozi wake unakoma, aidha kuna uwezekano Msajili akakitumia kifungu hiki nyakati za chaguzi mbalimbali kama za Urais, Ubunge, na Udiwani kuwafukuza wagombea ambao wanaonekana kukubalika kwa wananchi na hivyo kuwafanya wagombea wa CCM kupita bila kupingwa.

4.12 Kifungu cha 6A (6) kinazuia vyama vya siasa kufanya shughuli za kiharakati au kuweka shinikizo kwa umma kuhusu masuala yanayohusu watu. Kifungu hiki hakifai kwani kinafuta dhana na dhima anuai ya chama cha siasa kama chombo cha kupinga ukandamizwaji na kutetea haki. Maana ya kifungu hiki ni kuwa sasa vyama havitatakiwa kuwatetea wafanyakazi, wakulima, wavuvi na makundi mbalimbali katika jamii kwani kufanya hivyo ni kufanya harakati.

HITIMISHO.

Kwa kuwa Muswada huu una nia mbaya na ovu, Msajili wa vyama vya siasa anawekewa kinga ya kutoshtakiwa Mahakamani.

Kifungu cha 6 kinamlinda Msajili wa vyama vya siasa na Maafisa wake kutofunguliwa mashtaka wakati wa utekelezaji wa majukumu yao hapo juu. Sasa ni wazi kuwa kama sheria hii ikipitishwa Msajili atafanya maovu yote na kamwe hataweza kushtakiwa na huku ni kumfanya Msajili kuwa juu ya sheria kitu ambacho kinapigwa marufuku na katiba ya nchi.

Sasa ni wazi kuwa msajili anajiwekea mazingira ya kuhalalisha kuvuruga vyama vya siasa kisheria kwani alipojaribu kuiharibu CUF amejikuta akiburuzwa Mahakamani na imekuwa fedheha kubwa kwake.

Kutokana na hila mbaya zilizojificha katika Muswada huu, tunatoa wito kwa Wabunge wote, Wadau wa siasa, Taasisi za Dini, Mashirika yasiyo ya kiserikali na Jumuiya ya Kimataifa kwa ujumla kuupinga muswada huu.

Wabunge wasipotimiza wajibu wao wajue kuwa sasa Msajili wa vyama ndiye atakaeamua ni nani agombee ubunge kwenye Jimbo fulani kwani sheria inampa mamlaka ya kuingilia uteuzi wa wagombea ndani ya vyama, hakuna atakayekuwa salama kwa sheria hii.

Tamko hili limetolewa leo tarehe 09.12.2018 na viongozi wa vyama vya siasa vilivyotia saini hapa chini kama ifuatavyo;

YEREMIA MAGANJA.

ACT-WAZALENDO.

DOYO HASSAN DOYO.

ADC.

DAVID MWAIJOJELE.

CCK.

DR. VINCENT MASHINJI.

CHADEMA.

HASHIM RUNGWE.

CHAUMA.

JORAM BASHANGE.

CUF.

GEORGIA MTIKILA.

DP.

MARTIN MUNG'ONG'O.

NCCR-MAGEUZI.

TOZI MATANGWA.

NLD.

FAHM DOVUTWA.

UPDP.
Kama mmekosa ya kufanya nendeni mkalime. Uhuru wa kiuchumi bado. Hamasisheni vijana wapate technolojia ili taifa liendelee ki tech. Hizo siasa ni maneno tu kama ya kwenye kanga.
 
Wanafiki tu hao wasaka tonge
ISIS haupo sawa wewe, IBILISI anatawala maisha yako, okoka. Wewe ni moja ya watu ambao hawaamini katika Mungu Muumba mbingu na nchi, huu ni muda wako wa kuomba toba umuabudu Mungu wako. Kutokumjua Mungu wako aliyekuumba inapelekea pia kuwa na akili chafu, na ni mara nyingi pia umekuwa ni mtu wa kuisafisha CCM humu ndani.

Badilika dada yetu, Mungu anakupenda.
 
'...sheria hii wameikopi kutokwa sheria ya Rwanda ya mwaka 2013'
uswahiba wa mkulu na mwenzie wa Rwanda unagharimu sana nchi!!!
 
Back
Top Bottom