Mbinu hii chafu ya ccm ndo imesaidia kufanyika mageuzi ya kweli nchini kenya.
Mienzi minne baada
ya mwenyekiti wa CHADEMA wilaya Bagamoyo kutekwa na kuteswa na wanaCCM
Oktoba mwaka jana wakati wa uchaguzi wa kata ya magomeni. UBABE
umeendelea kutumika kuhakikisha CCM inaendelea kushinda kila CHAGUZI!...
Hali hii imepelekea vurugu kubwa kuzuka katika kijiji cha kidomole!...
Hali hii inatokana na msimamo wa CCM kuhakikisha kwa namna yoyote
CHADEMA haichukui nafasi yoyote ya kuongoza eneo la BAGAMOYO kwa madai
kuwa ni aibu kwa WAKUBWA!...
Utamaduni wa chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kukamia kila
uchaguzi mpaka chaguzi za vijiji na vitongoji umeleta kizaa zaa katika
kijiji cha kidomole mchana wa leo!...
Kidomole ni moja ya vijiji 7 vya jimbo la Chalinze wilaya ya Bagamoyo
ambavyo uchaguzi wa viongozi wa vijiji na vitongoji vyake umefanyika
leo.
Kwa wiki tatu mfululizo uongozi wa CHADEMA mkoa wa pwani, wilaya ya
Bagamoyo, jimbo la Chalinze na kata husika uliwekeza nguvu kubwa
kuwakikisha ushindi unapatikana.
Hali hii iliishitua CCM na kumwaga pesa na makada kwa siku 2 za mwisho
ambao wamekuwa wakizunguka nyumba kwa nyumba nyakati za usiku kushawishi
wapiga kura wawapigie. Viongozi wa serikali na yule kijana tajiri
kuliko wote TANZANIA walitia timu jana na juzi.
CCM iliamua kuwekeza nguvu kubwa kidomole ambako kuna migogoro mikubwa
ya ardhi iliyowafanya viongozi na wananchi kuvunja uongozi na kuhamia
CHADEMA april mwaka jana. Hivyo CCM iliamua kuhakikisha CDM haipiti.
Leo uchaguzi umeanza saa 2 asubuhi kukiwa na majina ya wagombea wa CCM
pekee vituoni - ya wagombea wa CHADEMA yakiwa yamefichwa na wasimamizi
wa uchaguzi. CCM walionekana wakiwazuia wafuasi wa CHADEMA KUPIGA KURA
na vikosi vya katibu mwenezi wa CCM aitwaye BOLIZOZO au ZOZO kwa ufupi
vikiwasaidia wanaCCM kupiga kura mara nne nne!!.
Wana CDM walipopinga hali hii waligeuziwa kibao na kuanza kupigwa kwa
fimbo, mawe na mapanga. Wanachadema wengi wameumizwa ingawa hawapo
katika hali mbaya. CCM walionekana kuwa wajiandaa kwa silaha.
Hivi sasa viongozi watatu wa CHADEMA wamekamatwa na wanaCCM polisi
wamekuja kuwachukua. Mwenyekiti wa CHALINZE Torongey mpaka sasa yuko
kituo cha polisi BAGAMOYO.
Source: Mimi - Katibu Mwenezi wa CHADEMA BAGAMOYO.