Bado tunazikumbuka jamii zetu??

Dark City

JF-Expert Member
Oct 18, 2008
16,253
11,598
Ndugu wana MMU,

Hivi majuzi nilipata nafasi ya kutembelea mitaa ya watu wa kawaida na kukutana na maisha halisi ya Watanzania. Nilijihisi na kukubali kuwa nimetengwa (detached) na maisha ya kawaida ya ndugu na jamaa zangu...Baadhi ya mambo niliyoshuhudia ni ngumu kuamini!

1. Kuna jamaa yangu ndiye mwenye simu katika kimtaa chake..kwa hiyo inaazimwa na kuzunguka karibia usawa wa mabalozi 2 wa nyumba kumi kumi. Watu wanafanya kubadilisha chips...Kwa hiyo alinambia nisipompata nijue simu iko kwa majirani!
2. Mwingine alinambia kuwa redio yake ikiharibika basi unakuwa mwisho wa kupata chakula cha usiku. Anasema kwa jinsi vyumba vilivyobanana na kwa vile hakuna ceilings...redio ndiye mkombozi wao...Hii ilitokana na mshangao wangu wa kwa nini redio zinapigwa karibia 24hrs
3. Kuna wengine hawana vyoo...kwa hiyo wanapata hifadhi kwa majirani...Hapa nikamkubuka Ex-GF wangu ambaye aliwahi kunambia kuwa hajawahi kuchimba dawa (kubwa) porini!!
4. Watu wengine walishasahau sura za noti..ukimpa noti ya shs 500 au 1000 anafunga novena kukuombea!!
5. Jamaa niliosoma nao miaka ile wanaonekana kama babu zangu...wamechoka na tayari wengine tumeagana...very sad in deed
6. Pamoja na matatizo niliyoona,....bado watu wametinga T-shirt za kijani za kuanzia Mkapa 1995 hadi JK 2010 na mabango yao. Pia bendera za kijana ndio zimepamba mitaa yao utadhani wanaandaa dhifa ya Taifa kwa Mgeni maarufu wa Ikulu..
7. Pamoja na kutambua kuwa sumu inayowaua ni umaskini...hawataki kusikia sauti nyingine zaidi ya kuwaeleza kuwa walinde amani yao!!
 
sooooo sad DC, wapi huko, maaana kijijini kwetu naona pamekucha tu
ila mama angu mdogo alinipa kali, eti anasikia mjini kuna vyama vingi mbona
wao sijawapelekea?? nikajiuliza how?nikabaki kucheka tu
 
sooooo sad DC, wapi huko, maaana kijijini kwetu naona pamekucha tu
ila mama angu mdogo alinipa kali, eti anasikia mjini kuna vyama vingi mbona
wao sijawapelekea?? nikajiuliza how?nikabaki kucheka tu

BB,

Ngoja niwalindia heshima na utukufu wao (kama wale wachunga kondoo wanaotumaliza na heroin)!! Yaani nimekubali kwamba hiz key boards zimetutenga sana na ndugu zetu!!

Kuna vitu hata nilishasahau kwamba vipo katika dunia hii...mfano kwenda "toilet" bila maji wala toilet paper na badala yake unaambiwa kuwa wenyewe wanatumia majani ya miti...Mhhhhhh.....Hii dunia hata sijui ikoje!!
 
Kawaida sana hii kule kwetu, mie pia nimekulia mmazingira hayo, na juzjuz tu nilikuwa huko muendelezo ndio huuhuu
unabeba jembe shambani huko kumaliza ishu, choo cha wageni ili kisijae, tena waliotoka dar
 
Sasa hawa ndugu zetu wanaoishi kama vile ni 1800s, wanaelewa hizi nyimbo za siku hizi za..kasi zaidi..nguvu zaidi na ari zaidi? Tena katika kufanya mambo negatively??
 
Kawaida sana hii kule kwetu, mie pia nimekulia mmazingira hayo, na juzjuz tu nilikuwa huko muendelezo ndio huuhuu
unabeba jembe shambani huko kumaliza ishu, choo cha wageni ili kisijae, tena waliotoka dar

Umenikumbusha mbali sana D,

Huko sehemu sehemu watu wanahisi Dar ni zaidi ya mbinguni..Kipindi nasome kidogo nipate mke kirahisi. Nilimtania dada mmoja kwamba kama yuko tayari ajiandae twende naye Dar...Yaani alinikalia kooni hadi ikabidi nitoroke wakati narudi shule...Kama ningekuwa tapeli huyo daa labda leo angekuwa anazurura katika mitaa ya dar!!
 
Cha ajabu saaana whatever differences kati ya wanadamu kila mmoja hukubali

na kuzoea mazingira yake... thou wa juu aweza shangazwa saana na anaeonekana

kama low life... Hio picha ume paint... ndo the type of jamii hataki kabisa change...
 
Back
Top Bottom