ExpertBroker
JF-Expert Member
- Jun 1, 2009
- 454
- 107
Mtu NHC anaambiwa alipe Laki 9 kwa Mwezi je mshahara kazini ngapi anapata kwa Mwezi Si njia za kufukuza watu hizi kwenye nyumba? Nyumba watachukua wenye pesa nyingi za mishahara wakati hao wanauwezo WA kujenga au kupanga sehemu, Tanzania imefika muda Dodoma,Tanga, Na Mikoa ya Kati ifanyiwe ujenzi WA makazi Na ukaaji kwa miundo inayotakiwa Dar-es-Salaam kuwekwe usafi Na kupunguzwe wakazi waone bora kukaa mkono kwenye Kazi Na pakukaa kwa nafuu Na elimu kwa Watoto Na Salama.nyumba ya mil 80 ambayo mtaan wewe mwenyewe unaweza ijenga kwa mil 40 ndugu zetu wa NHC wanakwambia eti hiyo ndio low cost housing!!!! alafu wanalalamika watu hawanunui
nyumba ya mil 80 ambayo mtaan wewe mwenyewe unaweza ijenga kwa mil 40 ndugu zetu wa NHC wanakwambia eti hiyo ndio low cost housing!!!! alafu wanalalamika watu hawanunui
Mipango miji Urban Planning kwetu bado ni mgogoro sana; hivi hushangai taasisi za huduma za jamii kama maji, umeme hazijui tathmini ya kiasi cha huduma kwa eneo husika! Yaani unajenga nyumba halafu unaungiwa bomba kwa style ya T; kuunganisha bomba katika bomba la maji yaendayo kwa mtu karibu yako. Vipi upimaji wa viwanja; ni nani hasa mwenye idhini - ni serikali au yule jamaa mwenye shamba lake anakukatia kisehemu kutoka kwako ambako hata hana hati wala kujua hasa eneo lake liko vipi?
Tusipojiweka vizuri bomoa bomoa itaendelea tu; usishangae ikaingia hata city center -Kha ...!
Kama lipo litumbuliwe harakaKwa hiyo kuna jipu
Kuna ujumbe upo hapa ingawa umepinda pinda sana..!Mtu NHC anaambiwa alipe Laki 9 kwa Mwezi je mshahara kazini ngapi anapata kwa Mwezi Si njia za kufukuza watu hizi kwenye nyumba? Nyumba watachukua wenye pesa nyingi za mishahara wakati hao wanauwezo WA kujenga au kupanga sehemu, Tanzania imefika muda Dodoma,Tanga, Na Mikoa ya Kati ifanyiwe ujenzi WA makazi Na ukaaji kwa miundo inayotakiwa Dar-es-Salaam kuwekwe usafi Na kupunguzwe wakazi waone bora kukaa mkono kwenye Kazi Na pakukaa kwa nafuu Na elimu kwa Watoto Na Salama.
NHC wameomba serikali iwaruhusu wauze na kupangisha nyumba zao kwa wageni...
hii nchi shida tupu
Muheshima ni low cost kwa maiaha ya watu wa kawaida kama hiyo pesa unaiilipa up to almost 20 years, mimi nimechukua hiyo ya m60 nimekusanya millioni 3 nikakopa benki 3 nikawa na jumla ya m6 nikalipa down payment ya 10% then baada hapo nikikabithiwa na lipa laki mbili kwa mwezi mpaka namaliza,nyumba ya mil 80 ambayo mtaan wewe mwenyewe unaweza ijenga kwa mil 40 ndugu zetu wa NHC wanakwambia eti hiyo ndio low cost housing!!!! alafu wanalalamika watu hawanunui
kwa mfano pale magomeni kota, msimbazi, na temeke, kama vile vijumba vimeshaonekana havifai (kuchoka kutokana na umri na maendeleo ya jiji) basi vibomolewe na zijengwe flats aidha iwe ni mradi wa hizi taasisi zetu za kifedha, au NHC wa-initiate mradi wa kifedha unaofanana na NSSF, PSPF n.k. ambapo kwenye hizo flats wakazi wake watakuwa wanalipa kwa kukatwa kwenye mishahara kama zifanyavyo hizo taasisi za kifedha.
Hiyo hela inayokatwa ni ya pango let's say 70% na 30% subscriber's contribution kwenye mfuko wa nyumba. mfano unakatwa kwa mwezi 100,000, ni bora na naamini utakaa kwenye nyumba inayoeleweka isiyo na usumbufu na hutajutia
Na iwe ni kwamba mwanachama hata akihama mji, as long as bado ni mwanachama hai, basi akikuta nyumba za NHC ni kumuona meneja wa eneo husika na kuomba apewe nyumba ya kukaa (ni sera na mipango tu)
Ikitokea muda wa kustaafu unauziwa nyumba kwa nusu bei