Bado sijaelewa nani anaongoza CHADEMA kwa sasa

Bado sijaelewa nani anaongoza CHADEMA kwa sasa

Lizaboni

JF-Expert Member
Joined
Feb 21, 2013
Posts
33,901
Reaction score
20,416
Wadau, amani iwe kwenu.

Inavyoonekana Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe ama amezidiwa nguvu na Lowassa, au ameamua kumuachia aongoze chama au amesusa kutokana na yanayoendelea ndani ya chama hicho. Si siri tena kuwa Mbowe amepoteza uwezo wa kukiongoza CHADEMA. Na hii ni kutokana na chama kukosa ajenda ya kuisimamia hasa baada ya ajenda yao ya ufisadi kuwaelemea. Watafanyaje sasa ilhali mtuhumiwa namba moja wa ufisadi ndo anaongoza chama!

Lowassa kwa sasa anajinafasi chamani. Anapewa hadhi ya ukuu wa CHADEMA ilhali yeye ni Mjumbe tu wa Kamati Kuu. Lowassa kwa sasa ndiye anayefanya kazi ya Mbowe ya kuzungumza na Mabaraza ya chama ya ngazi zote. Ziara zake zinapewa hadhi kubwa kuliko ile anayepowa Freeman Mbowe.

Taarifa zisizo rasmi ni kwamba, harakati nyingi za CHADEMA kwa sasa zinaratibiwa kutoka Masaki na si Ufipa tena. Ufipa imebaki kuwa kijiwe cha watukanaji tu kama akina Ben Saanane, Yeriko Nyerere, Hilda Newton na wengineo.

Taarifa za ndani zaidi zinasema kuwa Lowassa anajiandaa kugombea Uenyekiti wa CHADEMA kwenye uchaguzi ujao. Azma yake ni kuona kuwa anaingia uchaguzi Mkuu wa 2020 akiwa na mamlaka yote chamani. Hataki yamtokee kama yaliyomtokea akiwa CCM.

Tusubiri tuone. Sisi nyumba ya jirani kazi yetu kuchungulia dirishani tu pindi majirani wanapogombana usiku wa manane.
 
Kuna kuwashwa kwingine si lazima pilipili ihusike...

Ndio kama hivi sasa...
Hahahahahaaaaaaaa! Wakati ule ukiwashwa baada ya kumeza Chloroquine, Asprin zilikuwa zinasaidia kutuliza hali hiyo
 
Mkuu, mbona nipo siku zote humu?

downloadfile.jpeg

rambirambi wapi?

swissme
 
  • Thanks
Reactions: PNC
Kazi kweli kweli....nashukuru sana kuto penda chama chochote cha siasa...maisha yangu raha msitarehee...wacha nione kinacho endelea
 
Hiyo aya ya mwisho ndio umeeleza ukweli wote wa jinsi ulivyo. Kweli hiyo ndio kazi yako wala hujadanganya.
Labda umesahau mahakama ya mafisadi imeshaanza kazi na kuna watuhumiwa tayari wameshafikishwa huko. Sasa inakuwaje Fisadi namba moja anadunda tu mitaani haguswi? Anaogopwa?
 
unajitahid sana kufungua thread huku unakuwa unamuwaza lowassa hiv hauwez kuanzisha thread leo ukamsifia kiongoz fulan kesho kiongoz mwngne wa chama chako yaan wewe nakufananisha na mtu kaenda kanisani kila muda analitaja jina la shetan
 
Back
Top Bottom