jiwe angavu
JF-Expert Member
- Aug 28, 2015
- 19,234
- 36,223
Wanasema unaweza ukamtoa mtu kijijini lakini ukashindwa kutoa kijiji kichwani mwake
Maana yake nini, watu wetu wengi bado ni washamba sana (wapori-porii), bado wanatambaa na mawazo ya kale vichwani mwao.
Hapa sina nia ya kumsema mwendazake na genge lake (sukuma gang) au watu wa mikoani, la khasha, hii ni kwetu sote, ata wa mjini.
Wanatekeleza mila na tamaduni bila kuhoji uhalali wake, faida zake na relevance yake katika maisha ya sasa.
Ninatoa mifano midogo katika haya yanayofanyika:
1. Kusalimia salimia watu hovyo;
2. Kulaumu watu wengine wasipo shiriki misiba au sherehe:
3. Ku force force kujuana juana tunakoishi au mitaaini kwenye hustle nakasirika zaidi nikiwa safarini, sikujui hunijui unaniongelesha nini?;
4. Kulamba viatu vya viongozi na watu matajiri au wenye umaarufu (uchawa)
5; Kusengenya watu makazini, majumbani, kwenye nyumba za ibada na kwenye siasa;
6. Ulozi, kuloga watu wasifanikiwe au kujihusisha na ushirikina na kufanya matambiko;
7. Kufuatilia mambo ya watu wengine, udaku na umbeya mambo ya kishamba sana;
8. Kuongea ongea kwa nguvu kwenye public places, hii ikiwa ni,pamoja na kuongea kwa nguvu ukitumia simu na kujiongelesha mambo yako au kuwasha simu na kusikiliza audio au kutazama video zenye sauti kali kwenye hadhara ya watu, huu ni ushamba mwingi sana;
9. Kuwasha maredio kwa sauti kubwa, majumbani, kwenye gari au boda boda, au kwenye pubs au bar huu ni ukenge sana;
10 Kutembea na wake au wapenzi wa watu ili usifiwe, huo ni ukenge mwingi sana;
11. Code za kilokole, kuvaa masuruali ya vitambaa yenye celebration au turn-ups na mashati oversize, yaani ni ushamba mwingi sana
Kuna mambo mengi sana ya kijinga zaidi haya bado yanendelea kufanywa na kuaminiwa na watu ambao ukiwaona utashangaa.
Kuna baadhi ya nyuzi nimejaribu kutoa humu JF nakupata uhalisia wa watu wetu na mitazamo yao na hiili limenifanya nitafakari uzi huu.
Watanzania wengi hawaogi na hawapaki deodorant
Heri ya sikukuu ya sabasaba. Kwa masikitiko makubwa naomba niwakilishe malalamiko yangu kuhusu ndugu zangu na wananchi wenzangu. Wengi wenu hamuogi, hamfui nguo zenu na hampaki deodorant achilia mbali perfume. Jana nilikua kwenye misongamano ya watu sehemu mbili tofauti katika jiji la Dar es...www.jamiiforums.com
Kwanini watu wa mikoani wanapenda kusalimia salimia?
Amani iwe nanyi wana JF Niko shamba kwa mitikasi ya hapa na pale, yaani kila mtu anasalimia, kwa siku unasalimiwa zaidi ya mara 200 Mambo ya kijinga sana na ni code za kigoloko sana, unakuta una mawazo yako mtu ana ku-distract halafu cha ajabu hakujui na hiyo salamu haijengi chochote. Kwa...www.jamiiforums.com
Ni Tanzania pekee ambapo ujinga unatetewa na kundi kubwa la watu
Wasalaam wana JF Katika kipindi cha miaka sita iliyopita nchi yetu ilishuhudia utawala usiofuata sheria na kutojali haki na heshima za binadamu. Watanzania wengi walikua wamekatwa mikia na kugugumia. Haki za kisiasa na kiraia ziliporwa na watu waliumizwa kimwili na kiuchumi na wengine kupoteza...www.jamiiforums.com
80% ya Wanawake Tanzania ni 'omba omba'
Wasalaam wana JF Naomba niwasilishe utafiti wangu uchwara kuhusu hawa watu. Ni reflection ya ukweli. Katika jitihada za serikali kupunguza umasikini na kuondoa omba omba hili kundi haliangaliwi, yaani wanawake na akina dada. Wana njaa kali na wanajitoa muhanga kwenye front zote. Wako...www.jamiiforums.com
Wizi wa mali za Umma ni reflection ya jamii ya watu wasiostaarabika
Kwa hasira kabisa ni wafokee wezi wote wa mali za umma. Jamii yoyote iliyostaarabika inatizama mustakabali wa vizazi vijavyo. Unapoiba pesa au mali za umma ni kielelezo cha ubinafsi kama mtu mmoja lakini kwa jamii nzima ni reflection ya kuwa jamii hiyo haijastaarabika. Vipo viashiria vingi...www.jamiiforums.com
Hii ni sehemu ndogo tu ya reflection ya uhalisia wa watu wetu unaojitokeza kwenye comments zao
Hoja hupingwa na hoja iliyo bora na si vinginevyo
Kutambika hatuachi ndio asili yetu.