Bado nampinga RC wa Geita | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Bado nampinga RC wa Geita

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Chief Lugina, Oct 10, 2012.

 1. C

  Chief Lugina JF-Expert Member

  #1
  Oct 10, 2012
  Joined: Jul 1, 2011
  Messages: 290
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Nampinga mkuu wa mkoa wa Geita kuhusu .

  Ni mda sasa tangu magari mawili madogo maarufu kama"mchomoko" yalipo gongana uso kwa uso,moja likitoka katoro jingine likitoka Geita. Huu ni mwendelezo wa ajali nyingi ambazo zimekuwa zilitokea kwenye barabara hii. Vipanya vimekuwa ni mwajiri mkuu wa vijana wengi wilayani Geita,baada ya wabunge wa Busanda na Geita kushindwa kutafuta njia ya kuwawezesha vijana wa katoro na Geita, vijana hawa wameamua kujikwamua kwa kupitia michomoko. Lakini kama haitoshi pia mkuu wa mkoa ameamua kufifisha kabisha ndoto za hawa vijana za kujipatia riziki ya kila siku.
  Ifahamike wazi kuwa mimi siungi mkono ajali wala sifurahii kuona watu wakifa kwa ajali hasa zinazosababishwa na either uzembe wa askari au dereva,lakini swali la kujiuliza ajali nchi hii zimeanzia Geita au Katoro? Jibu hapa ni hapana, je nani chanzo cha ajali hizi? Hapa unahitaji analysis kidogo,kimsingi kwa ajali nyingi Polisi ni watuhumiwa nambari one. Kimsingi hivi vipanya vinatakiwa kubeba abilia watano hadi Sitta. Lakini polis kwa uzembe/kupenda rushwa wamekuwa wakiruhusu madereva kubeba abiria zaidi ya kumi. Hivyo mkuu wa mkoa alitakiwa aanze na trafiki wake kwanza na siyo kukurupuka na kuzuia watu asiendelee na biashara yao .kimsingi RC wa Geita amekurupuka /ameshauliwa vibaya juu ya hili.karibuni imetikokea ajali ya meli lakini sikusika serikali ikikataza safari za majini. Iweje RC wa Geita akataze usafiri wa michomoko, mbunge wa Busanda kila mara anapokwenda Katoro amekuwa akiwapa fedha waendesha michomoko kwa madai ya shukurani kwa wao kutoa huduma hiyo. Lakini tangu RC aifungie hii michomoko Mbunge amekuwa bubu, anakula hata kwake Mikocheni . Nauli zimepanda kutoka 1500 hadi 3000 kwa safari ya kutoka Geita kwenda katoro.Nimekuwa siku zote nasisitiza Kuwa Busanda na Geita ni moja ya maeneo ambayo hayajawahi kupata wawakilishi,na hii imejidhihilisha mara baada ya RC kuzuia ajira za watu zaidi ya 100 kwa hoja dhaifu kabisa.
  Sasa ni dhahili Kuwa Katoro na Geita haina watetezi hivyo ndugu zangu wana Katoro na Geita ni wakati sasa wakitafuta njia mbadala ya kupambana na magamba haya kuanzia mbunge wa Busanda (Lolencia Bukwimba -CCM) na mbunge wa Geita Donald MAX-CCM.
   
 2. Fadhili Paulo

  Fadhili Paulo Verified User

  #2
  Aug 25, 2013
  Joined: Sep 1, 2011
  Messages: 3,241
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 135
  Hata kuruka mstari huwezi, uandishi gani huu? unategemea nani achangie mada kwa uandishi wa namna hii?
   
Loading...