Bado nampenda

jina baya

JF-Expert Member
Mar 12, 2014
573
377
Wasalaam wote wakubwa kwa wadogo

Nimeona leo niwashirikishe mkasa huu ulionikuta ile angalau nipate mitazamo mbali mbali kutoka kwa watu wenye uzoefu nayo, siyo mtaalam sana wa mahusiano na nina wivu kiasi.

Ni hivi;
Leo katika story na mpenzi wangu akagusia kuhusu kukutana na ex wake ambaye ni wa long time japo kwa maelezo ya mpenzi wangu huyu aliniambia hawakuwahi kukutana kimwili.

Kutokana na hofu ya kuchapiwa nikamuuliza kama bado anampenda akanijibu kwamba anampenda japo hawezi kumpa nafasi tena kwasababu ya tabia yake basi baada ya kupata jibu hilo sikuongea chochote zaidi ya kukaa kimya mpaka sasa.

Je, nifanyeje na kakiri kwamba bado anampenda japo anajitetea hawezi tena kuwa nae?

Je, ni kosa kumuuliza swali kama hilo?

Nawasilisha.
 
Chukulia kam wewe ndo x wa uyo mpenz wako mnaend kuonan nn ungefany, ukpat majibu fany maamuz
 
Unaanzaje kuuliza past past za watu
Washasema mahusiano ni kama swimming pool ustake kujua nan aliogelea wa mwisho
 
Dah... Wewe vipi bana... Mwenzio juzi tu hapa mkewe kanasia huko Kenya.... na bado anasema anampenda...
 
ningejua huko kenya ningeenda mkuu maana hata sitamani kumuacha na kutokana na hayo maneno yake imani yangu kwake imepungua kabisa for sure......
 
and of course sikupenda kumuuliza hilo swali but kwanini anijibu hivyo?????
 
Back
Top Bottom