Bado nalia na Sheria ya Bodi ya Mikopo ya 2016

FATHER OF HISTORY

JF-Expert Member
Aug 15, 2012
800
466
Bado nalia na Sheria ya Bodi ya Mikopo ya 2016.Leo nimesoma katika gazeti moja la nipashe majibu kuhusu Utekezaji wa Sheria hii.

Pamoja na mambo mengi Bodi wanasema wanakata asilimia 15 badala 8 na Retention fee inayokatwa kwa mdaiwa eti Sheria hii ilihusisha wadau ikiwemo vyama vya wafanyakazi na wao wanatekeleza kama ilivyo.
Kilio cha wanufaika ni:

1:Kubambikia watu madeni.mfano.Mdaiwa ambaye ni Mtumishi alipokea deni lake kupitia Maafisa utumishi na hao ndiyo waliidhinishwa kufanya makato na kurejesha Bodi mpka deni linaisha kupitia mshahara.

2: Maendeleo ya deni jinsi linavyopungua mdaiwa anaona kwenye salary slip yake

3 .deni likiisha mdaiwa huyu sasa anajua amemaliza deni na sasa yuko huru.

4. Je zile penalty tulizopigwa mfano,mtu alikuwa na deni halisi alilopewa kwa barua na Bodi siku malipo maliza chuo shilingi mil 6, baadae akaingiziwa kwenye salary slip mil.9, Hiyo mil. 3 iliyoongezeka ili cover vitu gani halafu mtu deni limeisha kwenye salary slip uniambie bado Retention fee?

Kama lengo ni kuongeza mapato ya serikali Labda,sna uhakika na hilo,si Bora ingepigwa tu flat rate kwa wadau wote Labda Laki tano tano ingepatikana hela kibao Kuliko haya madeni yasiyolipika?

Jambo la kusikitisha hapa ni kauli ya Bodi kuwa eti:

1 .deni la mdaiwa halihusiani na lile ambalo linaonekana kwenye salary slip.

2. deni halisi Bodi wao ndiyo wanalijua na siyo hilo la kwenye salary slip,hivyo unapewa tena deni jingine jipya

3: Eti deni lako likiisha unatakiwa kuripoti Bodi ili upewe certificate of clearance,usiporipoti wao wanachojua ni kwamba deni lako bado linaendelea .

4:Mara eti hata kama deni lako limiisha kwenye salary slip bado unadaiwa Retention fee.

Sasa Mimi maswali yangu kwa Bodi ni haya:

1:Kadiri walivyopeleka madeni kwa Maafisa utumishi ndiyo walitakiwa kupokea taarifa ya waliomaliza madeni kutoka kwa hao hao Maafisa utumishi,kwa nini hiyo hawataki wanataka Mtumishi binafsi ndiyo akaripoti Bodi?

2:Kwanini wakati wanapeleka deni la mdaiwa kwa afisa utumishi wasipeleke deni kamili pamoja na penalty zake zote zionekane kwenye salary slip?

Kwanini clearance certificate zisitumwe direct kwa afisa utumishi iliawakabidhi waliomaliza deni au mfumo u generate automatically certificate mara tu mdaiwa deni lake linapokwisha kwenye salary slip?

3:Hivi unaposema deni halisi liko Bodi ya mkopo na siyo hilo la kwenye salary slip Bodi mnakuwa mnamaanisha nini?

Jamani naomba ieleweke hivi,sote tunapenda na tunapenda kulipa deni hili la serikali kwa moyo Safi na mkunjufu,jambo ambalo hatutaki ni huo utata wa maelezo ya Bodi haueleweki.

Pili,Wadau walioshirikishwa kwenye Sheria hii sidhani kama walijua vema au walikusudia yatokee haya ya kubambikiana madeni yasiyoisha.

Bodi tunaomba fungueni dirisha maalumu kwa njia ya mtandao tutoe maoni yetu jinsi ya Kuboresha Sheria hii,kwa hivi ilivyo siyo rafiki hata kidogo.

Asante
 
Mitano tena kwa Magufuri , Magurudi oyeeeeeeeeee naomba HESLB kuongeza retention fee ifike 15% na makato yafike 45% , maendeleo kwanza watu wacha wale majani ha ha ha ha ha ha , CCM oyeeeeeeeee kuisoma namba ndio hiii sasa pigeni kelele weeee ila uku tunaibiwa na CCM wote
 
Sema hamjui tu,hawa wametengeneza tatizo hilo saizi ila tunapoelekea uchaguzi ujao 2025,mgombea atakayekuja kupitia sisiemu atakuja na sera ya kufuta au kurekebisha kabisa madeni ya sisi wadaiwa.

Kwahiyo msihangaike sana mtu ajaye anajua hali itakuwa ngumu maana hata wanasisiemu wanalia.Pia hata huyu Magu utashangaa anakuja na mkakati mpya kwa madai ya kuwaokoa wanyonge na watoto wa maskini, kuweni wapole tu soon hili jambo litatatuliwa kiaina. Kwani hii Gavamenti yetu bado tu hamjaijua? Kelele zikizidi headmaster wa nchi atalitumia hilohilo.

Ni suala la muda tu
 
Pole mkuu...

Unafikiri Magu hajui hayo..

Wacha tumalize Stiglers kwanza..

Na badoo
 
Mitano tena kwa Magufuri , Magurudi oyeeeeeeeeee naomba HESLB kuongeza retention fee ifike 15% na makato yafike 45% , maendeleo kwanza watu wacha wale majani ha ha ha ha ha ha , CCM oyeeeeeeeee kuisoma namba ndio hiii sasa pigeni kelele weeee ila uku tunaibiwa na CCM wote
lazima tuambizane ukweli hii nchi imechezewa sana au nasema uongo ndugu zanguuuu
 
"Tatizo mlizoea maisha ya dili, ndugu zangu tumechezewa sana. Nitahakikisha wale waliokuwa wakiishi kama malaika, sasa wataishi kama mashetani".
Alisikika MwanaLumumba, kigogo, huku akipiga kifua chake kilichojaa mtimanyongo.
 
Back
Top Bottom