Bado nakupenda sana

Bado nakupenda sana

Joined
Nov 25, 2019
Posts
9
Reaction score
2
BADO NAKUPENDA SANA:07
ili nipoteze muda, nikakuta voice note yaani ujumbe wa sauti kutoka kwa aliyekuwa mpenzi wangu "usinifanyie hivyo mama sahau yaliyopita au nikopeshe basi. "Safari hii hakunisumbua, alizoea akifanya hivyo mimi nachanganyikiwa mpaka nakopa kumpa yeye asiteseke wakati yeye hakuwahi hangaika kwaajili yangu mahangaiko yake ni ya kiburi na dharau hivi vitu alijaliwa kujitia anajuwa kila kitu, hivyo nako nilimpa block takatifu ndiyo nilimfungia huduma asinipate, muda wote huo sikuona chochote kitu kutoka kwa Hansy, sikuona kitu chochote kile niliamua kuupoteza muda kwa kupekua kurasa mbali mbali Instagram lakini wapi hivyo nikawaza kuzima data nilale nilipotaka kufanya hivyo ujumbe wa sauti yaani Voice note iliingia kwa namba mpya moyo ulinilipuka na nikajikuta natabasamu huku nikiupakua, ulipokua tayari nilisikiliza waaaaaaaao alikuwa Hansy, alisema "Ney mama samahani sikuwa na kifurushi cha kawaida na hapa nina MB chache sana za WhatsApp tu, nimewaza nikaona usije hisi mimi mlugaluga ikabidi nikucheki tu nikuambie nitakupigia kesho mama ili tuongeee. "Nilijikuta nacheka cheka huku nikirudia ule ujumbe kuusikiliza, nilipenda alivyokuwa akaniita mama, nikajikuta naandika ili kuujibu ujumbe ule "nakupigia" na kabla hajajibu tayari simu yake ilianza kuita, alipokea kwa sauti ya upole nami nikajikuta nadeka nikisema "nimekununia umechelewa kunipigia" Hansy alijibu "hapana mama sijapenda ila nimekupa sababu, Nisamehe bure. " Mpenzi wangu yule kichomi... Nawatakia usiku mwema, asanteni mnaonisupport kwa namna moja au nyingne Mungu awabariki katika kazi zenu binafsi nawapenda na msiache nunua vitabu vyangu Chozi la MWANAMKE na maisha bila wazazi
Screenshot_20191204-132724.jpeg
 
Back
Top Bottom