C.T.U
JF-Expert Member
- Jun 1, 2011
- 5,080
- 3,771
Ulikuwa mwanasiasa hodari, ambaye usiyekuwa na habari,
Usiyekuwa na ufahali, wala usiyejilimbikizia mali,
Mwanasiasa uliyeona mbali, ila hukuona ile ajali,
bado nakulia chacha wangwe, bado nakulilia chacha wangwe
Zamani nilikutambua, kabla ya wengi kukujua,
Kabla mnyoa kipara hujakua, ila mfuga dreds ulikuwa,
Nyerere akakuumbua, nyoa nywele halafu ubunge utakua
Bado nakulilia chacha wangwe, bado nakulilia chacha wangwe
Safari yako ilikuwa na mengi, na iliwakasirisha wengi
Kifo chako kilishtua wengi, utakumbukwa na wengi,
Chama chako kina matatizo mengi, masalia wamekuaa wengi

Hukumuogopa mtu, usoni uliwapa makavu
Ulijali utu, na kuwapa zao laivu
Ajali ilikuchinja kama kuku, bila ya wewe kula zako mbivu

Huku tunaendelea, watu wanataka uraisi
Yale uliyoyakemea yanaendelea, wengine wanageuka mafisi
Kukulilia naendelea, uliowatetea wamekumiss

Note
Sijafuata taratibu zote za uandishi wa shairi ila nimeweka katika mfumo wa shairi ili iwe na utofauti fulani