mshana jr
Usijisumbue kwa sababu hatakujibu hilo swali lako umemweka kwenye kona kali mno. Huenda huyo aliyepanda hapo hajui kazi ya paa la gari SUV kama hiyo.
Pili, huenda washauri wake hawapo au hawana akili timamu kwani kama wanamjua kuwa kaogopi kujirusha kutoka kwenye gari linalotembea hata hapo si ajabu akaamuru gari liondoke akiwa hapo ili aoneshe uwezo wa kusimama bila kujishika.
Sijui atakaaje pale magogoni ajizuie asirukie baharini kujifunza aina ya samaki waliotembelea eneo la magogoni. Jamani angalieni msijemfanya mtu akafa kabla ya wakati, haya nyiye msifuni tuu hata kwa kitu cha kijinga.
Hizi sio enzi ya zidumu fikra
Ma Samia je? Ana Mngwira je? kwanini Lowasa tu?
Tusichepuke tubaki njia kuu jee kama jukwaa ni bovu paa la gari ndio linafaa kuwa jukwaa?
Linafaa ndio mana kahutubia na mkutano ukaisha
Ngoja nikwambie hicho alichokifanya Magufuli ni kituko na ndio msingi wa hii mada na kwenye mitandao mingine ya kijamii
Let's learn to cherrish what we have...kuthamini na kujali ni dhana pana sana, kama sasa hajawa rais anafanya haya akiwa rais je?
Mkuu naona unataka kutaga sasa wiki ya mwisho ya kampeni ha ha ha! Kama imekuuma kwani msiandamane au kutoa tamko? Mambo ya Magufuli yanakuhusu nini na wewe unae mgombea wako? Mbona hatuoji utoaji wa kubwa majukwaani? First lady analewa mpaka anashikwa kalio je wakiwa ikulu itakuje?
Naona ushaanza kupaniki hii picha iko kwenye mitandao mingi tu ikijadiliwa kwa kejeli hasa....hayo mengine kama una picha zake niite tu nitachangia lakini kwasasa mada ni hii , kwahiyo tusitoke nje ya mstari
Lowassa anaweza kusimama hivyo kweli?
Kwani hiyo ndio kazi ya paa la gari?
Unadhani hiyo gari bodi lake ni kama gari lako hiyo armoured, gari la deraya.
Kazi inafanyika popote. Ili mradi watu wamepata wanachotaka. HAPA KAZI TU, NIKIWA NIMELALA NI KAZI, NIKIWA NIMESIMAMA NI KAZI, NIKIWA NIMECHUCHUMAA NI KAZI. Huo ni mfano wa kazi sasa.